Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia hotuba ya Wizara hii ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2024/2025.

Mheshimiwa Spika, nitachangia hoja hii kwa kuanza na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kwanza, naipongeza sana Serikali kwa kuendelea kuongeza fedha za mikopo ya elimu ya juu na hivyo kuongeza wanufaika wa mikopo hii ambao kimsingi wengi ni vijana na pia napongeza hatua ya Serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, lakini bado gharama ya kugharamia mikopo wa elimu ya juu ambayo ni asilimia kubwa ya bajeti kila mwaka, mfano mwaka huu ni zaidi ya 60% ya bajeti nzima, tena fedha hizi zinahesabiwa kama recurrent expenditure (miradi ya maendeleo).

Mheshimiwa Spika, ili fedha hizi zistahili kuwa sehemu upande wa miradi wa maendeleo ni lazima ziweze kuzalisha na kufikia hatua fulani. Bodi isitegemee tena fedha za Serikali kujiendesha, ziwe revolving zenyewe.

Mheshimiwa Spika, wakati Waziri anahitimisha, atueleze kwa nini Serikali mpaka leo haioni haja ya kuleta fungu mahususi la fedha za kugharamia elimu ya juu?