Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia kwenye hoja au ajenda hii inayowahusu vijana moja kwa moja. Kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa Ng’wasi Kamani kwa kuona namna gani ajenda hii inavyotugusa tukiwa kama Wabunge wa kundi la vijana.
Mheshimiwa Spika, wenzangu waliotangulia hapa wameongelea zaidi kwenye hili Jeshi Usu. Binafsi nimeshaona matangazo mengi ambayo yanasema kigezo namba mbili au tatu cha mwombaji wa ajira ni umri. Umri wanatangaza kuanzia degree wanasema kwamba isizidi miaka 24 mpaka 25, lakini tukishuka ngazi nyingine, kuanzia diploma wanasema isizidi miaka 20 labda mpaka 23.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la ajira ni kubwa kwa nchi yetu na kwa sababu asilimia isiyozidi 60 vijana wa nchi hii wanasumbuliwa na tatizo hili la ajira. Kwa nini tusiangalie vigezo vingine ikawa hiki kigezo cha umri siyo kigezo cha msingi zaidi au ikiwezekana basi tuishauri Serikali tuongeze umri sasa kutoka miaka 25 kwenye degree tupeleke mpaka miaka 30; kwenye ngazi ya diploma tutoke hapa ambapo tuliweka miaka 20 mpaka miaka 22, iwe miaka 25; na kwenye degree tutoke kwenye miaka 25 mpaka ngazi ya miaka 30?
Mheshimiwa Spika, kwenye ngazi hii ya elimu watu wanatofautiana. Tukiangalia kuna wanafunzi ambao wanatoka moja kwa moja kuanzia darasa la kwanza mpaka kwenda kwenye ngazi ya degree, hao tunaweza tuka-assume kwamba wanaweza waka-cover katika miaka 25. Kuna wanafunzi wengine bahati mbaya sana wanafika Form Six, lakini wakifika Form Six hawafanikiwi. Je, wakiwa hawajafanikiwa, hawa wanafunzi wanakuwa wamemaliza kusoma? Hawajamaliza. Wengine wanarudi kuanza kwenye ngazi ya diploma. Kwa hiyo, wakianza kwenye ngazi ya diploma kule ikafika miaka 25 na hii miaka mitatu ya diploma je, mwanafunzi huyu tutamwona katika namna gani?
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja miaka iongezwe ifike miaka 30. (Makofi)