Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Amina Daud Hassan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Spika, naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika Wizara ya Elimu na maendeleo kwa wanafunzi wetu. Vilevile nampongeza Mheshimiwa Waziri, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri na uongozi wake wote kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa ikitekeleza mkakati wa elimu jumuishi unaowaweka pamoja wanafunzi wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu. Lengo hasa la mkakati huo ni kuleta usawa na kuondoa unyanyapaa na ubaguzi kwa watoto wenye ulemavu ambao waliachwa nyuma kwa sababu ya imani potofu.

Mheshimiwa Spika, kuna uhaba wa fedha ya kukidhi mahitaji ya elimu jumuishi, unyanyapaa, miundombinu isiyo rafiki na kukosekana kwa malezi ya ziada kwa wanafunzi hao. 67% ya walimu wake walikiri shule zao kutokuwa na walimu waliobobea kufundisha wanafunzi wasioona, hivyo ni lazima Serikali iandae mazingira rafiki zaidi kwa watu hawa kupata elimu sawa na wanafunzi wengine ili kupunguza unyanyasaji.

Mheshimiwa Spika, ili kumaliza changamoto za elimu jumuishi, utafiti huo unapendekeza wadau wote ikiwemo Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, walimu, wazazi au walezi kushiriki katika kuleta mabadiliko haya.

Mheshimiwa Spika, mazingira magumu ya shule na vyuo vikuu hasa ukosefu wa mabweni husababisha wanafunzi wadogo kuanza maisha ya kujitegemea yasiyo na ulinzi wala huduma wezeshi katika kujikimu. Hii husababisha ngono za mapema, ukatili wa kijinsia na mimba zisizotarajiwa.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ongezeko la kupata mimba kwa wanafunzi wanaoishi ghetto na chanzo kikubwa cha mimba hizi ni kutolindwa kwa ma-ghetto yaliyozunguka chuo, na na kukosa mahitaji ya muhimu kutoka kwa wazee/walezi wao ambao hawajui kinachoendelea kuwa wanafanya majukumu yote ya ndoa.

Mheshimiwa Spika, hilo boom haliwatoshi. Serikali ihakikishe kama wanalipia ada moja kwa moja vyuoni, basi na mabweni walipiwe moja kwa moja ili isiwape nafasi ya kutoka kwenda kupanga mazingira mengine yanayosababisha uharibifu wa tabia.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.