Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hoja ya dharura kuhusu kuongezwa kwa umri wa waombaji wa ajira za Serikali

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Tumpongeze mtoa hoja, nakubaliana tuongeze miaka iwe 30 lakini kwa sababu umetoa nafasi tuwashauri, ushauri mwingine haya matangazo yanayotolewa kwa Kiingereza tunamfaidisha nani? Kwa nini wasitoe hili tangazo kwa Kiswahili? Kwa hiyo, kama kuna eneo lingine la kurekebisha, wakarekebishe matangazo haya yawe kwa Kiswahili. Sasa unataka dereva, halafu leo unataka aongee Kiingereza, halafu ni dereva wa wanyamapori, anaenda kuzungumza hicho Kiingereza na nani? Hilo ni moja. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naangalia kitu kingine hapa. Hili tangazo la wiki mbili pekee, ni vizuri kwa sababu wamesema ni online, kwamba wana-propose online tuweke kwenye portal, lakini mara kadhaa imekuja shughuli, mitandao yetu inakuwa na shida na tume-extend matangazo mengi hapa kwa sababu ya muda mfupi unaotolewa. Kwa hiyo, ushauri mwingine waongeze iwe mwezi mzima.

Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa naangalia kwenye tangazo hapa anaambiwa, “A signed application letter should be either in Swahili or English.” Sasa kama kuna hizi option, tangazo liwe kwa Kiswahili. Kilichonishtua zaidi pale kwa dereva, sifa za dereva anaambiwa awe na one year experience without causing accident. Sasa hiyo imekaaje? Yaani kweli sisi sote ni madereva na tuko barabarani, not every accident inakuwa caused kwa sababu ya maintenance ya gari and after all utapataje hiyo data?

Mheshimiwa Spika, yaani leo dereva ni mwananchi kutoka Kiteto halafu eti unamwambia one year experience halafu without causing accident. Hii imekaaje? Ingekuwa kila mtu anaye-cause accident anakuwa nje ya barabara, matangazo kama haya ambayo ni unreasonable kati ya maeneo ambayo yanatakiwa yaondolewe, ni sehemu hiyo. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi)