Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Amina Daud Hassan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kutafuta fedha za kuendeleza maendeleo katika nchi yetu. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na watendaji wake wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuendeleza maisha bora katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapitio ya hali ya uchumi kwa mujibu wa Taarifa ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uchumi wa dunia ulikua kwa wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.5 mwaka 2024 na unatarajiwa kukua kwa asilimia 3.2 na asilimia 3.3 kwa mwaka 2024 na 2025 mtawalia. Kwa hiyo, uchumi ulikuwa kwa wastani wa asilimia 1.7 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 2.6 mwaka 2022 na unatarajia kukua kwa asilimia 1.7 na asilimia 1.8 Mwaka 2024 na 2025 mtawalia na ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulikua wastani wa asilimia 4.6 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2022 na unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024 na asilimia 6.1 mwaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji wa uchumi wa Taifa, Serikali inaonesha kwamba, mwaka 2023 pato halisi la Taifa Mwaka 2015 lilikuwa shilingi trilioni 148.39 kutoka shilingi trilioni 141.25 mwaka 2022. Sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 4.1 mwaka 2022 na shughuli za uchumi zilizochangia ukuaji huu ni kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa madaraja ya juu na miundombinu ni mchango mkubwa katika kuchochea uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa. Ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi ambalo utekelezaji wake umefikia 93% na linatarajiwa kumalizika mwaka 2025 pamoja na madaraja ya juu ya Dar es Salaam. kukamilika kwake kutaongeza ufanisi katika shughuli za kiuchumi, kukuza biashara na kuvutia wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha Kimataifa. Serikali itumie mpango wa kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kwa kutumia ECGA, ili kukamilisha vipande vyote vilivyobaki kwa haraka, hususan vipande vya Uvinza, Malagarasi, Msagati na Kaliuwa, Mpanda na Karema. Pia, Serikali itumie fursa ya uwepo wa sheria ya mfumo wa kukaribisha sekta binafsi kutumia miundombinu ya reli kwa makubaliano ya malipo ili kuvutia wawekezaji katika reli ya SGR.