Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi kuweza kuchangia mawazo yangu kwenye Wizara hii nyeti ya Maji. Kwanza kama wenzangu, nachukua fursa hii kumpongeza Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayofanya na msukumo mkubwa anaoufanya kupeleka fedha nyingi kwende miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Waziri mwenye sekta, ndugu yangu Mheshimiwa Aweso pamoja na Naibu wako ndugu yangu Mheshimiwa Kundo, mnafanya kazi nzuri, pamoja na Naibu Waziri aliyemtangulia Mheshimiwa Kundo pia alifanya kazi nzuri akihudumu kwenye Wizara hii. Menejimenti yako nayo inafanya kazi nzuri mimi nawapongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa namna ya pekee, kwa kuwa mimi mkoani, nafanya timu na RM na timu ya wilaya, nampongeza Meneja wangu Boaz, anafanya kazi vizuri na Engineer Maganga, wanatupa ushirikiano mzuri na ndiyo maana mambo yanaenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitaongelea mambo mawili, la kwanza ni la jumla. Tumekuwa tukipiga kelele ndani ya Bunge hili, miradi ya maji haiendi. Kama nchi, shida siyo vyanzo vya maji, shida ni financing kwenye miradi ili maji yaweze kuwafikia wananchi. Tuna maji ya chini na surface water lakini ni namna gani tutayatoa yawafikie wananchi, ndiyo jambo linalotuumiza vichwa kama Taifa. Leo hii umetoa hotuba yako Mheshimiwa Waziri na concentration yako ulikuwa unaongelea habari ya Green Bond ya Tanga UWASA. Umeona kwamba Tanga UWASA ilivyo-perform na ukachukulia mfano ni wazi ndiyo taasisi ya kwanza Barani Afrika kutoa Hati Fungani ya Kijani kwa maana ya Green Bond. Sasa, huo ndiyo mwelekeo wa kutafuta alternative financing kwenye miradi ya maji. Tuking’ang’ania vyanzo vya Water Funds, PforR, sijui Government Fund, tutapiga mark time hapa, hatutaenda mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mchakato ulikuwa ni mrefu sana, haujaanza leo, umechukua muda mrefu. Kwa Bunge hili, nachukua nafasi hii, pamoja na kukupongeza wewe Mheshimiwa Waziri, nazipongeza taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye mchakato huu. Kwa kuwa ndiyo uelekeo tunaoenda nao, lazima tuwape moyo ili tutakapokuja na jambo hili kwa taasisi nyingine, watuunge mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana UNCDF (United Nations Capital Development Fund), wao ndiyo waliotusaidia katika michakato ya ku-fund process zote mpaka hii Green Bond ikaingia kwenye soko na sasa hadi tulipofikia ni hatua nzuri. Pia, tunawapongeza pia Tanzania Capital Market and Security Authority (CMSA) kwa ku-support mchakato huu na kutoa approval yote mpaka tumefikia hapo tulipo na ni Green Bond ambayo inatupa heshima katika Bara hili la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawapongeza Dar es Salaam Stock Exchange (Soko la Hisa la Dar es Salaam), wamekuwa wakitoa ushauri mzuri sana pamoja na Benki ya NBC ambao ndiyo financer wanaosimamia hii Green Bond ya Tanga UWASA. Vilevile, kwa namna ya pekee Wizara ya Fedha, haikuwa rahisi kwa sababu hii Green Bond pia inahusika na approval kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Msajili Wa Hazina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitaongelea katika aspect ya uwekezaji. Tumeenda, tume-subscribe, tulikuwa tuna malengo ya kupata shilingi 53,120,000,000 lakini within the time tulivyoweka hii bond tumepata shilingi 54,722,600,000 yaani tume-oversubscribe sawa na 103% ambayo it’s over and above. Kwa hiyo hili ni jambo kubwa na ndiyo starting ya game changer kwenye uwekezaji kwenye sekta ya maji. Green bond maana yake ni bond inayotolewa kwa ajili ya mazingira na dunia uelekeo wake ni kwenye utunzaji wa mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, leo hii una mamlaka sita zenye Category Class A. Tuna hiyo Tanga imeshaodoka, Tanga UWASA imekuja na Green Bond ambayo inaenda ku-finance Mradi Mkubwa wa Maji Mkoa wa Tanga na ita-extend mikoa ya Jirani. Vilevile, kuna Mamlaka ya Maji Moshi, nayo iende kwenye uelekeo huo tukitoka hapo Mamlaka ya Maji ya Dar es Salaam, tayari najua wako kwenye pilot study wanataka waingie na bond ya shilingi 252,000,000,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamwomba Mheshimiwa Waziri, kama tulivyofanya Tanga UWASA, nao hawa twende kwa spirit hiyo hiyo. Pia, Mamlaka ya Maji ya Kahama nao wako vizuri, nao ni Category AA wanaweza wakaingia kwenye mfumo huu. Pia, Mamlaka ya Maji ya Iringa, nao wako katika category hii, Mamlaka ya Maji ya Mwanza, zote hizi tutapunguza mzigo wa kugombaniana. Shilingi 60,000,000,000 leo zimetolewa na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kwenda kulipa madeni lakini tunagombaniana, mara Mamlaka za Maji, mara RUWASA huku, kuna vurugu mechi kila mahali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tukiwa tuna vyanzo vya financing, tutaondokana na kugombania chanzo kimoja cha fedha, tutakuwa na vyanzo vingi. Naendelea kuishukuru hii Tanga UWASA, mimi kupitia Kamati ya Uwekezaji, nimepitia tangu mwanzo bond hii inaanza, nimeifuatilia kwa sababu nilijua ndiyo itakuwa mkombozi. Kwa kweli Bodi ya Mamlaka ya Maji ya Tanga, naipongeza lakini na Engineer Godfrey Hilly ni shujaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliona hata miradi mingine, walichukua mkopo wa shilingi bilioni 7.2 ambayo umeleta maji kule Tanga, wanavuna takribani lita 15,000,000, Shilingi bilioni 7.2 waliyochukua kwenye Benki ya Maendeleo ya Taifa. Sasa, ndiyo spirit tunayotakiwa twende kwenye Mamlaka za Maji, tusitegemee fedha kutoka kwenye Mfuko mkubwa wa Hazina. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo mimi binafsi nimeona ni jema na wewe sasa unavyokuja kuliongelea, uliongelee kwa msisitizo kwa baadhi ya mamlaka kama pilot nilizokutajia hizi sita kubwa giant ili tuweze ku-move mbele kama Taifa. Kwa hiyo nilitaka kutoa hilo wazo kwenye alternative financing kwenye Miradi ya Maji, tusikariri chanzo kimoja tu ambacho tunagombaniana. (Makofi)

MMheshimiwa Mwenyekiti, la pili sasa kwa sababu ya muda, niongelee habari ya jimboni kwangu. Habari ya kwanza ni usafiri, nilikuomba mwaka jana. DMO wangu wa wilaya hana gari, gari tumeomba, wenzangu naona hapo wanakwambia tunakushukuru Mheshimiwa Waziri, mimi si kwamba sishukuru najua tu nipo kwenye waiting list. Naomba brother utuletee gari ili DMO wangu anayechapa kazi, afanye kazi kwa ustadi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna madeni ya wakandarasi, kuna lile Bwawa la Kwela, ni bwawa ambalo ni mradi wa shilingi 6,000,000,000 lakini yule anadai shilingi 2,000,000,000 mwaka mzima wame-stuck. Brother, naomba katika shilingi 60,000,000,000 ulizopewa shilingi 2,000,000,000 hizi utuletee Kwela ili Mradi wa Kwela uweze ku-take-off. Pia, Mradi wa Kaoze Group, yule mtu mmempa kazi, ameenda kuchukua Advance Payment Bond benki kama security lakini hamjampa hela. Advance payment ya shilingi 300,000,000 Kaoze Group ime-stuck hamna kinachoendelea. Nakuomba brother, ukafanye haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine, Mamlaka ya Maji katika Mji Mdogo wa Laela. Mmeanza mchakato, mnataka muifanye Laela iwe na Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Laela ambayo itaweza sasa kuwa na watumishi permanent na kuendesha mambo yake binafsi kama Mamlaka ya Maji. Naomba hili jambo uli-push na ukifanya hayo kuna mambo mengi nitakuandikia kwa maandishi yanayohusu kero ya maji Jimbo la Kwela na Mkoa wa Rukwa tukiwa na ajenda ya Lake Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)