Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunichagua katika mwaka huu wa 2024, nitaendelea kumkwepesha Mwenyezi Mungu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nichukue fursa hii kuwapongeza wana Kamati wenzangu kwa ajili ya taarifa hii ya mwaka na kipekee kabisa naipongeza Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa mikakati mizuri endelevu ambayo inaitaka Tanzania yetu kujikwamua katika sekta mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tuliona wiki iliyopita wakati tunachangia ile Miswada mitatu ya Sheria za Uchaguzi na kadhalika, tuliona mijadala ile namna gani ambavyo ilitekwa na suala zima la jinsia na ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia. Vivyo hivyo sasa hivi hakuna namna ya kurudi nyuma, dunia imeshatekwa katika suala zima la TEHAMA na teknolojia ya habari. Kwa hiyo, nasi kama Tanzania tumeshaingia huko na napongeza Bunge letu hili, tulipitisha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Lengo la sheria ile ni kuhakikisha mwananchi mmoja mmoja anakwenda kunufaika na uchumi wa kidigitali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya initiatives mbalimbali kuhakikisha nasi tunaingia huko, na hili la sheria ni mojawapo. Naiomba sana na kuishauri Serikali, ihakikishe lile suala la digital identity linakwenda kukamilika ili mwananchi mmoja mmoja aweze kunufaika. Hatuwezi kwenda kuingia katika ulimwengu wa kiteknolojia na kunufaika na uchumi wa kidigitali kama kila mwananchi hataweza kuwa na digital identity.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mipango katika hili, niwakumbushe kulisimamia kuhakikisha Watanzania mmoja mmoja wakakwenda kunufaika na uchumi wa kidigitali. Sheria tuliyotunga ya Ulinzi Binafsi, lengo lake kubwa ni kuhakikisha taarifa za mtu binafsi zilizopo sehemu mbalimbali zinaweza kuwa accessed pamoja na kuweza kumnufaisha Mtanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano sasa hivi unaweza ukaenda benki ukakopeshwa kulingana na kile ambacho tu kinaonekana kiko ndani ya benki, lakini benki inaweza vilevile kumkopesha Mtanzania kwa kutumia fedha zake zinazopita katika simu kila siku. Kwa hiyo, hiyo ndiyo maana halisi ya uchumi wa kidigitali, nasi Tanzania na wananchi mmoja mmoja tukanufaike na uchumi wa kidigitali kwa kuhakikisha kwanza kabisa nilichokisema, digital identity inakamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili ambalo ninaishauri Serikali, zipo nchi nyingi duniani ambazo zimeshanufaika na uchumi wa kidigitali. Tutafute technical assistance, tutafute ushauri au msaada wa kiufundi, msaada wa kitaalam ili nasi tuweze kunufaika na uchumi wa kidigitali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee kabisa naipongeza tena Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri iliyofanywa na initiatives nzuri iliyofanywa kwa kuanzisha Chuo Mahiri cha TEHAMA Jijini Dodoma. Hivi karibuni tumeshuhudia Serikali ikiingia makubaliano na wadau wale ambao watatusaidia kuhakikisha Chuo hiki cha TEHAMA kinakwenda kukamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna mahali ambapo Serikali hii inafanya jambo kubwa na la maana kwa vijana wa Tanzania, basi ni Chuo hiki cha TEHAMA. Chuo hiki mahiri cha TEHAMA ni jambo moja kubwa sana ambalo Serikali hii inakwenda kulifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi wote tunafahamu kwamba dunia inakwenda kwenye hiyo inayoitwa artificial intelligence, dunia inakwenda katika robotic technology, lakini kila mmoja wetu hapa haimaanishi kwa sababu siyo mtaalam wa ICT basi huwezi kwenda kusoma kupata uelewa kuhusiana na mambo kama hayo. Kwa hiyo, Chuo hiki siyo kama Universities nyingine ambazo zinafundisha labda degree ya ICT au degree ya Computer Engineering au degree ya Information Technology, bali chuo hiki kinakwenda ku-bridge the gap. Gap iliyokuwepo katika ICT knowledge ndiyo lengo la chuo hiki. Kwa hiyo, vyuo vingine vilivyopo nchini viangalie dhamira hii kama kuipa support, siyo kama competitive kwa vyuo vingine ambavyo vinatoa course na mijadala kama hii ya ki-TEHAMA nchini. Kwa hiyo, naipongeza sana Serikali kwa dhamira yake hii kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzishwa kwa chuo hiki mahiri cha TEHAMA nchini, kunakwenda sambamba na kuanzishwa ICT hubs katika mikoa yetu, na tayari Mkoa wetu wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo inaenda kunufaika na ICT hubs kama ambavyo Mbeya itanufaika, Arusha itanufaika, Mwanza itanufaika, Zanzibar itanufaika na Lindi itanufaika. Naipongeza sana Serikali, hapa ndipo mahali ambapo tunaenda kutumia TEHAMA kuhakikisha vijana wetu wanazalisha ajira nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunakubali wote kwamba kuna watu milioni nane Tanzania wanatumia smart phones, lakini mafundi wote wanaorekebisha simu zetu zinapokuwa zimeharibika ni wapi hasa ambako wanaenda kujifunza? Hakuna mahali sahihi, wanafanya kama kwa kipaji, wanafanya kama kwa kubahatisha, lakini tukianzisha ICT hubs, hapa ndipo ambapo vijana wanaenda kujifunza na kupata uelewa mpana wa kuzalisha vifaa vya ki-TEHAMA na kufanya marekebisho ya vifaa vya ki-TEHAMA, na hapa ndipo ajira za vijana wengi zitazalishwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba sana Serikali, jambo hili la kuanzisha ICT hubs kama ambavyo hizi kanda nane zilizochaguliwa zinaenda kutekelezwa, yale malengo Serikali iliyojiwekea kuhakikisha kwamba hivi hubs zinashuka kwenye kila wilaya nchini Tanzania, yatekelezwe in a holistic approach, ionekane kwamba ni jambo kubwa kwa manufaa ya vijana wa Kitanzania, kwa hiyo, tushirikiane kuanzia katika Wizara ya Mipango jambo hili liweze kusimama, kuliko kulilia minara ya simu ambapo kila siku tunakwenda kupoteza fedha nyingi kwa kutumia simu na hatuzalishi chochote. Hayo ndiyo mambo ambayo kama Taifa tunatakiwa tuyasimamie.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili liangaliwe in a holistic approach ili liweze kutimia ndani ya muda mfupi katika Taifa letu, ili vijana wa Tanzania waweze kujiajiri wenyewe. Kwa hiyo ushauri wangu kwa Serikali ni kuhakikisha jambo hili linakwisha kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile naomba kuishauri Serikali, sasa hivi kumekuwa na tishio duniani la ku-attack critical infrastructures. Miundombinu mbalimbali ya ki-ICT inakuwa attacked, zile cyber-attacks, kama tulivyoona katika nchi ya Lesotho, Benki Kuu yao mfumo ulikuwa hacked ukawa ni shida katika suala zima la kifedha. Vilevile tuliona katika nchi ya USA, mifumo ya hospitali ilikuwa attacked. Kwa hiyo, ni lazima kama Taifa tutafute namna ya kuhakikisha systems zetu zinakuwa resilient enough against cyber-attacks. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima mambo haya yafanyike leo, tusisubiri mpaka tunakuja kuwa attacked ndiyo tunatafuta namna ya kutoka. Mifano hai tumeiona, Sri Lanka na yenyewe mifumo yake iliweza kuvamiwa na kusababisha chaos kubwa. Hebu imagine sasa hivi unaenda Muhimbili, wagonjwa wote wakiwa wamelazwa, halafu mfumo wa Hospitali ya Muhimbili uwe umekuwa attacked, maana yake itakuwa ni chaos kubwa na watu wengi wanaweza kuharibu maisha yao au maisha yao kuweza kupotea.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali ione namna ya kuhakikisha mambo haya wanayasimamia ipasavyo na utekelezaji wake unakuwa ni wa haraka.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)