Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, kwanza niipongeze Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu Wizara ya Kilimo kwa kuongeza bajeti. Hii inadhihirisha kuwa Serikali imedhamiria kuinua wananchi walio wengi kwani tunafahamu kilimo ni uti wa mgongo.
Mheshimiwa Spika, ushauri wangu, upimaji wa usalama wa vyakula nchini katika masoko ya ndani kwa ajili ya mabaki ya sumu (residuals) inayotokana na mbolea, madawa na wanyama kutokana na matumizi holela ya viatilifu na madawa ya mifugo ndiyo inahatarisha afya za Watanzania. Napendekeza kuwekwe vifaa vya upimaji katika masoko yote nchini na utoaji wa elimu ya matumizi ya viatilifu na madawa ya mifugo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu masoko, bado kuna haja ya Serikali kuangalia namna ya kusogeza karibu upatikanaji wa masoko kwa wakulima. Katika hili nishauri kuwepo na mawasiliano ya karibu na Wizara nyingine na Serikali iangalie suala ya miundombinu maana kama tunavyojua kwa sasa barabara ni mbovu, wananchi watashindwa kusafirisha mazao yao.
Mheshimiwa Spika, nawasilisha.