Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Njombe - Songea imeharibika vibaya, barabara ilijengwa zamani na Kampuni ya Buffer Beat ya Marekani ambao walijenga kwa kiwango. Sasa hivi barabara inahitaji siyo ukarabati bali ujenzi uanze upya.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Songea - Tunduru imejengwa na ina umri wa miaka karibu sita, leo hii ukienda barabara imekwishabomoka kwa sababu ya magari makubwa ya mkaa wa mawe. Barabara zinajengwa kwa kufuata design zinazowekwa, lakini magari yanaruhusiwa kupita na uzito wa ajabu.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa reli Mtwara-Mbamba Bay unasuasua mno, ni ahadi tu, hii inasababisha barabara itumike hovyo. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inabidi wakae pamoja ili kunusuru na kuzuia upotevu wa fedha za ukarabati. Wakati mwingine ni hujuma au kitu gani ili wenye magari labda waendelee kufaidika na reli isijengwe kwa ajili ya usafiri. Barabara zitazidi kubomoka kama Serikali haitakuwa makini kwenye kusimamia matumizi mazuri ya barabara. Tunahitaji reli Kusini ili kuokoa barabara zetu.