Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana, kwa kunipa nafasi, nami niweze kuchangia kwenye Wizara hii ya Ujenzi. Nami nianze kwa kusema moyo usiyo kuwa na shukrani hukausha mema yote. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, sisi Wanambeya, sisi Wanabusokelo pamoja na wasadizi wake Mheshimiwa Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na timu yote, kwa kutembelea Jimbo la Busokelo na kuona hali halisi ya miundombinu ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mara mlipotembelea Mheshimiwa Waziri, mwaka jana mkiwa na Waziri wa Fedha, mliona ile barabara ya kutoka Katumba - Suma – Mwakaleli - Langwa - Mbambo mpaka Tukuyu Mjini, leo hii barabara ile tumesaini mkataba na tunasubiri Mkandarasi aanze kazi. Tunawashukuru sana tena sana, kwa sababu ni barabara ambayo hakika Waheshimiwa Marais wengi wamepita, lakini Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amethubutu. Maana tangu enzi za Mwalimu Nyerere ile barabara ilikuwa ikiahidiwa yenye kilometa 56. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barabara hii ni lango kuu la uchumi wa Wanarungwe, wa Wanambeya, kwa sababu kule tunalima mazao mengi, tunafuga, lakini zaidi ya yote gesi asilia inatoka kule aina ya Kabondayoksaidi. Kwa hiyo, uwepo wa mkandarasi ambaye ameshaonyeshwa site hii, tunaiomba Serikali, tunaiomba Wizara ya Fedha, advance payment iweze kufanyika mapema ili kazi ianze mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze pia kwa kushukuru kwa barabara ya kutoka Mbambo mpaka Tukuyu, Bujesi yenye kilomita 10 ambayo imeshakwisha kamilika. Nashukuru pia barabara ya kutoka Tukuyu Mjini mpaka Kibanja yenye kilomita saba ambayo pia imekamilika na barabara ambayo bado ni ya kutoka Luteba mpaka Ipelele kwa wenzetu Makete. Mheshimiwa Waziri, ulivyokuja uliona, tunaomba sana barabara hii iweze pia kukamilika, kwa sababu inaunganisha kati ya Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Njombe. Tunaombeni sana Serikali iweze kuliona hili, kwa kuwa kule kuna fursa nyingi za kiuchumi pamoja na utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ningeshauri mambo yafuatayo machache; Waheshimiwa Wabunge, wengi wamezungumza suala la bajeti haitoshi. Ni kweli haitoshi, lakini nini tufanye kama Taifa? Mataifa yote yaliyoendelea asilimia kubwa pamoja na China wana Benki maalum kwa ajili ya ujenzi. Tungekuwa na benki maalum kwa ajili ya ukandarasi wa Tanzania maana yake hata mafungu ambayo leo hii tunasema hayatoshi, huenda angalau yangeweza kukidhi kiwango kwa asilimia fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, katika ujenzi wa barabara tuna teknolojia nyingi ambazo zinatumika; duniani kote tuna teknolojia zaidi ya 100 teknolojia, lakini Tanzania teknolojia tunazozitumia hazizidi saba. Niwashukuru Wizara mmeshaanza ku-practice hata teknolojia nyingine mpya sasa hivi. Tuongeze kasi zaidi, kwa sababu zile teknolojia ndizo zinazopunguza gharama ya ujenzi wa Barabara, vinginevyo, tukiendelea kutumia teknolojia za zamani zile automatically gharama za barabara zitakuwa kubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia, na Mheshimiwa Waziri kwa kuwa wewe ni mtu ambaye una exposure ya Kimataifa. Technical timu yako ikitumwa kwenye Mataifa ambayo wanatumia teknolojia ambazo wanatumia udongo katika maeneo ya barabara husika. Kwa mfano, mngekuja kule Busokelo mngetengeneza barabara ile ya Mbambo ile tunaizungumzia sasa hivi Tukuyu ama ya Katumba mpaka Suma kwa kutumia udongo halisi wa kule. Automatically, gharama zake zingeshuka na tungeokoa na tungetengeneza barabara nyingi zaidi ndani ya Taifa letu la Tanzania. Kwa hiyo, tukazanie tuweke mkazo zaidi katika suala la tafiti za teknolojia mpya katika kutengeneza barabara zetu hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshukuru sana pia Manager wangu wa Mkoa TANROADS na timu yake yote. Sasa hivi kule mvua zinanyesha na timu yako Mheshimiwa Waziri, mmezunguka sana. Hivi tunavyosema Rungwe mvua inanyesha na bado barabara zimeharibika. Tunaomba kama ambavyo mmetusaidia huko nyuma muweze kutusaidia tena.

Mheshimiwa Spika, kwenye barabara ya TANZAM ambayo ndio barabara kuu ya uchumi wa Wanambeya na Watanzania wote na ambayo ndio inapitisha mizigo mingi na ndio lango kuu la uchumi wa SADC. Tunaomba sana Mheshimiwa Waziri tunajua ipo kwenye EPC+F. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maeneo haya ambayo ni ya kimkakati, kwa sababu ikiboreshwa ile automatically fedha nyingi za nchi za Congo, Zambia mpaka South Africa kwa kuwa mabasi au trucks zote zinapita kule. Barabara hii itafungua zaidi fursa za kiuchumi pamoja na nchi za Malawi. Kwa hiyo, tuipe uzito mkubwa barabara hii ya TANZAM, kwa sababu ni ya kimkakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukija kwako wewe ambaye ni Rais wa Mabunge duniani, Mbunge wa pale Mbeya Mjini na Spika wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuna barabara ya by pass sisi Waheshimiwa Wabunge wote tunapita pale mjini. Ili twende Majimboni kwetu lazima tupite Mbeya Mjini, sasa hivi mkandarasi anadai bilioni tisa hajalipwa, ndio maana ile njia ya four-way inachelewa, kwa sababu ya madai ya mkandarasi. Tunaomba Wizara muone kwa umuhimu katika kufungu lango hili la barabara katika Mkoa wa Mbeya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo niishukuru tena Wizara, nimshukuru Mheshimiwa Rais, kwa namna ambavyo ametuona sisi Wanabusokelo, Wanambeya na Watanzania wote katika miundombinu. Ahsante sana. (Makofi)