Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi na ninampongeza Mheshimiwa Rais kwa Royal Tour, nadhani itafanya nchi yetu ijulikane zaidi na tupate watalii, ili maeneo haya tunayojaribu kuyahifdhi yawe na manufaa na tija kwa nchi yetu. Ninampongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri na kwa kweli, leo nitachangia hii bajeti nikiwa na furaha kidogo kwa sababu moja; kwanza Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Maliasili na Mazingira mmenifurahisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kweli, Mheshimiwa Mwenyekiti shikamoo na Wajumbe wako wote. Hii inaweza ikawa ndiyo ripoti ya kwanza ya Bunge hili, nzuri sana, ya Kibunge, hongereni sana. Mmezungumza yale yanayowasibu Watanzania, hongereni sana, lakini vile vile nitachangia kwa upole kwa sababu, Mheshimiwa Waziri Angellah Kairuki wakati anaanza hapa amesema hii ndiyo hotuba yake ya kwanza akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli, nikianza kutwanga hapa wakati ndiyo hii ya kwanza, itakuwa siyo uungwana. Kwa hiyo, leo nashauri sana tu na kwanza nakupongeza kwa kuanzisha ile mijadala ya kuwaita Wabunge wa Mikoa yote na kuzungumza nao, ili upate wanachotaka Watanzania kupitia Wabunge wao, ukiendelea hivyo, utajifunza mambo mengi sana. Kwa hiyo, kwa kweli, nakupa big up sana, hii itakuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ya kwanza ambayo nachangia nikiwa a bit calm. Vile vile Naibu Waziri wako ni mtu mwema na atakusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu, kamati imepunguza kazi yangu kubwa sana, leo niseme Mheshimiwa Waziri, kitu ambacho hatutaki ku-negotiate ni mahusiano ya wananchi na watu wa hifadhi na ni kwa kuwa, kwenye hotuba yako umezungumza habari ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ukurasa wa 113, inasema hivi, “kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi” kwa hiyo, siyo takwa tu, is not just a speech ni commitment ya Chama Cha Mapinduzi. Nakuomba sana uwe mkali sana linapokuja jambo la mahusiano kati ya wananchi na watu wako wa hifadhi, uwe mkali sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ilikuwa inasema hivi; “Ili kuwa na uhifadhi endelevu ni lazima mjali haki na maslahi ya wananchi.” Ilani imezungumza vizuri sana. Mali zao zilindwe, mashamba yao yalindwe, mifugo yao ilindwe na more importantly, maisha yao kila wakati, ukifanya hili utakuwa Waziri mzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, ushauri wangu mwingine Mheshimiwa Mchengerwa alipokuwa Waziri hapa alikuwa na kauli zake mbili nzuri sana, ambazo ningekuomba uazime. Wananchi wa Tanzania ni wahifadhi namba moja na kwamba kazi za nyinyi mnaohifadhi kazi zenu zitapimwa kwa kusikiliza Wananchi wa Tanzania wanataka nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, amezungumza Mheshimiwa Profesa Kabudi hapa kwenye utalii na uhifadhi; sisi tunafikiri utalii ni kuwa na mbuga za wanyama nyingi tu na mapori tengefu, hapana siyo kweli. Ukiangalia nchi 10 Barani Afrika ambazo zina maeneo ya hifadhi na hiyo mka-update na nyinyi list yenu Wild Atlas bado inasema Tanzania ina mbuga 16 wakati tunajua zipo 21 ambayo inafanya Tanzania ya tano, sita huko wakati ilitakiwa actually iwe ya pili, ya kwanza ni Kenya, halafu Tanzania, halafu Zambia, lakini bado hawaja-update. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukiangalia nchi ambazo zinafanya vizuri ni Egypt ina watalii karibu 11,000,000 unajua wana mbuga ambazo hazizidi hata tano. Maana yake utalii lazima tufikiri more broadly kuliko tunavyofikiri. Ukitembelea Washington DC utalii watu wanakwenda African American Museum, John Kennedy Memorial Centre na Luther King Junior. Ukienda Italy wanakwenda kwenye St. Peters Basilica Church yaani ni vitu vingi sana kuliko sisi tunavyofikiri ni kwenda tu kuangalia Wanyama pori na maeneo mengi. Kwa hiyo, lazima tufikiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ukiangalia nchi kama Morocco haina mbuga nyingi sana, lakini watalii ni wengi, kwa sababu factors nyingi zinazoleta watalii. Vilevile ukiangalia Tunisia hawana mbuga nyinyi, lakini watalii ni wengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tunazungumza habari ya 33% ya nchi hii ipo kwenye hifadhi; ushauri wangu mwingine usikubali proposal nyingine ya aina yoyote ya namna ya kuongeza maeneo ya hifadhi, kwa sababu is not sustainable, population yetu inaongezeka sana. Ni afadhali tuweke nguvu kwenye haya tuliyonayo yawe well managed na ilete return kwa nchi yetu. Siyo namba tu ya mbuga za wanyama na mapori yanaongezeka, lakini uhalisia ukiangalia hatuoni benefit. Halafu mnaongeza kwa kuwatoa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimshauri Mheshimiwa Waziri kuhusu WMAs na mimi ninazungumza hapa kama Mwenyekiti wa Wabunge wenye WMA. Nikushukuru umewaalika watu wa WMA hapa. Mahusiano tunataka kuona hapa hawa ni wahifadhi na nyinyi ni wahifadhi mnauza nchi yetu na mnafanya kazi mmoja mdumishe mahusiano. Tunataka mtu wa TANAPA apande ndege aende akauze mbuga zake na mtu wa WMA aende akauze mbuga zake wote mpo kwenye ndege moja. Mmoja ana banda pale, mwingine banda pale, mwekezaji aliyepo WMA ni kama aliyepo Serengeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, kama walivyosema Kamati ya Bunge, mwaka jana na leo wamerudi, tunakuomba Maazimio ya Bunge, yalishapitishwa hapa kwamba pesa za WMAs zinazodaiwa na WMAs zirudi, lakini Bunge lilisema hivi tengenezeni mfumo ambao utawezesha kila mdau na kwa sababu tumeshaweka mpango huu kwa mujibu wa Sheria kila mtu anapata pesa zake kwa wakati. Kila mtu akipata pesa zake kwa wakati uhifadhi utaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni migogoro; Mheshimiwa Waziri WMAs zinafanya kazi za uhifadhi kama unavyofanya wewe. Mimi sioni logic ya kugombana kuhusu mipaka kwa sababu wote tunafanya kazi hiyo hiyo moja. It illogical kufikiri eti pori linaweza chukua sehemu ya WMA for conservation wakati hata wao wanafanya shughuli hiyo hiyo ya conservation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea ku-promote WMAs na kuna Wabunge wengi wanataka kuanzisha WMA. WMA ni nzuri, kwa sababu ni modal ambayo inafanya wananchi washiriki moja kwa moja kwenye uhifadhi. Nchi kama Namibia, Kenya, Botswana, Zimbabwe na South Africa wote wanafanya hivyo. Ni modal nzuri sana, zitauza Wizara yako vizuri sana, kwa sababu ni modal ambayo ina-empower wananchi wenyewe washiriki kwenye conservation. Kwa hivyo, tutafika mahali wewe utakuwa uhangaiki, kwa sababu wanyama pori wanalindwa sawa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, …

(Hapa kengele ililia kuashira kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. Muda wako umeisha.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ala muda umekwisha kumbe? Haya. Basi nashukuru kwa kuwa, leo nina furaha basi nitaishia hapa. Ahsante sana. Ninaunga mkono hoja. (Makofi)