Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, nami pia nachukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mmoja wa wachangiaji katika hotuba hii ya Wizara ya Uchukuzi. Kipekee naungana na wenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika Sekta hii ya Uchukuzi, hasa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika Shirika letu la Ndege la Air Tanzania, tunaona ndege ni nyingi kweli kweli, sasa hivi karibu regional routes hizi ndege zetu zinafika kwa sehemu kubwa kwa majirani zetu na tunafanya routes za hapa.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la SGR pia naungana na wenzangu ambao wametambua mchango mkubwa, huu ni uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita, chini ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pia, uwekezaji mkubwa ambao umefanyika katika bandari, maana mwaka jana wakati wa bajeti gati Na.8 mpaka 11 bado yalikuwa na urefu wa kina cha mita 11 na kwa taarifa nilizonazo tuliposimama hapa leo tayari zile gati zimefika kina cha mita 15. Kwa hiyo, faida kubwa ambayo tunaiona vina hivi vilivyoongezwa, maana yake tumepunguza zile meli ndogo za kontena 2,500, sasa hivi tunapokea meli kubwa za kontena mpaka 6,000. Kwa hiyo ni advantage kubwa, nikimaanisha kwamba mizigo inakuwa mingi zaidi ambayo inapita katika bandari yetu.
Mheshimiwa Spika, kwa wale ambao wamebahatika kupita Dar es Salaam, naweza nikasema jinsi tulivyojitangaza na yale ambayo yanafanyika hasa kuvutia wenzetu wa nchi jirani wanaopitisha mizigo hapa na ndani pia biashara zinavyokuwa, naamini sasa hivi meli ni nyingi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi cha nyuma ulikuwa unaweza ukakaa ukaona mzigo labda unafika ndani ya wiki mbili, kutakuwa na delay, lakini sasa hivi meli ni nyingi, nimejaribu kufuatilia, ni low season lakini meli zinafika mpaka 35 ambazo zipo kwenye foleni. Kwa hiyo, tunategemea tutakapofika high season kuanzia mwezi Agosti, Septemba mpaka mwezi Novemba, huenda inaweza ikawa double mpaka meli 70 na kuendelea. Kwa hiyo, haya ni mafanikio makubwa, maana yake revenue yetu kupitia bandari inaenda kuongezeka hasa kwenye upande wa forodha, ukusanyaji wa kodi na mapato mengine yanayotokana na bandari. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kipindi tunayaona haya yote, mfanyabiashara always huwa ni mtu wa haraka kwa sababu ana commitment zake, anayo mikopo na kadhalika na anatakiwa ahudumie wateja, kwa hiyo, kila kimoja kinakuja na advantage yake na disadvantage pia.
Mheshimiwa Spika, tukijaribu kuangalia conjunction hii imesababisha sometimes meli zina-delay mpaka wiki tatu, nyingine huenda zinaenda zaidi kwa sababu muda wa kushusha meli moja sasa hivi ni siku tano, sasa tumesaini mikataba ya DRC kuanza kupitisha mizigo yao hapa kwenda nje. Sasa ukipiga hesabu ya meli moja kushusha mzigo kwa siku tano, nyingine ije ipakie, huenda meli moja inaingia kwenye gati itakuja kutoka baada ya siku nane au siku tisa, kwa hiyo ni lazima, hatukwepi suala la uwekezaji kwenye habari ya bandari. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile ni lazima TPA awezeshwe, aongeze magati mengine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilivyofuatilia bei ya kujenga gati moja siyo kubwa, ni dola karibu laki moja au bilioni 250. Sasa ukipiga hesabu uwekezaji wa gati kama 10 ni almost 2.5 trillion. Sasa ukiwekeza 2.5 trillion kwenye gati 10 na gati moja kama utaangalia average ya mapato tofauti na yale mapato ya forodha tumekuwa tunaenda mpaka trilioni 13. Kwa hiyo, ukifanya average kwa gati 11 tuliyonayo ni almost kila gati inakuingizia trilioni moja. Ukijenga gati nyingine 10 una uhakika wa kupata siyo chini ya trilioni 10 kwa mwaka, maana yake mapato yataongezeka.
Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali, Mheshimiwa Waziri yuko hapa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha yuko hapa, Kamati imesema kwenye habari ya wharfage, tunaomba hili jambo liangaliwe na TPA wawezeshwe, kama inawezekana watafute mikopo katika mabenki, wafanye uwekezaji wa gati 10 kwa mara moja au hata zaidi ya 10 ili ziweze ku-accommodate ile mizigo, kwa sababu foleni inavyozidi kuwa kubwa, mtu akaona anacheleweshewa mizigo maana yake ata-opt kwenda sehemu nyingine hatimaye tutapata hasara na hata yale mambo mazuri tunayoyatarajia hatutaweza kuyaona. Kwa hiyo, tunaomba jambo hilo walione, taarifa ya Kamati imesema, Mheshimiwa Waziri, alichukue ili waweze kwenda kulifanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, ukimwambia tena Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu akatafute tena pesa akope awape, kesho wakishindwa kulipa ni commitment nyingine tena, tutaanza kumhangaisha hapa. Maana atakuwa anakimbizana na barabara, reli na kila kitu kinamwangalia yeye, kwa hiyo, kama wanafanya biashara na wanao uwezo wa kujiendesha wenyewe, tuone kama tunaweza tukawarudishia hii pesa wakaingia kwenye business wakakopa, hatimaye wakaweza kufanya rejesho Serikalini na wakajiendesha wenyewe, the way ambavyo wanataka kujiendesha.
Mheshimiwa Spika, nahama hapo naenda kwenye habari ya SGR. Nimeipongeza sana habari ya SGR lakini sasa nimwombe Mheshimiwa Waziri, sina shida na haya yanayofanyika, ni mazuri sana, lakini kitengo chenu cha mawasiliano aidha kupitia TRC au Wizarani hawako-active kwenye kupambana na haya mambo. Kipindi cha nyuma tuliona picha za ajabu ajabu zinatumwa, watu wanaambiwa mabehewa mabovu, wanaambiwa hiki na hiki, lakini ukiangalia picha ambazo Mheshimiwa Waziri ameweka kwenye front page ya hotuba yake ni picha za Kituo cha SGR cha Dodoma, huenda watu wanajua tu kile kioo cha Dar es Salaam hawajaona jengo la Dodoma lilivyojengwa, hawajaona mpishano wa zile reli ambavyo umefanywa kwenye picha kama hizi.
Mheshimiwa Spika, tunaomba Serikali, vitengo vyao vinavyotoa taarifa, propaganda ni nyingi na hasa tunavyoelekea kwenye uchaguzi, watusaidie watu kwenda kwenye mtandao wa twitter wakaajiri vijana wenye uwezo wa kujibu mle, kunashindikana nini? Tunaomba Serikali waweze ku-counter attack. Kila upotoshaji unapotokea wawe na watu active wa kusaidia. Mambo makubwa yanafanyika, lakini bahati mbaya sana upande wa Serikali hawawahabarishi wananchi mpaka itokee taharuki ndiyo wanakuja. Wafanye wananchi wajue uwekezaji mkubwa kwa kuona kwa picha, wajue pesa hii ya kodi yao inapokwenda, hatimaye hata wao waendelee kuiunga mkono Serikali. Hata Mheshimiwa Rais anaposemwa vibaya kwenye mambo mengine, wasimame naye kwa sababu wanaona na wanajua kinachofanyika. Naomba hilo nilisisitize ili muweze kulifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kagera hususani Wilaya ya Biharamulo, kwenye mpango ambao Mheshimiwa Waziri anajua plan za TRC zipo, bado naendelea kusisitiza, reli ya kutoka Isaka kupitia Nyakanazi - Biharamulo, iende Rusumo na hatimaye iingie Kigali, tunaomba wazidi kuangalia possibility ya kutuunganisha na sisi pia, maana ndugu zetu wengi sana wamekufa huko, kwa sababu magari yanayotumika kuja mpaka Isaka kwenda sehemu nyingine ni left hand.
Mheshimiwa Spika, unakuta mtu anaye-drive gari kutokea Rusumo kupita Biharamulo mpaka afike Isaka kubeba makontena, nchini kwake anaendesha kwa left hand, sasa huyo mtu sometimes akishafika anaona barabara mita 500 mbele kuna nini, huwa wanahama wale watu. Sasa wewe ukimwona unajua labda amehama atarudi kumbe yeye ameshaingia kwenye driving ya nchi yake, hatimaye wanatusababishia ajali na vifo vingi sana kule. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutakapozuia kwa kuhakikisha mizigo mpaka inavuka border; kwanza tuta-facilitate CFR, kama ni CIF iwasogelee kule na ni sehemu ya SGR kutumika. Pia, tunaokoa barabara na ajali nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikitokea na kutusababishia vifo hasa watu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani. Kwa hiyo, niombe Waziri aendelee kuliangalia kwa sababu, uchumi tunavyozidi kuujenga tukisambaza reli kila sehemu advantage yake unaiona, tutaenda kufanikiwa.
Mheshimiwa Spika, nimepongeza Air Tanzania na nikasema mambo mazuri ambayo wanafanya, uwekezaji ambao unafanywa na Mheshimiwa Rais. Wenzangu walisema hapa asubuhi, sisi watu wa Kanda ya Ziwa tunajiuliza huwezi kuwa na Capital City kama hii ambayo shughuli zote za Serikali zinafanyika hapa, halafu the only way ya kuja Dodoma kwa ndege mpaka upite Dar es Salaam. Mtu wa Kagera au Mwanza, leo akitaka kuja Dodoma kwa ndege aende mpaka Dar es Salaam ndiyo arudi hapa, not less than 1.4 million. Hiyo ni nauli ya kwenda Dubai na kurudi, wewe utoke pale Kagera kuja hapa this is not fair.
Mheshimiwa Spika, sasa tuombe kwa Mheshimiwa Waziri yuko hapa, najua bado wanaweza wakapanga route nzuri maana ni idea kama watanyanyua ndege kubwa ikaamka asubuhi, ile ya Mwanza – Dar es Salaam iendelee kuwepo. Sasa hivi tuna Boeing Max nyingi tu, ikanyanyuka moja asubuhi ikaja Dodoma, ikatoka Dodoma ikabeba abiria ikapeleka Mwanza na the same ikatoka Mwanza ikarudi Dodoma, ikatoka Dodoma ikarudi Dar es Salaam. It’s a very easy route. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kinachotakiwa kufanyika, Mheshimiwa Waziri ile ndege haiwezi kutua kwenye Uwanja wa Dodoma, impact yake na uzito wake ni mkubwa, huu uwanja utaharibika, ndiyo maana haiwezi kutua hapa. Waziri amesema kwenye taarifa Uwanja wa Msalato uko fifty something percent. Kama kweli uko hapo na runway iko sawa aweke ma-tent pale watu waanze kutua. Tent zimetumika Nairobi wakati wa adha, mtu anapita pale tu kwanza zitakuwa zinatumika asubuhi. Hatuna haja ya kukamilisha Jengo la Abiria, ndiyo tuanze kurusha ndege kubwa.
Mheshimiwa Spika, leo ninaposimama hapa, simu yangu hii hapa Wabunge wanaweza wakaangalia, huwezi kupata booking ya kwenda Bukoba leo. Asubuhi nilikuwa naangalia booking iliyokuwepo ni ya tarehe 12. Ndege za kwenda Kagera zimekuwa kama anasa kwa maana ndege ni moja inajaa haraka. Tunapoomba tujengewe Uwanja wa Kajunguti tuna maana. Sasa haiwezekani leo mtu anayetaka kwenda Bukoba kwa dharura inabidi utafute safari ya kwenda Mwanza, ukifika Mwanza ndiyo uanze kusafiri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, huwezi tena kwenda na ndege maana ndege two weeks, one week ndege inakuwa imeshajaa, ndege ni moja, lakini watu wa Kagera tunasafiri na ndege mara nyingi, kwa hiyo inatusababishia adha. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaomba watusaidie, watujengee Uwanja wa Kajunguti maana Mheshimiwa Waziri, amesema wameona ni vyema uwanja ule uendelee kutumika. Nikwambie hata ukiweka ile rada, mvua Kagera zinavyoanza kunyesha hususan Bukoba hakuna rubani wa kutua na ile ndege pale. Tunajua sisi the way ambavyo tunakuja na ndege halafu tunakatishia safari Mwanza mpaka mvua iishe ndiyo tunaanza kwenda safari ya Bukoba. Tunaomba, tumeshapatwa na majanga mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ajali ya meli imetukumba wakati wa MV Bukoba, tumepata shida ya ndege na tumepata shida ya matetemeko. Kwa hiyo, hata sisi tunaposema tujengewe uwanja tuna maana abiria wapo Mkoa wa Kagera. Wakitujengea uwanja ile ndege haitarudi tupu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, yangu ndiyo hayo niliyotaka kuwasilisha, zaidi ya yote, naunga mkono hoja...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, bajeti ipite, Uwanja wa Kajunguti ujengwe, hatimaye waone flow ya biashara kutoka Kagera. Ahsante sana. (Makofi)