Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninakiri kwamba, Mungu ni mwema ametujalia tena wakati mwingine. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri na timu yao yote ya Wizarani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuongeza hiyo hela waliyoomba ikafikia shilingi 460,333,600,002, lakini bado kwangu naona ni kidogo, tena ni kidogo sana. Nilitarajia itakuwa mara tatu au hata mara nne kwa sababu, tunapozungumzia kilimo shilingi trilioni moja na kilimo ni kwenye ardhi tu, hawa mifugo wako juu ya ardhi na kwenye maji na hela yenyewe hii ni kidogo. Namwomba sana Mheshimiwa Rais wetu ambaye ni msikivu aangalie vizuri hili eneo. Hili eneo ni muhimu kwetu kwa ajili ya chakula tuweze kupata balanced diet, lakini pia, kwa ajili ya export. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia huku ndani kuna waumini wengi wa Janabi. Kwenye ile sahani inatakiwa three quarters ndiyo iwe protein na kingine iwe carbs, yaani carbohydrates, na kadhalika. Ukiangalia protein inatoka kwenye Wizara hii tu. Sasa watoto wanakuwa na kwashiorkor, wazazi tunakuwa na viribatumbo, na kadhalika, tutafika kweli? Maradhi yasiyoambukiza, kama sisi wenyewe hatuli vizuri proteins, hatuwezi kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hawa Wizara ya Kilimo wametuambia kuwa, kuna BBT ambayo mpaka sasahivi kuna vijana 161 na wametoka kwenye mikoa 26. Ukigawanya ina maana kila mkoa umetoa watu sita, ni kidogo sana, lakini ili BBT iwe sustainable kwa vile tuna sera, ni kwa nini badala ya kutumia hizo hela kuanzisha ma-block farms madogo-madogo, wasipelekwe JKT? Hapo kutakuwa hakuna ugonvi. JKT kuna nidhamu, watafundishika na watarudi hapa wakiwa wamekomaa, litakuwa ni jambo zuri. Kwa hiyo, naishauri hii Wizara waingie mkataba na JKT, ili waweze kuwa-train watu wao huko vijana warudi wakiwa wamekaa vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hili jambo liletwe hapa tutunge sheria. Leo Mheshimiwa Bashe yuko kwenye hii Wizara ya Kilimo, kesho akitoka anaweza akaja Mheshimiwa Waziri mwingine akaamua anavyotaka. Hayuko tena BBT anarukia kwingine, lakini kama ni Sheria na sera ziko mahali pake ni lazima wote tutaendelea na mfumo huo na tutazidi kujikuza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwapongeze sana wafugaji au watu private ambao wanaoendesha shughuli hizi za mifugo, wakiwemo watu wa dini, huko mission au kwenye vyuo vya misikiti vya Mabaraza ya Kiislamu, lakini pia hata hao wakubwa. Leo tumekuwa na ASAS, tumeona banda zuri pale na wale wengine wote. Nawapongeza wajasiriamali wote ambao wako kwenye hili eneo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeweza kuoneshwa na tumeonja mazao yao, lakini nimekuja hapa na ombi na kilio. Kila bajeti huwa nakuja na kilio na ombi hilo. Ni rahisi sana kwa mwanamke yoyote wa kijijini kufuga kuku, mbuzi, kondoo, wanyama wengine na pia, ni rahisi hao wanyama kuchukuliwa na kutumika nyumbani. Tunapata mayai, samadi na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilimwomba Mheshimiwa Waziri tufanye cross-breeding. Imefanyika kule kwenye Jimbo la Vunjo, lakini ng’ombe wetu wale wadogo hawakuweza kubeba yule ng’ombe mkubwa kwa hiyo, nyingi ziliharibika. Wanapotarajiwa kuzaliwa zinaharibika... (Makofi)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Raymond, ahsante.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)