Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Hon. Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri na timu nzima ya Wizara kwa kazi kubwa ya kuwatumikia Watanzania, hongereni sana.

Mheshimiwa Spika, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri amebainisha ujenzi wa Barabara ya Handeni kwenda Mafuleta kilometa 20, mkandarasi huyu anafanya kazi kwa kusuasua sana, ipo haja asimamiwe kwa karibu Wana-Kilindi wanataka kipande kiishe kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, mkandarasi huyu pia Serikali imempa kujenga kipande cha Mafuleta had Kileguru kilometa 30, je, ni lini ataanza kujenga kipande hiki? Naomba Mheshimiwa Waziri kupata majibu leo.

Mheshimiwa Spika, barabara hii kipindi cha mvua ya El-Nino iliharibika sana, hivyo ipo haja kipande chote kijengwe kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, niombe pia barabara ya Kibirashi – Songe - Kweluguru ifanyiwe ukarabati, nayo haipo sawa baada ya mvua zilizonyesha kupita kiwango.

Mheshimiwa Spika, mwisho ipo ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. Magufuli ya ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa tano, ni kilometa 0.9 tu zimejengwa Makao Makuu ya Wilaya, je, ni lini ahadi hii itakamilika?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.