Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mkutano uliopita nilizungumzia fursa ya samaki kwa kuzingatia maji tuliyonayo square kilometre 145,000 nilisema tunaweza kupata dola bilioni tatu, leo tunauza milioni 200.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika diplomasia ya uchumi amekamata soko la Ghuba, wako tayari kununua nyama kutoka Tanzania, potential ya soko lao ni dola bilioni sita, sisi tunauza nje dola 56. Maana yangu ni nini? Pesa tulizowekeza kuchukua masoko haya ni kidogo, soko lipo linatusubiri sisi hatujawekeza pesa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, uhifadhi wa Ziwa, tunahitaji kuhifadhi Ziwa. Mkurugenzi wa Uvuvi anajua, samaki wamepungua kwa asilimia 35 na maeneo ya Tanzania yenye matatizo yanajulikana, wakati umefika wa kuanzisha hifadhi, Mamlaka ya kuangalia hili Ziwa. Uvuvi haramu, overfishing ni tatizo, hatuwezi kusubiri ili kwamba sasa tuweze kwenda kupata hiyo potential ya Vietnam ya dola bilioni tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie ufugaji wa samaki. Nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, ninakushukuru Mheshimiwa Waziri, sehemu za Rushonga, Ihumbo, Bugasha, Kamugaza wote umewaweka kwenye chart tunakwenda kufuga samaki, lakini kufuga samaki lazima viwanda vyako vile ambavyo nimeelezwa na wataalam vianze mara moja. Tunapaswa tuwe na viwanda vya kutengeneza chakula cha samaki kwa sababu kwenye co-structure ya samaki sehemu kubwa ni chakula. Nina uhakika umeshajenga majengo tunataka mitambo ili kusudi tuende mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la mifugo. Nirudie tena, nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, ule mgogoro umekwisha, mgogoro umekwisha sasa Muleba tumejipanga ili kuanza kufuga na Muleba tutakuwa shule au darasa la kuifundisha nchi hii namna ya kufuga. Vitalu vyote viwe vya kufuga si kuchunga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, NARCO wasimamie mikataba to the dots mtu akikiuka nje. Mheshimiwa Waziri, vitalu hivi sasa vilenge kuwatajirisha Watanzania hata Wabunge wakitaka waje hapa, nitawapa darasa wakati wa kunywa chai waende wafuge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wawekezaji wametangulia kwenye sekta ya maziwa hasa Kagera, namzungumza Kahama Fresh. Kahama Fresh alindwe atoke kwenye kuchakata lita 20,000 aende kwenye kuchakata lita laki tano. Ni aibu kwa nchi hii kuchakata lita laki mbili na elfu ishirini na nne kwa siku. Uganda kuna kiwanda kinachakata lita laki nane kwa siku. Mtoto wa Mjomba ana kiwanda kinachakata lita 150,000. Serikali impe nguvu Kahama Fresh. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Heifer International, namuunga mkono Heifer International aanze kugawa mitamba, atupe mitamba sisi tumlipe maziwa Kahama Fresh. Tunataka watu wote, na sisi kwetu tunakushukuru sana kwa kuturuhusu kuingiza ng’ombe wa kisasa, wakulima wote wanakupongeza, Ustaadhi Bashe anakupongeza, tulete ng’ombe kama alivyosema mzee Profesa pale, ng’ombe anayetoa lita 40 kwa siku, hao ndiyo ng’ombe tunaowataka, lakini samadi inayotokana na hiyo inatengeneza kahawa, kahawa ya Kagera iweze kukubalika katika level za kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, watu wote nimeshawaahidi, kuna collection centre Nshamba, kuna collection centre ya Kahama hizo uzilete pale, halafu Mheshimiwa Waziri wakati namalizia ile show tuliyopiga Karagwe tunapaswa tuipige Muleba. Kazi uliyofanya kwa ujumbe uliopewa na Mheshimiwa Dkt. Samia si ya kawaida, tunataka tufanye show ya kibabe mtu anapewa ng’ombe anadaiwa maziwa, lakini lengo letu tunaomba pesa ziongezeke kusudi tuweze kupata mapato zaidi na pesa za kigeni. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa wanaouza nyama nje ya nchi na wanaouza samaki nje ya nchi watuoneshe pesa wanaziweka wapi. Hatuwezi kukaa kwenye namba wakati mtu anauza mnakalia makaratasi halafu angalia wengine wasituuzie invoice tunataka cash dola. (Makofi)