Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Spika, naomba kutoa mchango wangu wa maandishi kufuatia kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nampongeza Dkt. Doto Mashaka Biteko na timu nzima kwa kazi nzuri na yenye matumaini makubwa kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ngorongoro imekuwa na tatizo kubwa la kukatika umeme kila siku na hata kudumu kwa siku Nzima, ninaiomba Wizara itafute suluhu ya changamoto hii ili wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro waweze kujikita kwenye shughuli za uzalishaji bila kukwamisha.
Mheshimiwa Spika, naomba wananchi wa vijiji vya Wilaya ya Ngorongoro waunganishiwe umeme kwa bei elekezi ya shilingi 27,000 kwani wananchi hawataweza kuunganishiwa umeme kwa bei ya shilingi 515,000 kwa nguzo, wananchi wengi wameshindwa kuunganishiwa umeme kwa sababu ya bei ya nguzo kuwa kubwa ukilinganisha na uwezo wa wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ipeleke umeme kwenye Kijiji cha Pinyinyi ambacho mpaka sasa hakijapata umeme na wananchi wetu wanaona kama wametengwa, kwani umeme umefika kwenye eneo la Kitongoji cha Masusu badala ya makao makuu ya kijiji ambapo ndipo kuna mji.
Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara ianze utekelezaji wa mradi wa umeme kwenye vitongoji 15, vitongoji vya Mijitu, Bwelo, Kirangi, Katoregani, Magunkune, Luselebwe, Madukani, Orkiu Juu, Embulmbul, Lopolun A, Site A, Soitsambu, Esero, Embaash na Kapongoni.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.