Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

Hon. Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, nami naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kamani, kwa sababu mwisho wa siku muda wa masomo kwanza mtu mpaka asome afanye certificate, diploma na degree tayari umri unakuwa umeshasogea. Kwa hiyo, tunaposema miaka 18 mpaka 25 tutawaacha watu wengi nje.

Mheshimiwa Spika, pia tusisahau ni muda mrefu sana ajira zilikuwa hazitoki. Tunashukuru angalau kwa miaka hii mitatu au minne tumeanza kupata ajira. Sasa basi kama ni hivyo, tunaomba sana tufahamu kwamba Jeshi Usu linahitaji tu ukakamavu. Kwa hiyo, ukakamavu kwenye udereva unawezakana hata kama anakimbiza labda majangili au vitu kama hivyo, miaka 25, 26 au 30 ana uwezo huo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nakubaliana na Mheshimiwa Kamani kwamba angalau tusogeze miaka 30 na isiishie tu kwenye mambo ya TANAPA na hao wengine, tufanye na kwenye ajira nyingine. Vinginevyo watoto wengi ambao ajira zilisimama miaka sita au saba iliyopita, tutakuwa tumewaacha kwenye mfumo, wataendelea kuwa wakulima wakati wamesoma. Serikali imetumia gharama kubwa kuwasaidia na pia wanahitaji kuajiriwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naungana na hoja ya kuongeza umri kwenye ajira zote. Namuunga mkono Mheshimiwa Ng’wasi Kamani.