Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Maji.
Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema maneno haya yafuatayo; Mheshimiwa Awezo Waziri wetu, mtu makini, Waziri wa viwango Mwenyezi Mungu amjalie kwa ibada hii kubwa ambayo unaifanya ya kugawa maji kwa kila mwananchi wa hapa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sifa nyingi na kubwa zaidi zimwendee kipenzi chetu Mama, yetu Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye alitanabaisha kwamba, moja kati ya jambo kubwa ambalo yeye atalifanya ni kuhakikisha kwamba anamtua mama ndoo kichwani. Tunaona na tunathibitisha (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na nikupongeze kwa maneno ambayo uliongea jana mbele ya Mheshimiwa Rais, kwamba wanaomuelewa ni wengi zaidi kuliko wale ambao hawamuelewi. Kwa hiyo tupo naye, mafanikio tunayaona, kazi kubwa ambayo anaifanya tumeiona. Tumeona fedha za UVIKO zilivyokwenda kwenye sekta hii ya maji, tumeona jinsi ambavyo wananchi wengi wamepata maji kuliko miaka ile ya nyuma ilivyokuwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hatuna budi kumuombea Mheshimiwwa Rais wetu, kumuombea Mheshimiwa Waziri wetu, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote wa wizara kwa kazi hii kubwa ya ibada wanayoifanya. Juhudi hizi siyo sisi tu ambao tumeziona kama Watanzania au kama wananchi wa hapa Tanzania; Benki ya Dunia imethibitisha mwaka jana mwaka 2023 kwa kuona utendaji bora ambao umefanywa kwa mradi wa P4R, malipo kwa matokeo. Kutokana na faida hiyo na kazi kubwa ambayo Serikali yetu imeifanya hasa Wizara ya Maji, tunapata fedha kutoka bilioni 350 kwenda bilioni 654, na kwamba sasa mikoa itaongezeka kutoka mikoa 17 – 25; halmashauri kutoka mia moja themanini na sita, ukitoka themanini na sita hadi mia moja tfedhathini na saba.
Mheshimiwa Spika, hii ni kazi kubwa na mafanikio haya kwa kweli hatutaweza kupna kwa kipindi kifupi lakini huko mbele kunatia matumaini makubwa. Hongereni sana sana Wizara hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi ninaona kabisa kwamba kwa mafanikio haya fedha hizi zikija tukichanganya na fedha ambazo zitakuwa zimetoka kwenye mfuko wa maji nina uhakika acha zile changamoto ambazo zipo kwangu kule Kishapu zitashughulikiwa. Ninasema hivyo kwa sababu kwangu kule Kishapu kuna miradi ambayo kidogo imekwamakwama, na changamoto kubwa imekuwa ni fedha; lakini sasa hivi kwa uwepo wa fedha hizi Mheshimiwa Waziri sitamwelewa kama kwenye miradi ile ambayo imekwama ya Igaga, Mwamashele, Lagana, Mwamandota kule Ngofira, Nwang’olo, Ngenze pale Mwadui, Masanga kwenda Ndoleleji, miradi ya visima virefu ya Idukilo hadi Kabila; kama ikikwama sitaelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sitaelewa miradi hii ikiendelea kukwama baada ya kipindi cha mwaka mmoja kama mambo yakiwa yamekaa sawa sawa, maana fedha watakuwa tayari wanazo.
Mheshimiwa Spika, nitoe angalizo moja, tunachangia hapa tunasema kwamba mfuko wa maji uongezewe fedha kutoka shilingi 50 mpaka shilingi 100, lakini mimi angalizo langu ninapenda kulitoa kwenye kanuni ya ugawaji wa fedha kwenye mfuko wa maji.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa ninaomba kanuni ya ugawaji wa fedha kwenye mfuko wa maji iwe sawa sawa na kanuni ya ugawaji wa maji kwenye mfuko wa barabara. Leo hii tuna Waziri ambaye ni mwelewa, ambaye ni mwema na mcha Mungu. Siku ikijakutokea Waziri ambaye anajijua mwenyewe akaja akawepo Wizara hii ya Maji, mgao ule anaweza mtu akaja akaamua akapeleka fedha nyingi zaidi huku na huku kwingine akaacha. Kitu ambacho kinaweza kikatuletea shida. Kwa hiyo walao tukijaribu kuangalia mfuko wa maji, kanuni zikaendana na mfuko wa barabara ambao wenyewe unasema kwamba asilimia kadhaa itakwenda huku, fulani atapata hiki na fulani atapata hiki lakini sasa hivi haifafanui. Haifafanui nani anapata nini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo ningependa kulionge kwa msisitizo mkubwa sana, ninaomba sana Mheshimiwa Waziri; mafanikio mengi ambayo tunayasema kwenye Wizara hii, na mafanikio mengi ambayo tunawasifu watendaji; nimpongeze sana mimi kwa kweli kwenye watendaji napenda sana kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Eng. Clement Kifegalo. Mwenyezi Mungu amjalie mema sana na aendelee kumuweka Mkurugenzi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ambacho mimi napenda kukisema ni kuhusu malipo ya wakandarasi, benki sasa hivi wamekaa wathamini kule juu ukikopa bilioni tatu sasa hivi unalipa milioni 500 kwa mwaka, that is a lot of money. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, miradi hii mikubwa ambayo tunaifanya na inafanywa, mimi ninaomba Serikali ijaribu kuwa makini sana. Tusiache mpaka watu... Watu sasa hivi wameanza kuuziwa nyumba na wameanza kupata stress. Hili jambo mafanikio haya yaende sambamba na mafanikio ya wale ambao wanafanya hizi sifa zipatikane. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, miradi hii bila kufanywa na hao watu wakandarasi ambao wamekuwa wakiifanya kwa roho moja, kazi ingekuwa ni ngumu sana na pengine leo lugha hii ambayo tunaizungumza isingekuwa namna hii. Ninaomba sana Wizara ijaribu kukaa na Wizara ya Fedha. Wizara ya Fedha huko hebu wa-boost kidogo maana na wenyewe kule wana mambo yao. (Makofi)
SPIKA: Haya, ahsante sana. (Makofi)
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)