Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

Hon. Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi hii nichangie hoja binafsi ya Mheshimiwa Tarimo.

Mheshimiwa Spika, kwenye hoja hii naomba niwe clear, ninaunga mkono baadhi ya items kwenye hoja, lakini siungi mkono general ya hoja nzima, nadhani nimeeleweka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaungana mkono na Mheshimiwa Mbunge kwamba Jeshi letu la Zimamoto linakabiliana na changamoto nyingi na kwa mfano pia kwenye jimbo langu hivi karibuni tumepata majanga mawili ya moto lakini kutokana na changamoto ambazo ziko Jeshi letu la Zimamoto, changamoto hizo zimeshindwa kuhudumiwa kwa wakati unaostahili kuna basi liliungua Zimamoto hawana gari la kuzimia moto, lakini hawana askari wa kutosha lakini kuna nyumba ya mwananchi wangu iliungua. Kwa hiyo, ninamuunga mkono Mheshimiwa Tarimo kwamba Jeshi letu lina changamoto kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, changamoto ambazo zinakumba Jeshi letu la Zimamoto, moja ni upungufu wa askari wake, mbili, mitambo ya kuzimia moto, tatu, fire hydrants au vituo vya kujazia maji, ya nne upungufu wa magari ya administration, tano, ujenzi holela, sita fire detector huko mitaani.
Mheshimiwa Spika, hata kama tuna hizi changamoto sioni kama ni busara kuiongezea halmashauri zetu jukumu hili kubwa na zito. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, changamoto ipo, lakini sioni kama ni busara jukumu hili zito kulipelekea halmashauri zetu, lakini kama kuna halmashauri zinao uwezo wa kununua magari ambapo kuna baadhi ya halmashauri zimekwishakufanya hivyo, basi zifanye hivyo. Kama kuna watu binafsi au kuna taasisi ambazo zinaweza kusaidia Jeshi letu la Zimamoto zifanye hivyo kuliko kuongezea halmashauri zetu kazi hii kubwa ambayo hawataiweza na pia hii ni kazi ya kitaalamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nitumie muda huu wa kwangu uliobaki kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyopambana, dakika zangu tano bado.

Mheshimiwa Spika, moja tunashukuru Serikali yetu kupitia Jeshi letu la Zimamoto linakabiria kupata fedha zaidi ya dola milioni 100. Fedha hizi zinaenda moja kununua magari zaidi ya 150, fedha hizi zinaenda kununua helikopta, fedha hizi zinaenda kununua boti kwenye bahari zetu na maziwa yetu ambayo vifaa hivi vitaenda kuongezea nguvu kwenye Jeshi letu la Zimamoto. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba Serikali iweze kuzidi kulipa nguvu Jeshi la Zimamoto ili liweze kupambana na majanga haya kuliko kuchukua majukumu yake na kuwapa halmashauri ambayo kitalamu hawana uwezo, hawana watalamu wa kuweza kufanya hivyo, wakati tuna Jeshi ambalo lina watu wako trained, tuna Jeshi ambalo lipo mahususi kabisa kwa ajili ya kupambana na majanga ya moto.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi ninachotaka kuchangia hapa kweli hoja ni nzuri, lakini siungi mkono hoja kanakwamba kazi hii kubwa ipelekewe halmashauri zetu, badala yake Serikali iongezee nguvu Wizara yetu kupitia Jeshi la Zimamoto ili iweze kufanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kwa hilo. Kwa hiyo siungi mkono hoja kwamba halmashauri zetu zipewe jukumu hili kubwa, ahsante sana. (Makofi)