Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Augustine Vuma Holle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii, na mimi niweze kuchangia kwenye taarifa hizi mbili ambazo zimewasilishwa Bungeni leo. Awali ya yote kwanza napenda kumpongeza Mwenyekiti wangu wa Kamati Mheshimiwa Deus Sangu kwa uwasilishaji mzuri, pia, kwa namna ambavyo anatuongoza kama kamati; bila kusahau ushirikiano mkubwa ambao tunaupata kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina katika kusimamia mashirika ya umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwenye Sekta ya Utalii. Kwanza nadhani nianze kutoa takwimu. Miaka miwili iliyopita mapato ya utalii hapa Tanzania ilikuwa ni dola bilioni 1.3 kwa mwaka. Tunavyozungumza kwenye kalenda ya mwaka uliopita kwa maana ya Januari mpaka Disemba mwaka jana 2023 tumeenda dola bilioni 3.4, hiyo maana yake ni kwamba ni zaidi ya 8,500,000,000,000. Haya mambo hayajajileta, hayajatoke hivi hivi tu, ni kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya kupitia initiative yake ya Royal Tour kwa kutangaza vivutio vya Tanzania Kimataifa na hatimaye tumeweza kupata watalii wengi kiasi hicho. Leo hii tunavyoongea nchi yetu ni among of 20 best performing countries kwenye utalii duniani. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Wizara nzima kwa ujumla kwa namna ambavyo wamejipanga na kuongeza utalii Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo moja tu ambalo mimi nataka kujua. Hatujaona fikra za kimapinduzi za kuendeleza matangazo haya; kwa sababu hatutegemei kwamba kila siku Mheshimiwa Rais ataenda kufanya movie, hapana. Mheshimiwa Rais wetu ana majukumu mengi na ana kazi nyingi ambazo anazifanya lazima ninyi kama Serikali muanzie hapo alipoishia Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba mna-push mbele matangazo ya vivutio vyetu na hatimaye watalii wazidi kusonga mbele siyo kurudi nyuma, kwa maana ya idadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati tumekutana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), nasema haya kwa sababu hatujaona; wao ndio chombo ambacho kimsingi kinapaswa kuwa na mpango mkakati wa kutangaza utalii kwa ujumla kwa Tanzania nzima, lakini ukiangalia bajeti yao haitoshi. Kwa hiyo ni lazima Serikali ije na mkakati na itenge bajeti ya kutosha. Tumesema na tumeshauri kwenye taarifa yetu kwamba tunashauri hii bodi ya utalii iwe ni mamlaka ya utalii Tanzania, iwe mamlaka kamili. Vyanzo vyake vya fedha viwepo, wasiwe wanategemea OC kwa ajili ya kwenda kufanya matangazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji kuona TTB ambayo kwa kweli ina nguvu. Inaenda kufanya negotiation na matangozo na timu kubwa za mpira na michezo mingine duniani na wanamichezo na wasanii wengi Duniani ili kuhakikisha kwamba tunaongoza utalii katika nchi yetu. Bila kufanya hivyo kwa kweli tutakuwa hatujamtendea haki Mheshimiwa Rais kwa sababu yeye ameonesha njia sisi tufuate kwa ajili ya kuongeza mapato yanayotokana na utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalotaka kuzungumza ni kuhusu MSD. Hii nchi ni yetu sote tunapokaa hapa Bungeni, hili ni Bunge la Watanzania. Tunapokubaliana vitu hebu tujitahidi sasa kuvifanyia kazi. Bajeti iloiyopita tulikubaliana kwamba tunaweka uwekezaji pale MSD wa shilingi bilioni 561. Hii haikutokea kwa bahati mbaya, ni kwa sababu Wabunge wengi kwanza tulipiga kelele tukilalamika kwamba fedha nyingi za halmashauri za kununua vifaatiba ambazo zinkwenda MSD, vifaa tiba havifiki kwa wakati. Unaweza ukatoa leo vifaa mkasubiri mpaka mwaka au miezi 8.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majengo yamekamilika, Rais katoa fedha lakini vifaa tiba hakuna na dawa hakuna. Kwa nini, ni kwa sababu ya MSD. Hii nadhani tungeibadilisha jina siyo Medical Store Department sasa labda nayo tuiite Medical Agency Department; kwa sababu ina-store nini ilhali haina fedha ya mtaji ya kunani hii? Wao wamekuwa kama mawakala, ukitaka vifaa tiba unampelekea yeye ndiyo anaagiza. Kwa hiyo mambo ya shipping na vitu vingine vinachelewesha mzigo kufika. Inafaa tuwape shilingi bilioni 561, tukapitisha kwenye bajeti, lakini as we are speaking now wamepata zero kabisa. Kwa hiyo, maana yake ni kwamba tatizo liko pale pale; tunashindwa kuelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepitisha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya TANESCO, very good. Kwenye ile gridi imara wanaendele wakandarasi, kwa nini hatuwapi MSD fedha wakaagiza vifaa tiba na dawa za kutosha ili mtu wa Kasulu akitaka dawa tukanunue MSD? Siyo tuwapelekee MSD fedha waende kuagiza India, hapana. It is not fair. Hapa kila mtu anajua umuhimu wa MSD. Mimi nataka kwa kweli Serikali ije itwambie vizuri kwa nini haijapeleka fedha MSD kwa ajili ya kuweza kuwakomboa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumza kuhusu bodi za mashirika ya umma. Bodi ndizo roho, ndizo brain za taasisi za umma na mashirika ya umma. Sasa ubovu wa bodi ndio utapelekea ubovu wa taasisi husika. Umefika wakati sisi kutaka mashirika ya umma kila mara kwenye ratiba zetu. Sasa ifike mahala mchakato wa upatikanaji wa bodi members na wenyeviti wa bodi uwe ni mchakato wa wazi na ambao ni wa kiushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana wakati mwingine wanakuja wajumbe wa bodi au mwenyekiti wa bodi au mkuu wa taasisi, unafikiria huyu kapatikanaje? Inachanganya kidogo. Huo ndio ukweli. Tunaongea kwa uchungu. Anakuja mtu hata uwezo wa ku-own taasisi hana. Taasisi haijui. Hata uwezo wa ku-respond maswali kwa wajumbe hana. Anashindwa ku-own taasisi. Ni muhimu sana mchakato wa upatikanaji wa bodi members na hawa wakuu wa taasisi uwe competitive (uwe shindani).

Mheshimiwa Mwenyekiti, wako watu ambao wana uwezo, washindane. Halafu wakipatikana watano au sita mamlaka iteue lakini la sivyo tunavyoenda hivi hatufiki kwa sababu bodi ziko ambazo brain zake kwa kweli hazitusaidii, hazisaidii mashirika. Watu wamekaa hawana ubunifu wala hawana chochote, wanagawana posho na wanagawana per diem, basi. Hakuna kitu cha ajabu ambacho wanakifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu, kulikuwa na Muswada hapa, Muswada wa Sheria ya Uwekezaji. Huu ndio muarobaini wa uzambe uzembe mwingi kwenye mashirika ya umma. Sisi tunayasimamia haya mashirika kila siku. Tumeupitia ule Muswada, kwa bahati mbaya umeondolewa, lakini naiomba Serikali ijitahidi sana, kama inaenda kufanya mabadiliko sawa, lakini ituletee Muswada wa uwekezaji Tanzania. Huu Muswada ndio utaenda ku-deal na bodi za wazembe, huu Muswada utaweka uwazi na huu Muswada unaenda kusaidia mashirika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, chini ya sheria ile kama tukiipitisha tutaenda kuanzisha mfuko mkuu wa uwekezaji. Ziko taasisi nyingi, mbali na uzembe ni kwamba yako mashirika ambayo watu wako committed, bodi ziko vizuri na management ziko vizuri lakini hawana fedha kabisa. Wana mipango mizuri hawana fedha. Sasa kupitia huu Mfuko Mkuu wa Uwekezaji maana yake hawa watakwenda kupewa. Tunaona kama taasisi ya MSCL (Marine Service Company Limited), hawa wana potential kubwa. Meli zinazoleta mizigo Tanzania sehemu nyingine ziko nyingi lakini hawa wana meli kwenye maziwa tu. Hawajazuiliwa kwenda baharini, lakini hawana fedha za kununua meli kubwa. Kwa hiyo huu Mfuko wa Uwekezaji ukiwepo maana yake wanaweza kupewa fedha, siyo kukopeshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ule mfuko ulivyokuwa ni kwamba Ofisi ya Msajili wa Hazina inawekeza. Inanunua meli inawapa MSCL wanai-run halafu inakuwa inapeleka magawio Serikalini. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa kweli tuweze kufanya. Licha ya hivyo, itatoa nafasi kuokoa mashirika ambayo yako weak. Yapo mashirika ambayo yako weak na tusipochukua hatua yanaenda kufa, na kama yasipokufa yataendelea kukaa hivyo hivyo, hayaingizi chochote zaidi ya kututia hasara, kwa sababu yako mengine hata mishahara wanategemea ruzuku ya Serikali, lakini wana mipango mizuri wana-management nzuri na bodi nzuri, they don’t have money. Nani wa kuwapa hizi fedha? Benki hawakopesheki. Nani ambaye atakwenda kuwekeza pale?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu sana Serikali iende kuharakisha kwa kweli kama kuna marekebisho wajipange vizuri watuletee Muswada huu Bungeni ili uweze kwenda kusaidia mashirika mbalimbali, ni hayo tu nashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)