Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana CPA Charles Kichere, kwa kazi nzuri sana yeye na timu yake ya Ofisi ya Ukaguzi kwa uzalendo aliouonesha. Kipekee pia ni mpongeze na kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mawanda mapana ya ukaguzi na kukataa kabisa nchi yake kuwa pango la wezi, kuwa pango la wala rushwa, lakini kuwa pango la mafisadi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma taarifa ya CAG ya mwaka 2021/2022, nimesoma Taarifa za Kamati za Ukaguzi, nimesoma majumuisho ya majibu ya Serikali na Mpango wa Utekelezaji wa Taarifa ya CAG.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majumuisho ya Mpango wa Utekelezaji wa Taarifa ya CAG ina kurasa 1,111; ukizisoma zote kwa pamoja huoni hatua mahususi ambazo Serikali imechukua mpaka sasa toka ripoti ya CAG itolewa Machi, 2023, hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwahi kusema hapa niliposimama Bungeni kwamba tumepoteza zaidi, tumepigwa zaidi ya trilioni 30 katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022 na leo nasisitiza ni zaidi ya trilioni 230 na maneno haya yanathibitishwa na Taarifa ya FIU ambayo inasema zaidi ya trilioni 80 zimehamishwa ndani ya nchi na nje ya nchi, trilioni 280 na kati ya hizo trilioni 55.65 zimehamishwa fedha taslimu kupitia mipakani na maeneo mengine. Nyingine trilioni 222.81 zimehamishwa kupitia elektroniki. Sasa kama nchi hii masikini inawza kuwa taarifa shuku trilioni 280 usalama upo wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya Kamati ya PAC kipengele cha 2.2.3.2…

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Luhaga, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba.

TAARIFA

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuheshimu mchango anaochangia Mheshimiwa Mbunge ninaomba kumapa taarifa; moja ni miamala shuku ni transaction, siyo uhamisho, ni transaction zinazofanyika za private sector tu, anaweza akawa Mheshimiwa Kingu pale anaagiza mzigo wa vitenge Uganda, katuma halafu mhisani mmoja akataka kujua hiyo iliyokuwa inaenda kufanya vitenge ilikuwa nini, siyo uhamisho, ni shughuli za kila siku zinazoendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika mwezi na katika mwaka ni dhahiri kwamba shughuli lazima zinaendelea na ni nyingi kweli na hatuwezi kama nchi tukazuia shughuli za kiuchumi katika nchi. Kwa hiyo, siyo wizi wala siyo uhamisho wa fedha ambazo zinatoka Hazina ama zinatoka kwenye Idara ya Serikali kwenda mahali fulani, ni shughuli za kiuchumi na anatokea mtoa taarifa ndio anatoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu la pili, ukisema umepigwa trilioni 30 wakati bajeti ya nchi ni trilioni hatujafika hata 50 na kwenye makusanyo ya mwaka mzima takribani trilioni ishirini naa ni mishahara inaenda kwa watu n a wanaipokea na trilioni 14 zinaenda kwenye miradi ya maendeleo; ukisema trilioni 30 naa zimapigwa namba zinakataa kwenye bajeti kwa sababu bajeti ya nchi hatujawahi kufika huko. (Makofi)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifa kwamba hzi nyingine ni shughuli ambazo zinakuwa zinaendelea.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Mheshimiwa Luhaga Mpina endelea.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza anamaliza muda wangu, halafu nashangaa Waziri wa Fedha ambaye hajui kazi ya FIU. Hajui kazi ya FIU, hajui miamala shuku maana yake ni nini. Kwa hiyo, sitaki taarifa yake na aniache niendelee kuchangia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya SGR ya Kamati kipengele cha 2.2.3.2 katika lot namba 3 na lot namba 4; Kamati inakiri kwamba Serikali ilipoacha utaratibu wa njia ya ushindani ilipata ongezeko la dola za Marekani milioni 1.15 sawa na bilioni tatu kwa kilomita moja ya SGR. Kamati ina-confirm kwamba katika kipindi cha miaka mitano Serikali ilipokuwa inatumia njia ya ushindani kilometa moja ya SGR iliongezeka kwa shilingi bilioni 0.42 kwa miaka mitano. Serikali ina-confirm kwamba Serikali ilipochukua utaratibu wa single source ikaacha uataribu wa ushindani bei ya kilometa moja iliongezeka kutoka bilioni 1.4 hadi bilioni 3.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia maelezo ya kwamba gharama ziliongezeka kwa sababu ya miaka sita ilikuwa imepiata siyo ya kweli kwa sababu mwaka 2020/2021 tulitangaza tender kwa njia ya ushindani ya Isaka - Mwanza ambayo average kwa kilometa moja ilikuwa ni bilioni 9.1 sawa na kipindi kile cha mwaka 2017 kwenye lot 1 ambayo ilikuwa ni bilioni tisa. Kwa hiyo, 9 kwa bilioni 9.1 tofauti ya 0.1 tu. Kwa hiyo, tender hii ya lot 3 na lot 4 ilikuja kutangazwa baada ya mwaka mmoja tu 2020/2021 ikatangazwa mwaka 2021/2022 kwa hiyo maelezo hayo siyo ya kweli. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kwamba lot namba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mpina kuna taarifa kwa Mheshimiwa Naibu wa Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa David Kihenzile.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakubaliana anachokisema Mheshimiwa Mbunge mchango ni mzuri, lakini nilitaka pia nitoe ufafanuzi kidogo na taarifa kipi kinapelekea...

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naomba tuwe wasikivu. Waheshimi Wabunge, tuheshimu taratibu za vikao vyetu.

Mheshimiwa Naibu Waziri toa taarifa.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hii imezungumzwa kwa muda mrefu ambayo nampa taarifa Mheshimiwa Mbunge ya sababu zilizosababisha kutofautiana kwa fedha kati ya lot one na two visa vis three na four, zipo hoja nyingi. Namba moja ukingalia kwenye lot three na four ilikuwa na rift valley kilometa 50, one tu haikuwepo; ukingalia kwenye lot three na four ilikuwa na junction pale kuna karakana, kuna Chuo cha Reli, kule havikuwepo; ukiangalia three na four kuna ujenzi wa kituo kikubwa ambacho kinakwenda mpaka Kigoma na kadhalika, huku hakikuwepo, lakini pia kuna eneo kubwa la swamp…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri ahsante. Mheshimiwa Luhaga endelea na mchango wako. Taarifa hizi unazipokea?

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo ni fujo atakuja kuzungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, Kamati inakiri kwamba suala la kutumia mzabuni mmoja lilikataliwa na PPRA ambaye ndiye msimamizi mkuu wa manunuzi nchi hii, sasa Naibu Waziri huyu anaongea nini? Lilikataliwa na PPRA, lilikataliwa na Bodi ya Manunuzi. Na hawa hawakukataa tu, walikataa kwa sababu sheria za nchi haziruhusu, kwa sababu Sheria ya Manunuzi Na. 7 ya Mwaka 2011 iliyokuwa kazini wakati huo hairuhusu mambo hayo; wakakataa. Walikataa kwa sababu huwezi ukapata value for money kwa njia hiyo iliyotumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Fedha aliandika barua kupitia Katibu wake Mkuu, kutaka huo mkataba usainiwe ambao pia nao ni muendelezo wa kuvunja sheria za nchi. Lingine inasema kwamba, tulilazimika kutumia njia ya single source ili tupate mkopo wa Standard Charted. Mkopo wowote katika nchi hii unachukuliwa kwa mujibu wa sheria, hauwezi kuchukua mkopo kwa uvunja sheria za nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hoja hiyo ya kusema kwamba eti tulichukuwa kwa sababu ya mkopo huo tuliuchukuwa kwa sababu tunataka kukidhi matakwa ya sheria. Hapana, hairuhusiwi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba tano, manunuzi haya hayakuwa ya dharura na wala Yapi Merkez si kampuni pekee yenye uwezo wa kujenga reli hapa nchini …

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mpina kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Mheshimiwa Waziri wa Fedha naomba taarifa iwe fupi.

TAARIFA

WAZIRI WA FEDHA, Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitoe Taarifa ili Bunge lako lichukue kumbukumbu sawa. Hakuna mkopo wowote hapa nchini ambao umewahi kuchukuliwa kwa kuvunja sheria. Mikopo yote inayochukuliwa imepitishwa kwenye bajeti na Bunge hili na inafuata taratibu zote za ukopaji na inakuwa vetted, na hivyo ndivyo ilivyofanyika.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Mpina taarifa hiyo unaipokea?.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, akae na taarifa yake. Sasa ninaomba niende kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika hili. Moja, katika kutumia hii njia ya single source, nimeshajiridhisha kwamba ni wizi, rushwa na ufisadi tu, kwa sababu hakuna kitu kingine. Kwa sababu ukiziacha sheria ukafuata utaratibu wako, hakuna kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninapendekeza mapendekezo kwenye Kamati ya PAC kwamba, la kwanza; kufanya tathmini na kuvunja mkataba wa TRC kati ya Yapi Merkezi Lot 1 na Lot 3 na kuitangaza hiyo tender upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbwalawa, Mkurugenzi wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa, Mkurugenzi wa Yapi Merkezi na wengine wote waliohusika, wakamatwe, washitakiwe, kwa makosa ya uhujumu uchumi. (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Luhanga muda wako umekwisha, zungumza sentensi ya mwisho…