Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha mahitaji ya pesa shilingi 3,708,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali kama ifuatavyo:-

(i) Elimu ya msingi maboma 56 kila moja shilingi 17,500,000 mahitaji ni shilingi 980,000,000;

(ii) Elimu ya sekondari maboma 73 kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 1,460,000,000;

(iii) Matundu ya vyoo shule za msingi matundu 20 kila moja shilingi 1,500,000 na mahitaji ni shilingi 30,000,000;

(iv) Matundu ya vyoo shule za sekondari matundu 17 kila moja shilingi 1,500,000 na mahitaji ni shilingi 25,500,000;

(v) Maboma 32 ya Ofisi za Serikali za Mitaa kila moja shilingi 15,000,000 mahitaji shilingi 480,000,000;
(vi) Maboma sita ofisi za kata kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 120,000,000;

(vii) Maboma matano ya zahanati kila moja shilingi 50,000,000 na mahitaji shilingi 250,000,000;

(viii) Maabara tatu katika shule za sekondari kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 60,000,000;

(ix) Ukamilishaji ujenzi wa bwalo Sangabuye Sekondari mahitaji shilingi 10,000,000;
(x) Maabara zahanati moja mahitaji ni shilingi 7,500,000;

(xi) Ukamilishaji Kituo cha Polisi Nyamhongolo mahitaji ni shilingi 25,000,000;

(xii) Ukamilishaji wodi mbili za wagonjwa kila moja shilingi 50,000,000 na mahitaji shilingi 100,000,000; na

(xiii) Bweni la shule ya sekondari shilingi 20,000,000 mabweni mawili ya watoto wenye mahitaji maalum kila moja shilingi 70,000,000 na mahitaji ni shilingi 140,000,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, msaada wa Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ni muhimu sana kwa wananchi wa Jimbo la Ilemela; pili, naomba kilometa 12 za barabara za lami ahadi ya Mheshimiwa Rais tayari tumeshaainisha barabara husika kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Pansiasi kwenda Kiseke kilometa 3.2; na barabara ya Kahama kwenda Kayenze kupitia Nyamhongolo, Shibula, Bugogwa, Sangabuye hadi Kayenze kilometa tisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Ilemela ina upungufu mkubwa wa watumishi katika idara mbalimbali kama ifuatavyo:-

NA. CHEO/IDARA MAHITAJI WALIOPO UPUNGUFU

1. Elimu ya msingi 1943 1492 451

2. Elimu ya Sekondari 1348 1107 241

3. MEO ajira za kudumu 171 86 85

4. MEO wa Mikataba 41 41 0

5. Daktari Bingwa 6
1 5
6. Daktari 38
25 13
7. Daktari Msaidizi 44
9 35
8. Daktari wa Meno 2 1 1
9. Daktari wa Meno Msaidizi 5
1 4
10. Afisa Muuguzi 30
17 13
11. Wauguzi 228 101 127

12. Mteknolojia Maabara 20
9 11
13. Mteknojia Msaidizi Maabara 26 7 19

14. Mteknolojia Mionzi 12
4 8
15. Mteknolojia Macho 5 0 5
16. Mtaalamu wa Miwani 4 0 5
17. Afisa Muuguzi wa Macho 7 0 7
18. Mteknolojia Msaidizi Dawa 46 1 45
19. Afisa Afya Mazingira 54 24 30
20. Msaidizi Afya 111 41 70
21. Tabibu Msaidizi 48 6 42
22. Jumla 4460 3189 1271

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa watumishi ni mkubwa sana ningeomba Wizara ione namna ya kutuongezea watumishi ili kupunguza adha hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.