Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kuungana na Watanzania wenzangu wote kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia baraka zake mbalimbali katika Taifa letu kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kuungana na viongozi wenzangu wote kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali nzima ya Awamu ya Sita kwa jinsi wanavyoliongoza Taifa letu na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2020 hadi 2025.
Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax - Waziri, Katibu Mkuu, Makamishna Waandamizi, watendaji wote vikosini kwa kuendelea kuilinda nchi yetu wakati wote, hongereni sana na Mwenyezi Mungu awabariki.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha nampongeza sana Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na Wajumbe wake wote kwa jinsi walivyotimiza wajibu wao, hongereni sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba kutoa mchango wangu kupitia mapendekezo ya bajeti ya Wizara hii muhimu sana ya ulinzi na usalama iliyowasilishwa hivi punde na pande zote mbili kwa maana ya Wizara na Maoni ya Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaiomba sana Serikali yetu ijitahidi kupeleka fedha zote zinazoombwa kwenye bajeti ya Wizara hii muhimu sana kwa ajili ya kufanikisha mpango wake wa mwaka 2024/2025 ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Aidha, Serikali iangalie utaratibu wa kuwapatia nafasi za ajira vijana wote wanaohitimu mafunzo kutoka JKT nchini kwa kuangalia utaratibu wa ulinzi katika sekta binafsi hususan maeneo ya biashara na huduma ili kuleta msawazo wa idadi, viwango vya mishahara kwa kuangalia sera ya walinzi kwenye maeneo kama hayo kwa kuwa kwa sasa wanaolinda wengi wao ni wazee sana na wengine hawana ujuzi, lakini pia mlinzi mmoja hulinda eneo kubwa zaidi ya uwezo wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iangalie uwezekano wa kufungua ofisi za Suma-JKT katika makao makuu ya mikoa na wilaya zote nchini ili kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wote waliohitimu mafunzo yao hali itakayopunguza idadi kubwa ya vijana wetu hao mtaani.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali iangalie upya utaratibu wa kuwapatia vyeti vya uhitimu vijana wote wanaohitimu mafunzo yao ya mgambo katika wilaya zetu ili kutoa hamasa kwa vijana na endapo mhitimu ana sababu za kutokupewa cheti wahitimu waambiwe wazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali isimamie suala la kudumu kwa kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yanayopakana na makambi ya majeshi yetu na wananchi kote nchini ili kudumisha mahusiano mazuri kati yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kwa umuhimu naendelea kutambua mchango wa vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja 100% na naomba kuwasilisha.