Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, Serikali itafute soko la uhakika la zao la mahindi Ludewa, pia Serikali ijenge maghala ya kuhifadhia mahindi Ludewa na mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji yanayojengwa Ludewa yaweze kupandwa samaki. Pia Serikali iwekeze sana eneo la uzalishaji mbegu na isimamie ufungashaji ambao utaepusha utengenezaji wa mbegu fake hasa mbogamboga na mahindi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mbegu ya mahindi ya Pana 53 imefanya vizuri sana Ludewa na Ruvuma ila inazalishwa Zambia. Serikali ifanye utafiti wa mbegu hii, izalishwe na kuhakikisha inapatikana kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu TFRA wawe na ofisi ngazi ya mikoa, wananchi wanaipongeza sana Serikali kwa kufungasha mbolea kilo 25 na wanaomba iwepo ya kilo 10 na kilo tano.