Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha mchango wangu kwa maandishi.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya ya kuweza kuwepo kwenye Bunge lako Tukufu. Naomba pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya katika kuwatumikia Watanzania.
Mheshimiwa Spika, naanza kwa kuunga mkono hoja iliyopo mbele yetu na baada ya kuunga mkono hoja naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote walio chini ya Wizara.
Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mwanga kwa kazi kubwa anayoifanya ndani ya mkoa wetu, hakika mwanamama huyu amekuwa msaada mkubwa sana.
Mheshimiwa Spika, naomba nichangie katika maeneo machache kama ifuatavyo nikianza na suala la kumlipa kwa wakati mkandarasi anayejenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Matai kwenda Kasesya Border ambayo ni barabara muhimu sana kiuchumi kwa Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla. Kukamilika kwa barabara hii itapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa malori katika mpaka wa Tunduma na pia kwa wasafiri wanaoelekea nchi za Uganda, Burundi na Rwanda ikiwa ni pamoja na kuelekea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa kutokea nchi zote zilizo Kusini mwa Afrika.
Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kusaidia bandari yetu ya Dar es salaam kuwa na ufanisi na kupunguza msongamano katika mpaka wa Tunduma ni pamoja na kujenga kipande cha barabara kwa kuanzia Mji Mdogo wa Laela kwenda Mwimbi hadi kwenda kuunganisha barabara ya kwenda Kasesya kipande ambacho Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri wametembelea na kujiridhisha na umhimu wa barabara hii kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, pia kufanya marekebisho maeneo yaliyoharibika kutokana na mvua nyingi iliyonyesha katika Wilaya na Jimbo la Kalambo na hivyo kuharibu barabara nyingi na hasa zinazotumika kusafirisha mazao ya wananchi na hivyo kukosa bei yenye tija kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha