Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watumishi wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi. Hoja yangu au rai yangu ni kwamba Serikali iweke alama za mpaka haraka iwezekanavyo ili wananchi wafanye shughuli za kimaendeleo. Aidha, bado utoaji wa hati unachukua muda mrefu sana, hivyo nimwombe Mheshimiwa Waziri jambo hili litafutiwe ufumbuzi.
Mheshimiwa Spika, Wana-Kilindi wamefarijika sana kupata mradi wa matumizi bora kwa vijiji 83.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.