Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi naomba nitumie nafasi hii kwanza kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi. Pia namshukuru Mungu kwa kuturuhusu tuendelee tena kuwepo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi napenda nichangie katika maeneo mawili. Eneo la kwanza ni la uvuvi wa vizimba na la pili ni la uvuvi asilia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natumia nafasi hii kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ukitazama ongezeko la bajeti ndani ya miaka mitatu, kutoka shilingi bilioni 160 mpaka shilingi bilioni 460 ambayo inaongezeko la zaidi ya shilingi bilioni 291 tafsiri yake ni kwamba, iko kazi kubwa sana ambayo inafanyika kwenye Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natumia nafasi hii kumpongeza sana ndugu yangu, babu yangu na mjukuu wa Wasukuma, Mheshimiwa Ulega. Vilevile nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wake pamoja na Katibu Mkuu wao na yeye ni mjukuu wa kule Usukumani, Shemdoe, kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi nataka kuongelea maeneo mawili. Nimesema hapa tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri sana aliyoifanya miezi michache iliyopita. Kwa mara ya kwanza uvuvi wa vizimba katika nchi hii ulianzishwa miaka 10 iliyopita pale Nyamagana na Vijana wa Mpanju kwa kutengeneza bwawa la kuchimba. Leo, zaidi ya miaka 10 baadaye, tunazungumzia uvuvi wa vizimba uliotapakaa karibia Ziwa Viktoria lote na maeneo mengine pembezoni mwa Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni hatua kubwa sana ambayo Mheshimiwa Rais muda mfupi uliopita alikabidhi maboti zaidi ya 160 na vizimba 222 katika tukio lililofanyika pale Nyamagana, tukio hili siyo dogo. Ukitazama uhalisia wake ni tunafahamu vijana kwenye vikundi, makampuni mbalimbali na hata mtu mmoja mmoja wamenufaika na utoaji wa vizimba hivi pamoja na mikopo ambayo kiukweli ukitazama kwenye Sekta ya Uvuvi, vijana wetu wamekwenda kupata ajira. Halikadhalika vijana wametengenezewa mazingira rafiki ambayo yanawafanya wasikimbizane sana na mambo mengine kwenye biashara ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya yote viwanda vinavyotengeneza hizi cages viko Mwanza, pale Nyamagana. Tafsiri yake ni kwamba, vimeendelea. Mheshimiwa Waziri nakupongeza sana kwa sababu, umeendelea kutoa ajira kwa namna tofauti tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri ni kwenye hii hatua inayofuata ya cage 800 na zaidi ya maboti 490, tungeweza kuamua. Kwa sababu, ya changamoto zilizoko katika maeneo mengine, sio vibaya wakiamua kuchukua miaka mitatu waangalie kwa Ziwa Victoria peke yake na baadaye watoke nje, ili watu wawe wamepata ufahamu vizuri kuhusu cages na namna ya kuzifanyia kazi, ili vijana wengi zaidi waweze kupata kwenye Ukanda wa Ziwa Victoria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ni kubwa, namwomba sana Waziri atazame vizuri, hasa tunapozungumzia habari ya chakula, ni kingi, lakini gharama yake ni kubwa sana. Jambo la pili ni, atazame namna watengenezaji wa maboti wanapoanza matengenezo ni lazima mkubali kuwashirikisha wadau wenyewe ambao ni watumiaji wa haya maboti, ili yawe na tija na manufaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda, jambo la pili ni uvuvi asilia. Naomba hapa nishauri vizuri; kama unavyofahamu, pamoja na uwekezaji mkubwa ambao tunaufanya, pamoja na jitihada kubwa ambazo anazifanya Mheshimiwa Rais, nakuomba sana Mheshimiwa Waziri, hatuna mbadala wa uvuvi asilia. Ni lazima tuwekeze nguvu kwenye uvuvi asilia. Ndiko kodi inakopatikana, ndiko kuna ajira nyingi, ndiko kuna mchakato mkubwa... (Makofi)