Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

Hon. Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kwanza niseme mimi naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Tarimo na naunga mkono kwa sababu hata tukisema kwamba Serikali leo inaleta gari moja kila halmashauri, bado umuhimu wa sisi halmashauri zetu hasa zenye uwezo na ambazo miji inatanuka kwa kasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kuchukulia mfano wa Mji wa Geita, Mji wa Geita una watu takribani 400,000. Kwa hiyo, hata kama Serikali italeta leo gari la zimamoto ule mji unahitaji zaidi ya gari nne za zimamoto, kwa sababu haiwezekani mkawa na gari moja ambalo yakitokea majanga mawili au likitokea janga likiishiwa maji ikimbie ikazime, irudi ikimbie ikazime. Kwa hiyo, naunga mkono hoja kwa mantiki kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zenye uwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niweke kumbukumbu sahihi hapa tusije tuka-shift burden, kwa sababu katika mazingira ya kawaida upo uwezekano ukiliingiza ukaleta sheria, ukaliingiza kwenye kulifanya kuwa la lazima kwenye halmashauri, zipo halmashauri makusanyo yake kwa mwaka ni shilingi bilioni mbili. Gari moja la zimamoto ni shilingi bilioni moja, lakini changamoto kubwa ninayoiona ukiliweka suala hili kuwa la lazima, hizi halmashauri hazina namna ya kukwepa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tusi-shift hii burden, Serikali iendelee na wajibu wake, kwanza kutambua maeneo ambayo kwa kweli yanahitaji kufanyiwa marekebisho kwa mfano miundombinu. Kwa ujumla miji mingi inajengwa yaani inajengwa tu kama vile jambo hili halijulikani. Let us take this issue in a holistic and realistic yaani tuichukue kwa upana wake mkubwa tangu kwenye mipango miji, hao zimamoto wenyewe hawapo, wengine hawana ofisi, ukiwakuta hawana gari yaani changamoto ni nyingi kuliko gari la zimamoto. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali isikwepe huu mzigo, iendelee kushughulika nalo, lakini halmashauri zenye uwezo tuangalie namna tunavyoweza kununua vifaa na kuwakabidhi ili waweze kushughulika nalo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakuunga mkono na naunga mkono hoja. (Makofi)