Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Spika, pia nimpongeze Mheshimiwa Bashungwa ambaye ni Waziri mwenye dhamana ya Miundombinu, pamoja na timu yake yote.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Lushoto lina barabara za TANROADS mbili tu ambazo ni Magamba hadi Mlola kilometa 40 na kilometa sita a,bazo zimeshajengwa kwa lami, kwa hiyo bado kilometa 34 na hizi kilometa 34 zimeshaingizwa kwenye utaratibu wa kuanza kujengwa, lakini toka iingizwe kwenye mfumo wa kujengwa mwaka jana mpaka sasa bado haijatengewa fedha kwa ajili kujengwa kwa barabara hii.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ninaiomba Serikali katika kipindi hiki cha Bajeti itengewe fedha kwani barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, aidha, barabara ya kuanzia Nyasa Darajani kupitia Gare hadi Magamba ambayo ina kilometa 19 na hii ni barabara muhimu sana kwani ndiyo mkombozi hasa pale Barabara ya Magamba - Lushoto inapopata changamoto. Kwa kuwa barabara hii ni muhimu sana na ni ya changarawe kwa baadhi ya maeneo, niiombe Serikali kwa kipindi hiki cha bajeti barabara hii itengewa angalau kilometa kumi za lami ili zijengwe hasa kwenye maeneo korofi.

Mheshimiwa Spika, barabara yetu ya kuanzia Mombo kupitia Soni hadi Lushoto yenye urefu wa kilometa 32 barabara hii imekuwa nyembamba sana na kupelekea magari makubwa kupita kwa shida na kuongeza gharama za bidhaa madukani kuwa za ghali kwa sababu ya kupita magari ya tani kumi na changamoto hii nimeshaisemea hapa Bungeni kwa muda mrefu tangu mwaka 2016 kwa ajili ya kupanuliwa hasa kwenye zile kona.

Mheshimiwa Spika, ili kuondoa adha ya wananchi wangu wanayoendelea kuipata, sambamba na hayo naomba kwenye bajeti ya hii barabara hii itengewe fedha kwa ajili ya kuanza kutanua kona pamoja na kuongeza upana wa makalavati.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Meneja wa TANROADS Engineer Singano anafanya kazi kubwa mno. Engineer huyu halali, hata umpigie simu usiku, atapokea na kisha muda huo huo anatatua changamoto yako bila kusahau kuipongeza na timu yake pia wanafanya kazi kwa ushirikiano wa kiwango cha juu sana.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.