Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tandahimba
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta kauli ya neno mjinga. Naliondoa kabisa kwenye Hansard. (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante, endelea.
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa namaanisha kwenye mchango wangu ni Serikali inapofanya intervention sukari inapouzwa shilingi 6,000, sukari inapouzwa shilingi 7,000, sukari inauzwa shilingi 5,000, Serikali ikaingilia kati ku-rescue situation, kwa ajili ya wananchi wa Tanzania wapate sukari kwa bei nafuu. Akapatikana mtu akataka kutetea watu ambao kwenye Taifa hili ndiyo wanafanya hizo cartel ambazo, wengine tunao ushahidi, tunaweza kukupa ushahidi ukiutaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nataka nikupe mfano mmoja. Sukari inayouzwa kwenye Taifa hili mkulima wa miwa anayelima miwa Kagera, mkulima wa miwa anayelima miwa Kilombero, mimi ni Mmakonde, Wamakonde sisi kazi yetu ni wamachinga, tunatembea tembea; bei ya tani moja ya miwa Kilombero na Kagera ni tofauti, lakini bei ya sukari ni ile ile wanayoifanya. Leo inakuja Sheria hapa inataka kufanya mabadiliko, jiulize, ukanda huu wakala wa kuuza sukari yupo mmoja, yupo Dodoma hapa, Mkoa wa Manyara hakuna wakala wa sukari pale, pana jambo gani hapa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani kwenye Taifa hili watu saba waweze ku-drive Watanzania milioni 61. Haiwezekani, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, mimi nawapa comfort, Watanzania wana akili wanaona dhamira ya Serikali ya Dkt. Samia, wanaona kinachofanywa na Serikali. Isingewezekana kwa miaka yote tumekaa Bungeni hapa kila mwaka sukari inapanda bei Serikali ikae kimya, ikichukua hatua basi kunakuwa na maneno chungunzima, nawaomba waandishi wetu wa habari wakati unaandika habari, muandishi mzuri wa habari, lazima a-balance story. Yapo magazeti yameandika habari page nne, sijaona balance ya story ya upande wa Serikali wanasema nini, lakini wameweka taarifa kwenye magazeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama Bunge una namna ya kutuongoza. Kipindi kilichopita wapo watu waliandika taarifa ambazo hazikuwa na ukweli na Bunge lilichukua hatua kuwaita na kuwahoji, ili kujua ukweli wa kile kitu na kwenye hili linaloendelea, magazeti kuandika habari ambazo hawajafanya due diligence ya upande wa pili na wenyewe ikiwezekana waitwe wahojiwe tupate ukweli. Hatutaweza kukubali kuendelea watu saba, yaani ni sawa na umechukua ng’ombe wako, halafu mkia sasa ndiyo unaongoza ng’ombe. Yaani watu saba wenye viwanda saba, wao nim kia, sasa ndio wanataka waendeshe watu milioni 61 Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili haliwezekani na Waheshimiwa Wabunge wenzangu Bunge hili tulilonalo ambalo hatujamaliza, wote hapa tumelalamika bei ya sukari. Inapokuja finance bill leo twendeni tukaiunge mkono Serikali tufanye mabadiliko kwenye sekta ya sukari tutakuwa na stability kwenye bei zetu za sukari hapa. Otherwise kila mwaka tutakuwa tunakaa, ikikaribia Ramadhani sukari inakuwa shilingi 7,000, ukikaribia sijui muda gani sukari shilingi 8,000. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimeenda deep sana kwenye mambo haya yanayoendelea ya sukari, hao waliopewa vibali hawajaagiza sukari, vibali vyenyewe wameviuza kwa hiyo, wana migogoro wenyewe, migogoro mingine inakuja ndani. Mimi nawaomba wabunge wenzangu kama njaa zetu zitatoka tumboni zikahamia kichwani, hili Bunge litakuwa la ajabu. Kama njaa zetu zitatoka tumboni kuhamia kichwani hili Bunge litakuwa la ajabu sana, tutashindwa kufikiri kwa kichwa. (Makofi)
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Emmanuel Mwakasaka, Taarifa.
TAARIFA
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, lugha ya staha ni kitu ambacho ni muhimu sana na hasa kwa, siyo tu Waheshimiwa Wabunge, lakini kwa mtu mwingine yeyote. Kusema njaa zitatoka kichwani zinaenda tumboni au tumboni kwenda kichwani, hiki kitu hakijakaa sawasawa kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba Mheshimiwa mchangiaji atumie lugha nyingine kuliko hii anayotumia kwa Waheshimiwa Wabunge, ahsante. (Kicheko/Makofi)
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge nimefuatilia hoja ya Mheshimiwa Katani, ametumia lugha ya sanaa. Nadhani kwa mamlaka niliyonayo namruhusu aendelee. (Makofi)
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kukupongeza na unanipa matumaini makubwa kwamba Ph.D yako haikuwa ya kuungaunga. Kiswahili sanifu kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa namaanisha ni kwenye Bunge hili tuwe tunayatafakari yale tunayoyalilia na pale Serikali inapochukua hatua, kwa ajili ya kumlinda Mtanzania wa kawaida aliyepo Tandahimba, Mtanzania wa kawaida aliyepo Madaba, Mtanzania wa kawaida aliyepo Kiteto, Mtanzania wa kawaida aliyepo Longido, Wabunge tunapaswa kusimama pamoja kuitetea Serikali yetu. Nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge, yapo mambo ya msingi yanafanywa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye mabadiliko haya ya Sheria ya Sukari, Finance Bill inayokuja miongoni mwa dhamira zake ni kwenda kumlinda mlaji wa sukari wa Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa wazi inawatetea sana hawa waendeshaji wenye viwanda vya sukari. Wanapewa maeneo, wanapewa na incentive huko, lakini hawasemi, ni miongoni mwa mabadiliko ambayo Serikali inaendelea kuwatetea watu wenye viwanda. Nachelea kusema uweke watu wako vizuri, haya yanayoendelea mimi najua wapo watu wenye fedha wanazunguka huko nje wanakutana na baadhi ya wabunge kutaka kukwamisha dhamira njema ya Serikali. Ukienda kwenye Hoteli ya Esperanza pale nimekuta watu wanajadili kufanya sabotage ya jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Wabunge wenzetu. Sasa tunapotetea Watanzania ndipo pale...
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma, Taarifa.
TAARIFA
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, namuunga mkono mchangiaji, uncle wangu Mheshimiwa Katani, anachangia vizuri sana, lakini Bunge hili lipo live. Suala hili la sukari limegusa Watanzania wengi sana na watu wanafuatilia Bunge kuhusu huu mjadala. Kwa kuwa, Mheshimiwa Katani, mjomba wangu, amewaona hotelini Wabunge wenzetu wanajadili kufanya sabotage, hili suala tungemuomba Mheshimiwa atusaidie kututajia kwa sababu, hawa ni kama wahaini. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, unapokea Taarifa ya Mheshimiwa Kasheku Musukuma?
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea na nachangia kwa tahadhari kwa sababu jambo hili ndiyo maana unaona nazungumza mambo yale ya Kitaifa, tunasubiri mamlaka nyingine zitakapomaliza tutakapotakiwa kutajana, tutatajana wakati ukifika. Kwa hiyo, mjomba wangu usiwe na shaka, tutatajana tu hapa ndani. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Katani, muda wako umekwisha lakini. (Kicheko)
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
MWENYEKITI: Ninakupa dakika mbili kama huna uhakika una wajibu wa kulinda heshima ya Wabunge. Naomba uondoe maelezo yanayosema kwamba, Wabunge wameshiriki kwenye huo mchakato tafadhali. (Makofi)
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naondoa lakini nitakutafuta kwa wakati wako kukupa taarifa. (Kicheko)