Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuku na mimi kwa kuniona na kunipa nafasi ili niweze kuchangia juu ya Kamati hizi ambazo zimewasilishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wetu anahangaika sana kutafuta fedha usiku na mchana kwa ajili ya Watanzania. Kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Sasa mimi nina mambo machache sana ya kusema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja; Serikali imetafuta fedha imeanzisha Kiwanda cha Dawa kule Njombe, Makambako. Kiwanda hiki cha kutengeneza mipira (gloves) tayari kimeanza. Vilevile kuna kiwanda kingine ambacho majengo yake yalishajengwa, cha kutengeneza vidonge pamoja na syrup.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda hiki tangu kimenunuliwa na majengo yamejengwa ni zaidi ya miaka miwili na nusu ili Serikali ipunguze gharama za kuagiza madawa nje, lakini hakuna kinachoendelea, kiwanda hiki hakijaanza. Huu ni uharibufu wa fedha ambazo zimekaa tu huku Watanzania wanasubiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sipendi niliseme sana kwa sababu Makamu wa Rais alipokuja alitoa maelekezo. Sasa kupitia Bunge hili, na Kamati husika ya Bunge ilishakuja na ilizungumza juu ya kiwanda hiki; naombe kiwanda hiki kianze kama ilivyokusudiwa ili kuongeza tija ya viwanda vilivyopo katika nchi yetu. Tutakuwa tumeitendea haki Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imetoa fedha mabilioni na mabilioni kwa ajili ya kiwanda hiki, lakini zipo zimelala pale halafu, hakuna kinachoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na baadaye mitambo ya kiwanda hiki; kwa sababu haijafungwa, iko kwenye ma-box; baadaye itaonekana ni ma-scraper tu kwa sababu imekaa kwa muda mrefu. Kwa hiyo, tukuombe, Kamati inayohusika ihakikishe kiwanda hiki kinaanza kama ilivyokusudiwa. Tutakuwa tumeitendea haki Serikali ya Awamu ya Sita, ambayo imeleta fedha zimekaa tu pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, amesema Mheshimiwa Mbunge ambaye amemalizia hapa. Unajua wanasema mtu akifanya kosa anatakiwa aadhibiwe. Sasa inategemea na adhabu wanazopata watu, inawezekana wanaona kama ni ndogo. Kwa sababu adhabu zingine ni kwamba unatolewa ulipo na unakwenda mahala pengine, ile ni kama si adhabu. Mimi nadhani adhabu hii aliyoisema Mheshimiwa Waitara, hii ndiyo itatufikisha; watu wataogopa. Kutumia vibaya fedha za Serikali, fedha za awamu ya sita ambayo mama anahangaika usiku na mchana kwa ajili yetu sisi Watanzania. Kwa hiyo, nilikuwa nadhani hii sheria hebu iletwe hapa, acha ile sheria ambayo mtu akiua anatakiwa auwawe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, hii akiiba mali ya Serikali auwawe; anyongwe mpaka kufa, litakuwa ni jambo la muhimu sana. Mimi naunga mkono kabisa hoja hii kwamba, angalau itapunguza watu kuiba hela za mama ambaye anahangaika, anatuletea mabilioni na matrilioni. (Makofi/Vicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mawaziri wote walioko hapa hawalali, wanahangaika kuja kuwaambia wananchi huko kutembea kwa sababu ya fedha hizi ambazo zinaletwa za maendeleo katika nchi yetu. Sasa wanapatikana wachache wanakula hizi fedha. Ni lazima Serikali ichukue hatua ya kuona wanapewa adhabu.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE–SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Deo Sanga, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Christopher Ole-Sendeka.

TAARIFA

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kumpa taarifa Mbunge makini wa Makambako. Hatua ya kwanza ya kupambana na ufisadi huu ni kwa CCM kukubali kujitenga na wahalifu hawa. Mwalimu Nyerere amesema; “CCM iking’ang’ania umoja wa bandia na watu wasio waadilifu itaununua umoja huo wa bandia kwa gharama ya kuwekeza itikadi yake na kukubalika kwake na umma” na Mwalimu akaendelea akasema “CCM isiyo na msimamo katika mambo ya msingi itakuwa ni sawa na gulio au soko lililowakusanya watu kwa nia ya kutaka madaraka” na Mwalimu anasema “Nani anaitaka CCM ya namna hiyo?”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hatua ya kwanza ni Mawaziri wa CCM kujitenga na wahalifu ambao ni accounting officers, maafisa masuhuli walioingiza nchi hii katika janga la wizi. Namna ya kijitenga ni kuchukua hatua chini ya uongozi wa Waziri Mkuu makini, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa. Chukueni hatua, toeni maelezo hapa juu ya hatua mtakazo chukua. Vinginevyo azimio langu la mapendekezo litaendea kuwepo palepale.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Deo Sanga, taarifa unaipokea?

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, alikuwa anakazia kwa sababu ipo kwenye Ilani ya CCM, kwamba mafisadi watashughulikiwa. Iko kwenye Ilani, siyo jambo jipya iko kwenye Ilani. Ni hii tu sasa Bunge liweze kuona namna ya kutunga sheria ya kuwashughulikia hawa ambao wanaharibu hela ya mama ambayo ametuletea kwa ajili ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, juzi nimesema na sasa niseme tena; sasa niseme kwa unyenyekevu na utulivu mkubwa na upole kabisa. Tumepata heshima kubwa ya Dkt. Tulia Akson. Kwanza tunawashukuru wazazi wake kule Mbeya, pili, tunawashukuru Watu wote wa Mkoa wa Mbeya kwa kumlea kijana wetu vizuri na hatimaye ameweza kukubalika huko duniani. Tatu, tunampongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu ambaye amesimama kidete kwa ajili ya Mheshimiwa Spika wetu Dkt. Tulia Akson.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu, kwanza kwa Watanzania na kwa wenzetu wa Mbeya; waone kwamba heshima tuliyopewa ya kiongozi wetu huyu kwa kupata heshima kubwa duniani; watu wa Mbeya niwaombe, chonde, hebu tumuache huyu. Mungu ana makusudi yake na Mheshimiwa Rais ana makusudi yake. Tumuombee Watu wa Mbeya, asijitokeze mtu mwaka 2025. Mtaweka kikwazo cha mipango mikubwa ya Dkt. Tulia Akson. Bunge hili tunamuombea na Watanzania wote tumuombee Dkt. Tulia Akson kwa mambo makubwa ambayo yako mbele, Mungu ameyaweka, tusiweke kizuizi. Nimeona niliseme hili kwa dhati kabisa kwamba Mungu ana makusudi, tumuombee (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nirudie kwa Mawaziri wangu mnafanya kazi nzuri. Mmekuwa mkija kutoa ufafanuzi wa maendeleo yanayotakiwa. Mnafanya kazi nzuri chini ya Mheshimiwa Waziri wetu, Kiongozi wetu wa Seikali Kassim Majariwa Majariwa. Anasimamia vizuri shughuli za maendeleo na tunamuombea sana. Na wewe Mheshimiwa Majaliwa Majaliwa kule Luangwa; mimi kama mzee, watu wa Luangwa chonde chonde, tunamuhitaji. Msijaribu kufanya kitu chochote, hebu mmuache aweze kufanya kazi ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na Mungu akubariki. Ahsante sana. (Makofi/Vigelegele)