Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kuchangia bajeti ya Serikali na Mpango wa mwaka 2024/2025.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuchangia katika sekta ya kilimo, kwanza ninaipongeza Serikali kwa kuendelea kuongeza bajeti ya Kilimo. Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu na 65% ya Watanzania ni wakulima ambao wengi wanatumia kilimo cha mkono.
Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali kwa jitihada zake za kununua magari ya kuchimba maji katika maeneo yenye uhaba wa maji, kwani hii itasaidia wakulima kulima kilimo chenye uhakika ambacho ni kilimo cha umwagiliaji.
Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali iongeze magari haya ya kuchimba maji ili yasambazwe katika maeneo mengi yenye uhaba wa maji nchini kwa ajili ya kuboresha kilimo.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuongelea pia kuhusu upimaji wa udongo (afya ya udongo), nchi yetu ina eneo kubwa na kila eneo kuna wakulima wa mazao mbalimbali, lakini wakulima wanalima mazao ambayo hawana uhakika wa mazao yao kustawi katika maeneo hayo na hivyo hupoteza nguvu nyingi na kuvuna mavuno machache kulingana na ustawi wa mazao hayo katika maeneo husika.
Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali iongeze jitihada za upimaji wa udongo katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini ni mazao gani yanastawi wapi ili wakulima walime kilimo chenye tija na kukuza uchumi wa Taifa na mwananchi mmoja mmoja.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.