Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, nami nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Ng’wasi Damas Kamani kuhusiana na umri wa ajira zilizotangazwa na TAWA. Kimsingi hoja yake ni hoja ya msingi sana, ndiyo maana kama Wabunge ambao tunawakilisha kundi la vijana humu Bungeni lazima tuzungumze.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwenye jambo alilolisema kwamba tuongeze umri mpaka miaka 30. Nami nasema miaka 30 angalau ili sasa vigezo vile vya jumla, kwa sababu lazima wana utaratibu wao wa ku-train watu wao wanaowahitaji, basi waende wakashindwe field kama ikitokea kwamba mtu sasa ameshindikana.
Mheshimiwa Spika, kwenye hili, kwa sababu tunajua watakaoomba ni wengi, nami niseme, kwa sababu ajira za Serikali ni chache sana kutokana na jinsi ambavyo tunalifahamu soko la ajira, yaani kwamba wanaokuja mtaani ambao wanahitaji ajira ni wengi sana. Kwa maana hiyo sasa kuendelea kupunguza wigo (kupunguza goli) maana yake tunaendelea pengine kutengeneza malalamiko ambayo vijana wanaweza kulalamika kwamba tunategemea mkitangaza ajira ya Serikali, basi msitupunguzie goli ili tukapambane huko huko uwanjani ili tuone atakayefanikiwa aende.
Mheshimiwa Spika, jambo hili pia linahitaji graduates na kwamba kuna vijana wengi sana wako mtaani na utaratibu wetu wa mfumo wa elimu unatufanya wanafunzi wakae muda mwingi sana darasani kiasi kwamba anamaliza katika umri huo ambao anasema ndiyo mwisho wa wao kuomba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa nukta hiyo nami naomba kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Ng’wasi Kamani ili tubadilishe vigezo na tuongeze umri wa vijana kuomba nafasi hizi ambazo tunategemea haki itatendeka.
Mheshimiwa Spika, mwisho, tuwaombe isiwe kuna nafasi ambazo zimeandaliwa na watu fulani, wawaache vijana wakapambane kwa sababu tayari ilishaleta mkanganyiko kama hivi, ahsante.