Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Emmanuel Lekishon Shangai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Bajeti ya Wizara ya Maji. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na timu nzima ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi nipende sana kumshukuru Mheshimiwa Waziri. Kwenye Bajeti ya mwaka jana nilimwomba atupatie gari kwa ajili ya watumishi wa RUWASA Wilaya ya Ngorongoro. Nimshukuru kwamba tumepata gari kwa jili ya watumishi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ngorongoro, wanafanya kazi kubwa sana. Pamoja na wilaya yetu kuwa kubwa lakini wanafanya kazi kubwa usiku na mchana kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi yangu leo ni shukurani lakini pia nina maombi. Tunashukuru kwa sababu mradi wa Oldonyosambu - Masusu wananchi wa Oldonyosambu pamoja na Masusu hawakuwahi kupata maji lakini sasa hivi wanatumia maji, akina mama wanatembea mita 500 wanapata maji ilhali walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 10 kufuata maji mtoni. Kwa hiyo nashukuru sana. Tunashukuru pia kwa mradi wa quick win wa Wasso. Awali wananchi walikuwa hawapati maji ya kutosha lakini kwa sasa hivi wanapata maji ya kutosha; pamoja na maeneo mengine ya Oloirien na Lopoluni kwenye mradi ule wa Covid, maeneo yale pia wamepata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wilaya zetu za wafugaji sisi tunahitaji maji kwa ajili ya binadamu pamoja na mifugo. Leo ukienda Wilaya ya Longido ukiwawekea wananchi maji bila mifugo ule mradi hautakuwa na maana kwao. Kwa hiyo nikuombe sana ninyi pamoja na Waziri wa Mifugo muweze kufanya coordination, ikiwezekana kama wewe una milioni 500 na yeye aongeze milioni 500 angalau tuwe na miradi ambayo ina impact kubwa kwa wananchi wale. Kwa sababu unaweza ukawapa wananchi lakini baadae watalazimisha mifugo yao kunywa. Kwa hiyo ni vizuri sana mkiweza kufanya coordination.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda Simanjiro, ukienda Kiteto, Longido na maeneo mengine kama Shinyanga na Mwanza mfanyae coordination; mifugo ikipata maji na binadamu wao ndio wanajisikia vizuri, lakini ukiwawekea wao koki na mifugo yao hawajapata maji kidogo ni tatizo kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimwombe Mheshimiwa Waziri kuna mradi wake wa Mageli Vijiji Nane. Tunashukuru kwa sababu ule mradi kwa sasa umekwishafika asilimia 54. Tulikuwa tunahitaji zaidi ya bilioni sita kwa sasa hivi mmetupa bilioni tatu. Hatua ambayo mradi umefika sasa hivi ni kwenye ujenzi wa tenki la lita 1,000,000, lakini bado kuna matenki mengine nane ambayo bado hayajajengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Waziri hizi bilioni tatu zilizobaki. Mradi huo umeanza mwaka 2017, mpaka sasa hivi ni miaka saba. Wananchi zaidi ya 54,000 ambao wanategemea mradi huo wanahitaji kupata maji, kwa sababu wananchi wa kata zaidi ya nne na vijije nane wanategemea mradi ule. Kwa hiyo nikuombe sana Mheshimiwa Waziri utuangalie katika suala hili na na angalau kuongea na wataalam wangu wa wilaya tuone namna ya kupanua yale maeneo kwa sababu kuna vichotea maji zaidi ya 60. Na vichotea ma 11 vimetengwa kwa ajili ya mifugo kupata maji huko Mbautu. Ni muhimu sana sasa tukaongeza kwa ajili ya kufanya mifugo kutorundikana katika eneo moja. Kwa hiyo nikoumbe sana Mheshimiwa Waziri atuangalie katika hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, kuna mradi wa visima 14 kwenye Pori Tengefu la Loliondo. Unajua alienda na akawaahidi wananchi kwamba watakwenda kuchimba visima. Ni kweli kwamba visima vimechimbwa, lakini mpaka sasa hivi ni visima viwili ndivyo vinavyotoa maji, visima vingine vyote 12 hakuna. Visima hivyo ni kwa ajili ya Ngobereti, Arash, Losoito, Soitsambu, Loswashi, Orkuyane, Oloipiri, Ormanie kwa maana ya Oldovanioiti, Orkanda, Sukenya na Mondorosi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi hawa walikuwa wanategemea maji kutoka kwenye eneo la Pori Tengefu, sasa hivi hawapati maji. Sasa ni vizuri sana wizara waangalie namna hawa wananchi sasa vile visima vichimbwe pamoja na kuweka miundombinu ya wananchi kupata maji ya mifugo pamoja na binadamu. Ni muhimu sana wakatekeleza hilo lakini kwenye visima hivi, na mkandarasi aliyechimba baadhi ya visima mpaka sasa bado anadai shilingi milioni 342 ya awamu ya kwanza lakini bado anadai awamu ya pili advance payment ya shilingi milioni 710 ni vizuri mkawalipa angalau kazi ifanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine wakati huo pia waliahidi kwamba wizara watachimba mabwawa kwenye eneo la Pori Tengefu la Loliondo. Kulikuwa kuna mabwawa ya awali walisema 35, lakini baadaye Wizara ilipata fedha ya kufanya usanifu kwa mabwawa 18. Mpaka sasa hivi wameshafanya usanifu lakini mabwawa mengine 17 hayajafanyiwa usanifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wangu wameomba shilingi bilioni nne kwa ajili ya mabwawa sita ya awali. sasa mimi nimuombe Mheshimiwa Waziri, hawa wananchi walikuwa wanategemea kwamba kwenye mvua za mwaka huu tungeweza kupata maji mengi, na huu ndio ulikuwa mwaka wa fursa na kwamba wananchi wangepata maji mengi kulingana na mvua zilizonyesha, hatuwezi kujua mwakani. Mimi niombe, haya mabwawa yalikuwa kwenye kata zetu zaidi ya 17, kata ya Oldonyosambu ilikuwa ni bwawa moja, Engaresero moja, Malambo mabwa mawili Enguserosambu moja, Nam moja, Soitisambu moja, Ololosokwani moja, Samunge moja, Digodigo moja, Pinyinyi moja, Piaya, Arash, Ormanie, Losoito, Kirtalo Oloipiri na Loswash. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ni muhimu sana Mheshimiwa Waziri waangalie namna ya wananchi hawa. Wilaya yangu hadi sasa hivi upatikanaji wa maji ni 74%. Tukiweza kuchimba mabwawa haya pamoja na kutengeneza visima hivi wananchi watapata maji ya kutosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baada ya kusema hayanaimba kuunga mkono hoja. (Makofi)