Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa nami niwe miongoni mwa wachangiaji kwa jioni ya leo. Kipekee naomba nianze kumpongeza Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwa ujumla, kwa jinsi ambavyo anawatendea hadi Watanzania. Hakika kila mwenye macho haambiwi tazama, kwani yako dhahiri yanaonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kuunga mkono taarifa za Kamati zote mbili na hususan taarifa ya Kamati yetu ya Bajeti kwa sababu nimeshiriki. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na wengine wote. Hakika wamekuwa wasikivu, maoni ambayo yalikuwa yanatolewa na Kamati walikuwa wanaya-accommodate kwa kiasi kikubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kuchangia sehemu ambayo nadhani yanahitajika maboresho makubwa ambayo tuyafanye kama Taifa ili yaweze kutusaidia. Kwa mujibu wa Katiba yetu ya mwaka 1977, Sehemu ya Pili kifungu cha 27(1), inatuelekeza usimamizi wa mali za Umma nchini Tanzania ni wajibu wa Kikatiba. Juu ya umuhimu wa suala hili, ndiyo maana hata mkoloni 1956 alianzisha Ofisi ya Mhakiki Mali (Stock Verification). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu imeanzishwa ofisi hiyo kuja kuwa idara ambayo imekuja kupitishwa kwa mujibu wa sheria ni mwaka 2009, miaka 53 tangu mkoloni alivyoona umuhimu wake, sisi mwaka 2009 ndipo tunakuja tunaanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Mali za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini faida na umuhimu wa kuwawezesha kitengo hiki kifanye kazi kikiwa full fragged ikiwepo sera na sheria ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mambo ambayo kama Taifa tunafanya vizuri na inawezekana accounting system iliyokuwepo wakati huo haikuweza ku-accommodate mambo haya, lakini kwa uwepo wa IPSAS accrual ni wakati muafaka kwa Serikali kuhakikisha kwamba mali zake zote zinaingia kwenye register na taasisi zote za Serikali zihakikishe kwamba wanawajibu wa kuhakikisha kwamba mali zote za Serikali zinakuwa zimeandikishwa. Kwa taasisi iliyopo ambayo bado haijakamilika sasa hivi wanasimamia mali za Serikali zenye ukubwa wa thamani ya trilioni 77.4; nini tafsiri yake? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukianza kufikiria kwa sauti, mimi siamini kwamba nchi kama Tanzania sisi ni masikini, inawezekana tunasemekana kwamba ni masikini kwa sababu uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali kwenye vitabu hauonekani. Hivi tunaonekanaje sisi masikini wakati tunajenga Bwawa la Mwalimu Nyerere, wakati tunajenga reli ya kisasa, wakati tuna miradi ya barabara madaraja ya Kigongo Busisi. Hebu naomba mniambie Serikali, siyo wakati muafaka wakuja na formular ambayo sisi itatupambanua wakati tunapoenda kutafuta mikopo hata nje ya nchi zile assets za Serikali iwe kama collateral ili tunapo bargain wajue kwamba hakika Watanzania hawa ambao fedha ambazo wamezipata wameenda kutumia kwenye shughuli za maendeleo tunavyowatazama tusiwatazame sawa na nchi masikini ambao hawana chochote, tofauti yake na pale ambapo ingekuwa fedha zinatumika kwa ajili ya recurrent expenditure, watu wanalipana allowance, lakini sisi tuna-assets ambazo zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali ni wakati muafaka wa kuja na sera na sheria ije ili idara hii iwe ni idara ambayo itaweza kufanya kazi, mali zote za Serikali ziweze kuorodheshwa. Hapa kati kati tulifanya Sensa ya Watu na Makazi, sina uhakika kama sensa ambayo tulienda kufanya inaweza ikatupa takwimu ya stock za Serikali kwamba Serikali ina mali gani leo hii tunavyoongea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unakuta kila idara ya Serikali ina mali ambazo zipo, lakini ukitaka kwenda kuzitafuta huzipati. Leo hii hata katika Taasisi ya Bunge hii ukienda ukipita huku unakuta kuna mali ambazo unajua kabisa hizi zikiweza kuuzwa walau Serikali itapata kiasi fulani cha fedha, wewe mwenyewe ni shuhuda tulitembelea TRC, tukakuta wana mabehewa mengi kweli kweli, lakini ukiwauliza kwa nini hivi vitu haviuzwi kwa sababu haviwezi kutengenezeka wanasema hatujapata idhini ya Serikali, wakati huo Serikali tunalalamika hatuna fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ifike wakati muafaka kwamba mali zile zote ambazo tunajua kwamba haziwezi kutengenezwa zikaendelea kutumika na Serikali zikauzwa na tuanze hasa kwa wale watumishi waliopo jirani wawe mnufaika wa kwanza. Hapa katikati ilitokea kuna mali ambazo zilikuwa zinauzwa, lakini anatokea mfanyabiashara ndiyo anakuja ku-compete na mtumishi, kwa hiyo, kwa vyovyote vile mtumishi hawezi kupata chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye halmashauri zetu, ukienda TEMESA, ukienda Ujenzi kuna mali chungumzima za Serikali zinageuka inakuwa kama uchafu, lakini ni fedha hizo. Naomba mnisaidie Mheshimiwa Rais, tuhakikishe fedha hizi ambazo tunaweza tukazipata kwa haraka, hivi vifaa viuzwe ambavyo haviwezi kutengenezeka ili ziweze kusaidia katika kutunisha Mfuko Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilikuwa naomba nichangie, naomba niipongeze Mamlaka ya Mapato (TRA) inafanya kazi nzuri sana, lakini ni wajibu wetu Watanzania hakuna namna ambavyo tunaweza tukapata maendeleo kama sisi wenyewe hatushiriki katika kutoa kodi. Kodi ni wajibu kwa kila Mtanzania, kutoa kodi ni wajibu, lakini niiombe Serikali katika mambo ambayo pia yanawasumbua walipa kodi ni pale ambapo mifumo haisomani. Ni vizuri Serikali ihakikishe kwamba mifumo yote ambayo wameiweka inasomana na itasaidia kuhakikisha kwamba kila shilingi ambayo inatakiwa ikusanywe inakusanywa kwa wakati na inaenda kutumika kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema machache hayo, naomba niunge mkono hoja, naipongeza Serikali, pull up your socks, it is possible kila mtu akitimiza wajibu wake. (Makofi)