Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na kuwapongeza Waziri, Mheshimiwa Masauni, na Naibu Waziri Naibu Waziri, Mheshimiwa Sillo kwa kuteuliwa, tuna imani naye.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natoa pongezi nyingi kwa makamanda wote na watendaji wa Wizara hii kwa kazi nzuri ya kulinda amani nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi katika Mkoa wetu wa Iringa zipo changamoto nyingi, tunaomba kupatiwa pesa ya kutosha. Moja, uhaba mkubwa wa askari katika vituo vyetu vya polisi; pili, uhaba mkubwa wa magari na fedha za mafuta na matengenezo ya magari; na uhaba wa vitendea kazi kama computer kwa ajili ya matumizi katika mifumo ya ofisi; na kuhusu makazi ya askari, nyumba ni chakavu sana na pia askari wengi wanaishi uraiani kwa kukosa nyumba katika makambi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Jeshi la Magereza; changamoto kubwa tunaomba Serikali ihamishe Gereza lililopo Kihesa Mgagao katika Wilaya ya Kilolo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tuna dhana ya kulinda historia za wenzetu, hili eneo lilikuwa ni Kambi ya Wakimbizi wa Kusini mwa Afrika, kuna viongozi wa nchi waliishi pale kama Nelson Mandela, Thabo Mbeki, Walter Sisulu na kadhalika. Siyo haki eneo hilo Serikali iondoe hilo gereza kwa sababu yapo maeneo mengi katika Wilaya ya Kilolo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Jeshi la Zimamoto, kwana hawana makazi ya askari na hawana ofisi za wilaya, magari ya zimamoto kwa sababu tunayo misitu katika Wilaya ya Kilolo na Mufindi ajali za moto kila wakati na tuna Mlima Kitonga tunahitaji crane, ajali ni nyingi mlimani na vifaa vya uokozi vya majini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.