Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nikianza na kilimo cha umwagiliaji kiwe ndiyo uti wa mgongo wa Wizara na Kilimo badala ya kutegemea mvua za kudra ya Mwenyezi Mungu. Kilimo kiwe cha kisasa kwa kukibadili kutoka jembe la mkono mpaka kilimo cha zana za kisasa mfano matrekta na zana nyingine. Pia kuwe na vituo vya zana za kulimia vijijini vinavyoweza kukodishwa na wakulima. Nashauri mbolea zifungwe katika mifuko ya kiasi cha kilo mbalimbali ili wakulima wanunue kiasi wanachohitaji na kumudu.

Mheshimiwa Spika, katika Kijiji cha Majengo, Kata ya Ikongolo Uyui kuna mradi wa kusanifu bwawa la umwagiliaji, tafadhali wananchi wana mategemeo makubwa na bwawa hili, mradi huu uendelezwe kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.