Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZACHARIA PAULO ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kuungana na viongozi wenzangu kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia baraka zake katika Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kuungana na Watanzania wenzangu wote kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia baraka zake katika nyanja mbalimbali za ustawi wa Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoliongoza Taifa letu na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2020 hadi 2025 na Serikali nzima ya Awamu ya Sita.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo langu la Mbulu Mjini kupitia Bunge hili ninawathibitishia umma wa Watanzania kuwa katika miaka minne ya uongozi wa Mheshimiwa Rais wetu, umejenga madaraja la Mto Gunyoda na Udahaya miradi ambayo imekwama kwa miaka zaidi ya miaka 20 kwa zaidi ya shilingi ilioni tatu, Serikali imejenga Skimu ya Umwagiliaji Endayaya ulioshindikana kwa miaka 40 kwa shilingi bilioni nane, pamoja na miradi mingine mingi sana katika sekta za afya, elimu, maji, mawasiliano, nishati, utawala na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nitoe mchango wangu kupitia hotuba ya Mheshimiwa Waziri na maoni ya Kamati yetu ya Bunge. Kwanza Serikali iangalie utaratibu wa kuboresha koo za mifugo kwa kuanzisha mashamba darasa ya ufugaji katika halmashauri ambazo zina mifugo wengi ili kuonesha ufugaji wenye tija kwa kuhamasisha wafugaji wachache wenye mwamko na kushiriki maonesho ngazi za wilaya kabla ya Maonesho ya Nanenane.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Serikali ijitahidi kutoa fedha zote zinazoombwa na Wizara hii kwa kuwa ili kufanikisha malengo na mipango yote kusaidia na kukuza mapato yatokanayo na mifugo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Serikali ifanye tathmini ya ufugaji wa samaki katika maziwa madogo kama vile Babati na Tlawi katika Mkoa wa Manyara ili kuona mpango mzuri wa kutumia maziwa kama hayo kufanya ufugaji wa samaki kwenye vizimba nchini kukuza uchumi wa Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba sana Serikali itoe fedha za majosho matano yaliyopitishwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 na kuwa Mheshimiwa Waziri nimekuomba sana mara nyingi kwani ni hitaji la wananchi katika kata kumi za vijijini na huduma hiyo haipo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaiomba Serikali yetu ijitahidi kuajiri maafisa ugani katika sekta ya mifugo na uvuvi kwani kuna upungufu mkubwa sana wa maafisa hao na mfano ni Halmashauri ya Mbulu Mjini ina mahitaji ya maafisa 43 walioko wako saba tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga hoja mkono 100% na naomba kuwasilisha.