Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani mashine zilikuwa zimekataa. Nashukuru sana kwa kupata fursa ya kuchangia Wizara ya Maji jioni hii, waswahili wanasema, “Kushukuru ni bkuomba tena.” Nitajitahidi kutumia muda kushukuru na kueleza miradi yangu ambayo Serikali yetu imetufanyia kwa muda mfupi lakini ndiyo nitakuwa natumia gia hiyo pia kuomba katika kuhakikisha tunakamilisha miradi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa commitment kubwa aliyoifanya katika uwekezaji wa miradi ya maji mpaka Taifa letu limefikia kuwa kinara katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara, hii ni commitment kubwa sana katika rank za World Bank, tunampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu; kwa lugha nyepesi Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri wake wanaingia kwenye rekodi nyingine mpya ya kutekeleza miradi ya maji mingi sana nchini; tunawapongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nakupongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yako na Naibu Waziri kaka yangu Nsumba Ntale Mheshimiwa Kundo ambaye amehamishiwa Wizara hii na Mheshimiwa Rais. Nimpongeze Katibu Mkuu wenu na wasaidizi wake wote pale Wizarani pamoja na Katibu wako Gibson ambaye amekuwa akitupa ushirikiano mkubwa sana; tunawashukuru PR yenu ni nzuri katika kuhakikisha mnatusikiliza na kupeleka miradi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nampongeza Meneja wa RUWASA wa Mkoa wa Tabora, Engineer Kapufi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya igunga na Engineer Humphrey Mkurugenzi wa Maji Igunga - IGUWASA pamoja na Bodi yake na watumishi wote; kiukweli wanatutekelezea kwa hatua kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Igunga na specific Jimbo la Igunga ilikuwa ni miongozni mwa Majimbo kame sana lakini sisi Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi imetupatia mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 600 kutoka maji ya Ziwa Victoria. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais pamoja na chama chetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni takribani kilomita 400 kutoka Mwanza mpaka Igunga na sasa hivi sisi tunatumia maji ya Ziwa Victoria na ndiyo maana unaona hata mimi Mbunge wao ukiniangalia kipara kinawaka kwa sababu ya maji ya Ziwa Victoria, nashukuru sana chama chetu. Sasa tumeendelea kupewa fedha kwa ajili ya upanuzi wa miradi na changamoto kubwa kama ambavyo wamesema Wabunge wengi cashflow imekuwa siyo nzuri sana. Pamoja na hayo tunaendelea kushukuru; kiukweli mmetufanyia mambo mengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kusema mambo mawili matatu; jambo la kwanza, pale kwetu Mheshimiwa Waziri sisi tuna mradi mkubwa wa kupeleka maji katika kata saba vijiji 16 imefikia 60%. Unatoka sehemu inaitwa Bulenya ambapo limejengwa tenki kubwa lenye uwezo wa kubeba maji lita milioni 1, unakwenda Kata ya Mwamashiga, Kata ya Mbutu, Isakamaliwa, Kining’la, Mwamashimba, Mwamakona, Igurubi na Kinungu, tunaomba sana mumsimamie makandarasi ama mumfanyie extension ya muda. Tunaamini mpaka kufika mwezi wa 12 mwaka huu atakuwa amemaliza; kwa ufanisi na uwezo wenu wa kazi naamini mtalikamilisha linakwenda kwenye maeneo mengi ya wapiga kura wengi wa Chama cha Mapinduzi ambao ni wapiga kura wangu, Mheshimiwa Rais pamoja na Waheshimiwa Madiwani wetu wa Chama cha Mapinduzi, lakini pia ni moja ya miradi ambayo itatusaidia kwenye kampeni zetu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa tunamtua mama ndoo kichwani kwa vitengo nashukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa mradi huu ambao mlitupatia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, pale Igunga tuna mradi tunahudumiwa na mamlaka mbili, Mamlka ya vijijini (RUWASA) na mamlaka ya Mji (IGUWASA). Nishukuru sana IGUWASA kwa kweli kwa mamlaka ya mji, mimi ni mmoja ya mamlaka za mji ambazo kiukweli tunasema tumefikiwa na maji kwa 100% pale mjini. Tunakushukuru sana kwa jitihada ambazo umetusaidia na sasa umetupatia fedha kwa ajili ya mradi wa maji taka. Mkandarasi bado yuko site anajenga yale mabwawa, cashflow imekuwa siyo nzuri tunaomba utusaidie ili yale mabwawa yaweze kukamilika katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kuweza kuhudumia wakazi wa Igunga mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tuna maji kutoka Igunga Mjini, Makomelo kwenda Mgongolo ambao ni wa shilingi milioni 800 pia tunawashukuru Mheshimiwa Waziri ulitupatia huu mradi kwa ajili ya kufanya maboresho kutoa laini ya zamani kuweka laini mpya, tunaomba pia utusaidie huu mradi uweze kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, niipongeze bodi yangu ya Mamlaka ya Maji Mjini IGUWASA walibuni chanzo kipya cha maji. Wakatengeneza laini ya pili ambayo inaenda kuisaidia laini ya Ziwa Victoria, kutoka Igogo kwenda tenki kubwa pale la Mwamaganga ambalo linabeba maji lita 1,500,000. Sasa kuna fedha ambazo walikuwa wameomba Wizarani na tunashukuru Wizara yako mmetupitishia, basi tunaomba Serikali itupatie fedha na sisi utukumbuke katika kutengeneza hii laini. Lakini pia ndiyo mwenendo wa kuhakikisha kwamba tunaipunguzia presha KASHWASA. Tutakapokuwa na laini ya pili itakuwa inapa back up, hata inapotokea changamoto maji yanakosekana KASHWASA wananchi wa Igunga wanaendelea kupata maji kutoka kwenye hii laini yetu ya Igogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, point nyingine ambayo ningependa kuchangia kwa jioni hii, kuna suala la uchimbaji wa visima 900, mradi wa Mheshimiwa Rais; tunamshukuru sana kwa kuliona hili na mimi nimepata visima vitano, Ibole, Igurubi, Nguvumoja, Kityelo, Imenya, Lugubu na Mgazi – Lugubu. Lakini kabla ya hapo pia Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) walikuwa wameanza programme ya visima vingine vitano ambavyo vipo Mwajinjama Mtunguru, Mwajilunga Kinungu, Kining’inila, Isakamaliwa na Chagana, naishukuru sana Wizara, kwa hiyo, kwa ujumla nina visima 10 ambavyo viumeshaanza na kwa kuwa ile mitambo ilikuwa imeshafika kwenye jimbo langu, sasa wataunganisha na hivi visima vitano vya Mheshimiwa Rais. Naamini kufika mwezi wa 12 kama mlivyotuahidi kwamba mtatukabidhi visima basi tunawatakia kila la heri mkamilishe visima hivi ili tuendelee kumtua mama ndoo kichwani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ningependa kulichangia jioni hii kama ambavyo wamechangia Wabunge wengine ni vyanzo vya mapato ambavyo mnatumia kupata fedha kwa ajili ya kwenda ku-finance miradi hii. Ukifuatilia kwa haraka nchi nyingi za wahisani haziwekezi fedha nyingi sana kwenye maji maeneo ya vijijini wanakwenda sana mijini. Sasa kama Taifa inabidi tuamue ili angalau tuangalie namna ya ku-finance miradi ya maji ambayo inakwenda vijijini, na Wabunge wengi wametoa mawazo na mimi ningependa kuungana nao tuangalie structure mpya ya tozo za kwenye mafuta ambapo baadhi ya maeneo tunaweza tukahamisha kwa sasa wanapata kwa kila lita shilingi 50 angalau wapate hata shilingi 100 au 150 na waunde mgawanyo watengeneze structure RUWASA ipate fedha, maji mijini wapate fedha lakini pia na rasilimali maji wapate fedha ili tuweze kutatua kwa kiwango kikubwa matatizo ya maji yaliyoko vijijini kwa kuwa utafiti unasema katika Dunia hii ukiacha hewa jambo la pili linalofuata kwa umuhimu ni maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)