Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Namshukuru Mungu kwa kuwekwa hapa leo na kuweza kuzungumzia Wizara hii ya Elimu, niseme kwamba imekuwa vizuri Profesa Mkenda ametuletea hotuba yake ambayo inajadilika na imewekwa kwenye kitabu kizuri sana hata hii niliyoshika ni randama tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema tukajua kwamba mtu anaweza kukuibia kila kitu tangible au intangible lakini hawezi kukuibia elimu yako kwa sababu imefichwa na Mungu ndani ya ubongo kwenye medulla oblongata. Unakuwa nayo wewe mwenyewe na unaimiliki wewe mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumteua Profesa Mkenda kusimamia Wizara hii na timu nzuri sana, toka jana tunazungumzia maprofesa, Katibu Mkuu naye ni Profesa ina maana kuwa elimu kwao imetua na imebarikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshika hiki kitabu cha randama, kuna mambo ambayo naomba uniruhusu ninukuu. Majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yameainishwa katika hati idhini iliyotolewa tarehe 7 Mei, 2021 (GN. 385) na marekebisho yalitolewa tarehe 24 Januari, 2022 (GN. 57b) ambapo Wizara imeelekezwa kutekeleza majukumu yafuatayo, yako pale majukumu kama 17. Ni mengi lakini siendi huko kote, mimi leo nimesimama kuzungumzia jukumu moja tu, kusimamia maendeleo ya elimu ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukizungumzia elimu, tukienda Serikali za Mitaa kuna elimu na kila mahali, mimi nimekwenda kwenye kusimamia maendeleo ya elimu ya juu nikiwa na maana ya vyuo vya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetamkiwa safu ya maprofesa walisoma wakapata PhD zao wakawa madokta na baadaye wakaandika wakawa ma-professorial ambacho sasa hicho ndicho kiwango cha juu ulimwenguni. Tunao na wanaendelea kufundisha watoto wetu. Kwa nini nimependa kuwazungumzia? Kwa sababu nimeona kwamba kuna eneo ambalo watu hawa wanapunjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Moshi Cooperative University wakati imetoka chuo cha kutoa Diploma na mengineyo na bado ikashirikishwa na kile Chuo cha Sokoine University then ikapewa kuwa University, walichukuliwa maprofesa pale, wengine wakiwa Associates Professor na wengine full Professor wakapewa contract wakafundisha kwa moyo mzuri tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameisema pia Mheshimiwa Dkt. Ntara kabla yangu kuwa Maprofesa hawana hili la kusema kugoma wala nini, walikuwepo maprofesa kama 15 wamefundisha na wengine tumefanya Masters pale tume-graduate lakini mpaka leo wanadai stahiki zao na hawajawahi kupewa. Jambo hili wakanikabidhi nikazungumza na Waziri wa Fedha, madai hayo yakawa hayajafika. Nikazungumza kwenye Wizara ya Elimu wakasema wamekwishapeleka fedha, nikarudi Wizara ya Fedha, Naibu Waziri wa Fedha akaniambia madai hayo yameshahakikiwa yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba chonde chonde, baadhi yao wameshakufa, baadhi yao wamebakia na familia zao zina-suffer, Wizara iwapatie Maprofesa wale stahiki zao. Pia, namshukuru Mungu leo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu, Waziri wetu wa Fedha nchini yuko hapa na anakisikia tena hiki kilio. Pia, wao wako kule sasa hivi wananisikiliza, maana yake waliona waliponituma nimeshaulizia swali na swali halijaja, leo niseme wazi kwamba maprofesa wanasononeka! Nisingetaka wapate stress, walipwe ili waendelee kufundisha. (Makofi)

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongezee katika mchango mzuri unaoendelea. Hata stahiki zao za nyumba (house allowance) madai ni mengi, naomba na hilo katika hizo stahiki zao walipwe na house allowance fedha ambazo hawa maprofesa wanastahili, madai ni mengi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shally Raymond, unaipokea hiyo taarifa?

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea sana hiyo taarifa ya Daktari, anawajua wenzie zaidi, ahsante. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile ameshatoa hiyo taarifa naomba hilo nihitimishe. Mwaka wa Fedha 2023/2024 hii Wizara walikuja hapa wakaomba zaidi ya 1.6, tukawapa lakini mpaka sasa hazijatoka zote. Tatizo liko wapi? Kwa sababu ukiniuliza ni Wizara gani ipewe fedha nyingi zaidi hapa nchini? Nitakwambia ni Wizara ya Elimu kwa sababu elimu ndiyo itamkomboa kila mtu. Ukiwa na elimu utajua kulima, utaweza kilimo, utaweza mifugo, utaweza kujitunza, hakuna kipindupindu. Ukishapata elimu iwe ni ya level ya chini ya primary, secondary, ukishaelimika tu unaweza kujitambua na kujisimamia. Sasa kwa nini elimu isipewe kipaumbele? Mimi leo ningesema wapewe hata trilioni tatu, lakini basi kwa vile inaingia maeneo tofauti hadi kwenye Halmashauri, mpaka wapi, nyingine huwa zinakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba tu niulize kwa sababu jambo hili linazungumzwa kichini chini, ni nini kilichopelekea kufa kwa ushindani wa ufaulu wa shule za sekondari? Mpaka sasa hatujui kwamba labda walikuwa wakitolewa kwenye ushindani walikuwa wana-market shule nyingine? Kwa hiyo, mbona tukienda kiulimwengu tunajua kuwa kuna best universities? unakuta kuna Harvard University, Oxford University na university nyingi tu kutoka nje, tena bahati nzuri sasa hivi una-google tu, best universities in the world. Wizara wanafikiri hizo university zinakuwa best bila kuwa na best brains? Wengine hapa wamesoma huko, lakini Watanzania tuna uwoga tunaona kwamba tukisema best students sijui best schools tunadidimiza, hapana! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema wazi hapa kwamba Serikali lazima ipewe njinga njinga na private schools, shule za seminary yaani ipewe you know mikiki mikiki ili na yenyewe iamke. Kwa jinsi Mungu alivyotupangia akili anatoka mtoto kwenye shule ya sekondari ya Kata anawazidi wale wa hizo private schools. Sasa kwa nini walitoa ile na hawakutuletea na sisi tukajadili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona kwamba, ushindani ni kitu kizuri. Nilisoma Kifungiro na nililelewa kujua kwamba mimi ni kiongozi, toka niko standard four najua mimi ni kiongozi. Nikawa Head Girl na kokote nilikokaa nilichaguliwa kuwa kiongozi na leo mimi ni kiongozi wa Wabunge Wanawake hapa. Najiamini na najitambua kwa sababu mimi nilijengwa kichwani kwangu kwamba, hata kama hunikubali lakini I know it.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hilo? kwa sababu mwanafunzi yeyote lazima ajengewe confidence. Sasa kwa ushindani ule ndiyo ulikuwa unafanya shule za seminary zituoneshe sekondari za Serikali ziendeje, unafundishwa maadili na unafundishwa mambo mengi. Sasa naomba atakaposimama Profesa Mkenda, atueleze tu ni nini kilichoondoa ule ushindani? Tusiwe waoga, hakuna nidhamu ya woga kwenye mikoa hii tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, naomba ile hela waliyoomba wapewe yote na nimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliona kwamba ni vema basi mwanafunzi akipata ajali kwenye mahusiano hususani yule wa gender ya (KE) na hata huyu kijana akiweza warudishwe shuleni waendelee tena kujielimisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)