Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii ya kuchangia jioni ya leo. Awali ya yote namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kusimama mahali hapa. Kipekee kabisa naipongeza Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri inayoifanya katika Taifa hili, hususan katika Ofisi hii inayoongozwa na mtu bingwa kabisa, Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa mimi binafsi nayaona matumaini makubwa ya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa kwa uwepo wa Ofisi hii ya Rais, Uwekezaji. Hakika Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anapaswa kupewa maua yake kwa uwepo wa Ofisi hii ya Rais, Mipango na Uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, specifically naiona dhamira pana na akili kubwa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hasa pale ambapo ameona ni muhimu vipaumbele vya Taifa hili kuwa fixed, kuwa pin pointed, sio kila anayekuja katika Taifa hili anakuja anatengeneza vipaumbele vyake. Hili ni jambo la busara, hekima na akili kubwa kufanywa na mwanamke shupavu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Jambo hili nakumbuka limesemwa kwa miaka mingi kwamba, tunahitaji vipaumbele vya Taifa letu viwe fixed, lakini leo tukiwa tunatimiza miaka 60 ya uhuru mwanamama, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuja kulitekeleza jambo hili, Mheshimiwa Mama Samia anastahili pongezi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kiukweli kabisa natamani kuwashawishi Watanzania kwa kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, nikitambua pia michango mingine ya viongozi watangulizi wa Taifa letu, lakini natamani miaka 60 mingine ya uhuru inayokuja Taifa hili liendelee kuongozwa na wanawake ili tuweze kupima maendeleo ya miaka 60 ya uhuru na maendeleo, miaka 120 ya uhuru wa Taifa hili, Taifa hili litakuwa limefika wapi.

Mheshimiwa Spika, naona kabisa kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inanipa mwangaza kwamba, kuna wanawake wengi wazuri kwenye Taifa hili wanaweza wakalisogeza mbele kabisa. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha njia na ameonesha maono makubwa ya kuliendeleza Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 41 wa Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji ameeleza vizuri kabisa kwamba, Serikali ilichukua vile viwanda nane ambavyo vilibinafsishwa na kuhangaika kutafuta wawekezaji. Viwanda vinne kati ya vile vimepata wawekezaji, viwanda vingine kikiwemo cha Mkata Saw Mills bado hakijapata wawekezaji.

Mheshimiwa Spika, naomba sana kuikumbusha Serikali kwamba, jumla ya viwanda vilivyofungwa Mkoani Tanga ni 15, wakati Serikali inatafuta namna nzuri ya kuboresha uwekezaji nchini, pamoja na kutengeneza sera, pamoja na kupitia Sheria, naona ipo haja ya Serikali kuhakikisha inakaa chini na wawekezaji ambao wamevifunga viwanda vyao kule Tanga na wapo tayari kuvifungua, ili kuja na solution ya pamoja kuhakikisha viwanda vile vinafunguliwa. Viwanda vingine ni vipya kabisa, sitaki kuamini, sijawa convinced na logically it does not imply kwamba, watu wamefanya investment kubwa bila kufanya tafiti ya kutosha. Sisi Tanga tunazalisha ngano, kule Lushoto tuna mashamba ya ngano, haiwezekani kiwanda cha kuzalisha unga wa ngano Pembe Flour Mills kiwe kimefungwa within very short period of time, inaonesha ni failure ya Serikali katika uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna viwanda vingi, sisi Tanga tunazalisha mkonge, inakuwaje kiwanda cha mabusati Tanga kifungwe? Vilevile tunazalisha nyanya, inakuwaje kiwanda cha kuzalisha nyanya kule Bumbuli kifungwe? Naiomba Serikali na natamani sana kusikia tamko la Serikali wakati wanakuja ku-wind up, watuambie mpango wao katika kuhakikisha wanakaa chini na wawekezaji walio tayari ili kuhakikisha viwanda vile vilivyofungwa Mkoani Tanga vifunguliwe na viweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali, lakini vilevile kuna haja ya kuona umuhimu wa kufanya tafiti za kina ili kujua ni kwa nini viwanda hivi vilifungwa. Imagine katika mkoa ambao tumefanya investment kubwa ya bandari, ili meli kubwa zije ina maana ni lazima production iwepo, ni lazima viwanda vifanye kazi. Nina hakika miaka ile ya 80 kwa Mkoa wa Tanga kuwa na viwanda hivi vingi, kivutio kimojawapo kilikuwa ni bandari. Mtu anazalisha kiwandani, anapeleka mzigo bandarini unaondoka.

Mheshimiwa Spika, katika mkoa huu tumefanya investment nzuri, Serikali ni lazima ione namna, ili return of that investment iende simultaneously, ni lazima tuchochee na vilevile kuhakikisha viwanda vinafufuka na raw materials ambazo zipo Tanga ziweze kuwa processed kwenda kwenye products badala ya kuviacha viwanda hivi vife. Viwanda 13 kufa, ni vingi sana, Tanga Jiji peke yake kuna viwanda sita; Tip Soap Industries kimekufa, Gofu Mats kimekufa, Sandali Wood kimekufa, Play and Panel kimekufa, Bajader Packaging kimekufa, Usambara Drinking kimekufa, Usambara Factory kimekufa na Mkata Saw Mills ndicho ambacho wanasema wanakitafutia uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, viwanda vingine ni Kilindi Industrial Cooperative kimekufa, Derema Division ya chai, Namunga Division ya Muheza, Sange Salt cha Pangani vyote hivi vimekufa. Wakati tunaweka mipango ya kusema tutatumia uchumi wa blue vizuri tunaruhusu Kiwanda cha Kutengeneza Chumvi Pangani kinakufa. Kwa kweli, inaleta contradiction namna ambavyo tunaunganisha mawazo pamoja ili tupate yale matokeo tunayoyahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kipekee naipongeza Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo naona kabisa wanataka kuwekeza katika human capital, hili ni jambo la kupongezwa. Tunapozungumzia investment ni lazima tuone namna human capital nayo inakuwa na ubora gani. Ndugu yangu pale alivyoitaja DIT akanikumbusha usemi au tunaita University Motto or Institute Motto ya DIT inasema hivi “In Every Skilled Hand there is an Innovative Mind”. Kama hatuwezeshi vyuo vyetu kufanya fanya, there is no innovation that can happen in our country.

Mheshimiwa Spika, kwa nini Serikali inaamua kuondoa mafunzo ya katikati, yale tunayaita study tours, ili kuweza kuboresha productions, ili kuboresha uhamishaji, tunaita mafunzo ya kisayansi katika uzalishaji, kuhamishia mafunzo ya kisanyansi katika uzalishaji. Ni lazima tuweze kuzalisha na tuweze kuhakikisha watu wanawezeshwa kufanya fanya zaidi, lakini wanafunzi wetu hawawezeshwi kufanya fanya. We must help our kids from the very early age kuweza kufanya fanya na hili linahitaji investment ya muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kuainisha tips hizi ambazo zinatumika kuanzisha shule 100 za amali, its good initiatives, hususan kwa huu mtaala mpya wa elimu ambao unataka vitendo zaidi. So, it is also a good initiative, lakini ndani yake kama itakuwa more theoretical na hakuna kufanya fanya, frankly speaking hatuwezi kuhamishia maarifa ya kisayansi katika uzalishaji, lazima wanafunzi wawezeshwe kufanya fanya. Serikali ipange kurudisha zile study tours kwa walimu na wanafunzi wao, ili waweze kwenda kwenye maeneo ambayo mambo yanafanyika kwa vitendo na wanafunzi waweze kujifunza siyo kusubiria tu industrial practical training mpaka akitimiza mwaka mmoja wa chuo haitoshi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakuona unacheka Rais wa Dunia. Ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mwanaisha Ulenge nilikuwa najiuliza ni sentensi inakuwa ndefu ama, hiyo kufanya fanya ni nini? Kufanya fanya ni nini, ili Taarifa zetu Rasmi za Bunge zikae sawasawa? Maana umelirudia sana hilo neno, kufanya fanya nini?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namaanisha mikono yetu iwe imetengenezwa kuweza kufanya hands on practices like that. Yaani ile, sijui kama nimeeleweka? I am sorry, ile mazoezi kwa vitendo.

SPIKA: Haya. Kwa hiyo wajifunze kwa vitendo ama?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, wajifunze kwa vitendo lakini ni ili...

SPIKA: Kujifunza kwa vitendo ama kujifunza huku wakifanya kazi, wakifanya jambo fulani?

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, what can I say. Ni ile hali ya, yaani natamani mtoto kuanzia akiwa mdogo, anapokuwa nyumbani mpaka akiwa kwenye level za vyuo aweze kuwa trained katika hali ya kupenda ku-practice kufanya fanya. (Makofi)
SPIKA: Haya ahsante sana. Mheshimiwa Almas Maige naona unataka kuzungumza, lakini usituangushe kama mara ya mwisho nilikupa kazi ya kutupa neno kwa Kiswahili ukatupa ambalo halipo kabisa kwenye kamusi. Haya tusaidie, kufanya fanya ni nini?

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, kwa sababu mimi nimefanya fanya pia, maana yake ni kazi za mikono. Ni kazi za mikono, ndiyo kufanya fanya, anamaanisha hiyo.