Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, naomba kushauri kwamba vyuo vikuu vikabidhiwe majiji au halmashauri ili kukiwa na shida au changamoto yoyote, basi chuo hicho kinaweza kufanya tafiti kulingana na issue iliyopo na hiyo itafanya impact za vyuo zionekane direct kwa wananchi, na chuo kikuu kinakuwa ndiyo mlezi wa halmashauri au jiji. Hii itakuwa kama wafanyavyo Japan au Indonesia na inasaidia kuona chuo kiko karibu na jamii.

Mheshimiwa Spika, aidha, wanachuo waruhusiwe kufanya exchange program hata ndani ya vyuo vyetu, kwa mfano, kutoka MUST kwenda UDOM au UDSM kwenda Nelson Mandela na kadhalika. Kwa kufanya hivyo, wanafunzi wanajifunza na kubadilishana ujuzi mbalimbali, hivyo ku-gain jambo ambalo halipo kwenye home university.

Mheshimiwa Spika, pia vyuo vikuu vishiriki ambavyo vilitajwa katika kila mkoa vioneshe angalau maendeleo yao yamefika wapi. Mfano, campus ya Uhasibu Arusha na Songea hakuna kinachoendelea. Aidha, kuna maeneo kama Ruvuma, vyuo vikuu binafsi vyote vimekufa. Hivyo, naiomba Serikali itafute njia ya kukibeba chuo kama Peramiho, RUHUWIKO na AJUCO Songea wasaidiwe katika eneo ambalo wamekwama.

Mheshimiwa Spika, kuhusu retirement age, maprofesa na madaktari waendelee kufanya kazi kuanzia miaka 65 hadi 85 kwa kuwa kazi yao itakuwa zaidi ku-mentor na kuandika maandiko ya tafiti.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa idadi ya wahadhiri ni ndogo sana, vyuo vipewe autonomy ya kuajiri kutoka nchi mbalimbali ili kuweka maana ya university.