Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na mimi nianze moja kwa moja kwa kuunga mkono hoja. Vilevile, mimi naunga pale pale kwa Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla kwamba, niwaombe sana wapigakura au wajumbe wa Mheshimiwa Waziri Aweso basi muangalieni kwa huruma na kwake ninyi muwe watu wazuri ili tusiseme wajumbe noma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu, niseme tu nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Aweso kwa sababu ni kijana mdogo sana lakini mchapakazi sana. Kule kwetu Mkoa wa Mara tunamwita Chacha. Ukija kule Mkoa wa Mara ukisikia Waziri Chacha ujue ni Mheshimiwa Waziri Aweso kwa sababu wanaume wa Mkoa wa Mara ni wachapakazi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema hivi kwa sababu, mpe mtu maua yake akiwa bado yuko hai. Mheshimiwa Aweso ametuheshimisha sana vijana wa Kitanzania na anafanya kazi zinazozidi umri wake. Hii ni jinsi gani inaonesha kwamba Mheshimiwa Rais aliona vema na ataendelea kutuangalia vijana kutokana na vijana wenzetu ambao mmetuheshimisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze sana Engineer Mwakalukwa Meneja wa Mkoa wa Mara kwa kazi nzuri anazozifanya. Ni meneja ambaye ka kweli ni mchapakazi, halali, hatulii na haki ofisini; yeye anafanyia kazi site. Ombi langu kwa Serikali ni vizuri sasa miradi hii mnayowapatia hawa mameneja wetu, nikimuangalia Mwakalukwa alikuja akiwa handsome lakini sasa hivi amezeeka zeeka hivi. Anafanya kazi sana lakini pesa kidogo ndiyo inakuwa shida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi niiombe sana Serikali basi muwe mnawapa pesa kwa haraka mameneja hawa ili waweze kufanya kazi zao kwa urahisi. Vilevile, nimpongeze sana mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya. Hili jambo alilolianzisha la kumtua mwanamke ndoo kichwani, kwetu sisi Mkoa wa Mara tunasema Mama Samia anastahili mitano tena kwa sababu ametuepusha na hatari nyingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndoa nyingi za wakina mama wa Mkoa wa Mara zilikuwa zinavunjika kwa sababu ya kufuata maji mbali lakini sasa tuna maji ya kutosha. Ukija pale kwetu Msoma Mjini, ukifika mpaka mabomba yanapasuka kwa kuwa tu na maji mengi sana ya kupitiliza. Vilevile, Mama Samia amefanya miradi isiyowezekana na sasa imewezekana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kuna Mradi wa Mugumu – Serengeti. Mradi huu ulikuwa ni Mradi chechefu na sugu lakini sasa umewezekana. Hata hivyo, hii yote ilikuwa ni kutokana na kwamba hata wawakilishi wake ambao ni wachapakazi majembe kama alivyo Waziri wetu Mheshimiwa Aweso anavyofanya kazi usiku na mchana, anapomtuma anatumika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana sisi kwetu Mkoa wa Mara wanawake wote tunasema hatuna Rais mwingine, hatumfikirii mtu mwingine na anayewaza kuja kugombea na Mama Samia ajue amechelewa. Yeye asubiri bado sana. Sisi tuna Mama Samia mpaka kieleweke. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe sana Wizara ya Maji. Ombi langu kwenu, visima vilivyotolewa na Mama Samia iwe baraka kwa Watanzania. Hata hivyo, ni vema mkavipeleka katika taasisi muhimu kama vile hospitali pamoja na shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kuna shule ambazo mimi niliwahi kutembelea kama vile Shule ya Tagota Tarime lakini pia Shule ya Nyandoto na Nkongore ni shule ambazo wana shida sana. Kwa hiyo, watakapopelekewa visima wakati tunasubiria yale maji mengine ambayo yanaendelea kuunganishwa basi itakuwa ni vizuri. Kwa hiyo, mimi niseme kwamba tuangalie sana kwenye taasisi hizi muhimu ili kusudi kuwakwamua watoto hawa na madhila ya maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze sana Waziri wangu Mheshimiwa Aweso kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya ya kusimamia kazi anazopewa na Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa mfano, kuna huu Mradi ambao umefanyika wa Mugango – Butiama. Mradi huu kwetu sisi umekwisha na sasa wana-test mitambo. Muda si mrefu watu watapata faida ya maji yanayoitwa Maji ya Mama Samia. Kwa hiyo, mimi niseme naishukuru sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe wanawake wote wa Kitanzania. Ninyi ni mashahidi, tulikuwa tunafuata maji kwa shida sana lakini Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuja kututua ndoo kichwani na ndiyo maana tunasema Mama Samia mitano tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)