Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha mwaka 2024 tumekuwa hai na salama lakini vilevile ametupa kibali cha kuhudumu katika Bunge lako hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayofanya katika Taifa letu hili, hakika Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia kwamba tumepata kiongozi mwenye maono, mwenye utu, mnyenyekevu lakini mwenye kupenda sana Watanzania wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wenzangu hil jambo ni kubwa sana, nimepata fursa ya kuweza kushiriki na Mheshimiwa Rais katika nchi mbalimbali katika mikutano, hakika inawezekana Rais wetu tunavyomwona, inawezekana hatufiki kiwango kile tunachomwona. Naomba niwaambie kwamba, duniani Dkt. Samia Suluhu Hassan heshima yake ni kubwa sana na heshima hii ni jukumu la kwetu sote na hasa tuliopewa dhamana ya kuhakikisha kwamba tunaitangaza lakini tunamsaidia kwa kadri iwezekanavyo. Ndugu zangu naomba niwaambie Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana heshima kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wasaidizi wake tunapokuwa katika mikutano mbalimbali mingine, Dkt. Gwajima anafahamu tulikuwa juzi tulikuwa kwenye mkutano lakini na mikutano mbalimbali, inafika wakati watu wana-scramble kwa ajili ya kupata picha ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Naomba tuilinde legacy hii kubwa sana Watanzania, Mungu ametupa tuweze kuitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu naomba kuwashukuru sana Mwenyekiti, ndugu yangu Kaka yangu Kiswaga, Mwenyekiti huyu ni Mwalimu na mimi bahati nzuri nilianza kufanya naye kidogo mahusiano hata kabla hajaingia hapa Bungeni. Mheshimiwa Kiswaga Jackson, Mbunge wa Kalenga Mungu akulipe sana. Mama Anna Lupembe, ndugu zangu wengine ninyi Wabunge hamjui mimi nalelewa mule, nina watu ambao wanatoa shule kwa Wizara. Ukienda pale ukienda kwa Mheshimiwa Dkt. Bashiru, ukienda kwa Mheshimiwa Iddi akina Mheshimiwa Mlenge, naomba niwaambie, Kamati hii tumepata Viongozi na Wajumbe wa Kamati wenye kufundisha. Niwashukuru sana kwa kweli kwa hekima kubwa, nami naomba niseme kwa dhati tutajitahidi kila siku kwa kadri iwezekanavyo mimi na pacha wangu hapa Mheshimiwa Aweso ambao tunahudumu katika Kamati hii moja, tutafanya kila liwezekanalo lile ambalo kibinadamu tunaweza kulifanya tutajitahidi kulifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza ndugu yangu Vita Kawawa, Mbunge mwenzangu naingia 2010, nimemkuta hapa Senior hata kule watu wa magazine wanafahamu shughuli yake pevu. Najua unahudumu katika Kamati ambayo Mama yangu yupo na ndugu yangu Mheshimiwa Masauni yupo, hakika wewe busara zako ni kubwa Mungu aendelee kukulinda hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja zimekuja, mimi nachangia hoja tu lakini kuna mtoa hoja. Ningependa na mimi kuchangia hoja hii na hasa upande wa Sheria yetu ya Mazingira. Tukumbuke kwamba mwaka 2021 tulipitisha sera mpya ya mazingira badala ya kuwa na sera yetu ya mwanzo ya mwaka 1997 tulii-review tena. Tukahitaji sasa mabadiliko ya sheria na hapa nishukuru Mheshimiwa Mwenyekiti amesisitiza na Kamati hii na hili lilianza tokea katika Kamati kwamba kutoa msisitizo wa upatikanaji wa sheria mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli sheria yetu hii imepitwa na wakati na hasa inatakiwa iendane sambamba na sera yetu mpya ya mazingira ya mwaka 2021. Jambo hili naomba niwahakikishie Kamati ni kwamba linaenda vizuri, kama nilivyotoa mrejesho katika Kamati ya kwamba stakeholders’ analysis imeshafanyika vya kutosha na sasa hivi tuko katika Cabinet Secretariat inakwenda huko mwishowe lifike katika Baraza la Mawaziri na mwisho wa siku kwamba litakuja katika Bunge letu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii imekuwa ni comprehensive sana, imegusa vitu vingi sana, maana mabadiliko yake makubwa yanagusa mpaka taasisi yetu ya NEMC lakini yanagusa mpaka Carbon Monitoring Center ambayo Wajumbe walizungumza hapa yote ipo ndani ya sheria hii. Imani yetu kubwa kwa sababu ilikuwa inataka wadau wengi waweze kushiriki vizuri tutafika vizuri na sheria hii, mimi matarajio yangu nikiwa Waziri niliepewa dhamana katika eneo hili nikimsaidia Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatamani sana sheria hiyo ndani ya mwaka huu wa 2024 tuweze kuihitimisha vizuri ndani ya Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika masuala yale ya kikanuni ya maeneo lindwa na maeneo mengine, nikuhakikishie Mwenyekiti wa Kamati kwamba utaratibu wa mchakato wa kanuni ule, nadhani kabla hatujakuja katika Bunge la bajeti hapa na mwezi wa Nne kwenda mwezi wa Sita, zile Kanuni zingine zitakuwa tayari tumeshazi-approve tayari kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maeneo lindwa na maeneo mengine yanaenda kutekelezwa vizuri katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala zima mpango wa kibajeti nimesikia kweli ni hoja ya bajeti, tunajua ni wazi kweli, bahati mbaya sana Wizara hii naomba niwaambie huko tulikotoka zamani ilikuwa na unyafuzi wa mapato hali yake ilikuwa mbaya, uki-traceback tulikotoka hali yake ilikuwa ni mbaya zaidi. Niwashukuru sana Wajumbe wa Kamati, tumeanza kidogo hata hivyo kama Serikali tumesikia na katika mchakato wa bajeti wa mwaka huu kuona jinsi gani bajeti iweze kuongezeka. Hata hivyo, Wizara hii ni mtambuka inagusa Wizara nyingine, ukizungumza suala zima la usimamizi wa mazingira na hali kadhalika kupunguza emission, ukizungumza bawa la Nyerere ambao kuna investment zaidi ya shilingi trilioni 6.5 inaenda kupata renewable energy inagusa upande wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizungumza standard gauge ambayo zaidi ya shilingi trillion 27 watu wa uchukuzi wanafahamu, ambao hii ikikamilika SGR hii inaenda kutumia suala zima la nishati ya umeme maana yake tunapunguza emission, suala zima la usimamizi wa mazingira. Kwa hiyo, ukienda katika miradi ya Waziri wa Maji, Mheshimiwa Aweso ambapo kuna uchimbaji wa mabwawa, miradi ya kilimo ambayo ni smart agriculture yote ni upande wa mazingira. Hata hivyo, sehemu ya kisera tutaenda kuhangaika jinsi gani ya kuongeza bajeti katika jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala zima la taka ni kweli na naomba nitumie fursa hii kuwaambia wenzetu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, suala la uzoaji wa takataka ni jukumu la Mamlaka za Serikali za Mitaa. Niwaambie wenzetu wa Halmashauri mbalimbali zote katika Miji yao lazima waweke utaratibu mzuri wa utoaji wa taka. Sisi Ofisi ya Makamu wa Rais jukumu letu ni kusimamia sera wao ni utekelezaji. Nashukuru kuna yale madampo matano, lakini sehemu nyingine ukienda, juzi nilipita dampo moja bado Halmashauri hata suala zima la kumpa Mkandarasi lori zuri apeleke takataka watu wanashindwa. Utakuta mtu amepewa tenda hilo lori lenyewe ni takataka, hii haiwezekani! Naomba niwaambie Serikali tutaenda kufanya kila liwezekanalo lengo ni kwamba tuweze kufika mahala pazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala zima la carbon ni kweli. Hii sasa watu wanasema vijana wa Pwani kipa katoka goli liko wazi. Hii ni sehemu kubwa ambao ndiyo maana tumeamua kusimamia kutengeneza kanuni na miongozo for the first time, Halmashauri ya Tanganyika, si muda mrefu itakusanya zaidi ya bilioni 14 ndani ya mwaka huu biashara ya carbon. Hivi karibuni nilienda pale Kiteto na Mbulu wamepoteza 4.8 billion biashara ya carbon ambayo mpaka leo hii miradi 39 baada ya mwongozo imeshasajiliwa, miradi 12 imeshapata no objection. Lengo letu ni kwamba katika mwaka huu mambo yakienda vizuri zaidi ya one billion USD dollar tutaweza kuipata kwa ajili ya kuhakikisha tunaongeza pato letu kwa nchi. Kwa hiyo, naomba niwahakikishie we are very serious naomba niwaambie kabisa tupo serious kuhakikisha mambo yanaenda mbele. Naomba niwaambie mimi sinaga jambo dogo, tutahakikisha kwamba tunapambana katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kaka yangu Mheshimiwa Askofu Gwajima ulizungumza kwa uchungu sana nimekupata, ni kweli kule kumeharibika. Naomba nikuambie juzi tulikuwa tumeongea, nilipita kimya kimya hata sijawahi kukuambia na siyo hapo mpaka nilienda maeneo ya Mtanana huko ndani, uharibifu wa mazingira ni wa kwetu sisi sote. Naomba niwaambie, pale Dar es Salaam katika mradi wa DMDP II ulikuwa na version ya kuhakikisha wanatengeneza reserve ya mabwawa makubwa kule juu upande wa Kisarawe maji yanapotoka kuhakikisha kunapunguza mtiririko wa maji katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hivyo tu ndugu zangu, ndugu yangu hapa Mheshimiwa Aweso bahati nzuri amezungumza suala zima la uvunaji wa maji, majengo yaliyopo katika Jiji la Dar es Salaam mvua ikinyesha yanasababisha uharibifu wa miundombinu. Kwa hiyo agenda ya uvunaji wa maji hasa katika majiji ni compulsory katika nchi yetu, itasaidia sana katika utunzaji wa mazingira. Kwa hiyo, Kaka mimi nimekusikia vizuri sana na watu wangu wa NEMC kule walishapita na ripoti ninayo. Naomba nikuhakikishie…

MWENYEKITI: Malizia Mheshimiwa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishie tutafanya hiyo kazi vizuri na kwa kweli mimi naguswa, miundombinu imeharibika na pale nitafika kuongea na wananchi wako kujua kwamba Serikali iko site kuwasaidia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya haya machache ya siku ya leo ninashukuru sana, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)