Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri sana na zaidi kwa ushirikishwaji. Kama mwakilishi wa wananchi napata ushirikiano mkubwa kuanzia ngazi ya watu wenu pale halmashauri hadi kwa Kamishna Msaidizi pale mkoani. Kwa kweli sina malalamiko, nawapongeza pia hata watendaji wa ardhi hapa Dodoma, Kamishna Msaidizi na wasaidizi wake wote wanafanya kazi vizuri sana, hata pale Jiji wanajitahidi sana, malalamiko yaliyopo naamini ni kutokana na kuzidiwa na kazi, lakini pili kutokana na ukweli kwamba ile kuwa wamerithi baadhi ya migogoro kutoka kwa iliyokuwa CDA, nitafafanua baadaye.
Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi naomba kutoa ushauri na maombi nikianza na Baraza la Ardhi Mufindi; wananchi wa Mufindi wanalazimika kwenda Iringa kupata huduma za Baraza la Ardhi, mara ya mwisho niliambiwa kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha suala hili, ninaomba watusaidie kukamilisha suala hili, Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Mkoa anaweza kuwapa picha kamili, imagine mwananchi anatoka Mgololo, Sadani, Malangali, Mtula, Kisada na kadhalika mpaka Iringa, kwanza lazima asafiri mpaka Mafinga alale, siku ya pili asafiri hadi Iringa, is too costly, nawaomba watusaidie jambo hili likamilike.
Mheshimiwa Spika, pili, ni kuhusu revolving fund kwa ajili ya kupima industrial park; wakati wa bajeti ya mwaka jana na wakati wa semina ya kutujengea uwezo wa mradi wa LTIP, niliwafahamisha kwamba Halmashauri ya Mji Mafinga tumetenga eneo la ekari 750 kwa ajili ya Industrial Park na nikaomba kama sehemu ya utekelezaji ya mradi huo, tupimiwe eneo hilo, lakini niliambiwa kwamba tutapewa fedha kupitia revolving fund, nafahamu changamoto ambazo wamezipata baadhi ya halmashauri kwa kubadilisha matumizi ya hizi fedha, ninaomba dhambi ya wengine isituumize sisi watu wa Mafinga, kwa hiyo ninaendelea kuomba kwa msisitizo watupe fedha hii, wataona maajabu. Mafinga na Mufindi kwa ujumla ina viwanda vya mazao ya misitu 35 na uhitaji bado mkubwa ingekuwa jambo jema sana kupima industrial park.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kiliniki za ardhi; nawapongeza sana, mimi ni mnufaika wa kiliniki za ardhi kwa sababu mmeweza ku-unlock mambo mengi sana siyo ya kwangu binafsi, lakini ya baadhi ya wananchi, ndugu na jamaa, pamoja na kuwa watu wanasema Waziri utachoka.
Mheshimiwa Spika, ni kweli anachoka, lakini kilicho muhimu Mheshimiwa Waziri ameleta amshaamsha ambayo kwanza imeleta woga kwa matapeli wa ardhi, lakini pili imeleta matumaini kwamba kumbe haki inaweza tu kupotea kwa muda, lakini iko siku haki itarejea kwa mwenye haki. Hata hivyo, nina ushauri, walau Mheshimiwa Waziri siku moja moja uweke clinic at village level ambako nako kuna shida kama maeneo ya mjini.
Mheshimiwa Spika, kuhusu migogoro Dodoma vs CDA vs wataalam, mimi nina ushauri kwa Jiji la Dodoma and I will be very honest kwamba ile kurithi sheria delicate iliyokuwa ya CDA imeacha makovu mengi kwa pande zote kwa maana kwa upande wa wataalamu na kwa wananchi, kwa hiyo katika kupata suluhisho migogoro ya Dodoma inahitaji utulivu na umakini mkubwa sana, hapa Dodoma hata aje Malaika kama hatutaanzia kwa iliyokuwa CDA, tutaumiza watumishi, tutawapeleka TAKUKURU, tutawafukuza kazi, lakini nawaambia Dodoma ni unique case, kwa hiyo ushauri wangu wa kwanza Serikali ipime viwanja kwa mfano 1000, ikawa kama benki ndogo ya ardhi kama viwanja mbadala vya watu wenye migogoro ya ardhi, itasaidia.
Mheshimiwa Spika, la pili, migogoro ya kimakundi kwa mfano wale wananchi 562, hakikisheni migogoro ya aina hii maelekezo yakitoka yanatekelezwa, kwa sababu unakuta jambo linaenda, linarudi nyuma, linaenda linarudi nyuma, hii inaleta sura kwamba Dodoma ni ya migogoro, kumbe ni kwa sababu tu, migogoro haiishi.
Mheshimiwa Spika, kama Mbunge ambaye ninaishi hapa Dodoma kwa almost 70% ya muda wangu ninakutana na hizi kero mfano ikiwa ni huu mgogoro wa wananchi 562, maarufu kama Nala Shell Mbili. Tukiweza kumaliza migogoro ya makundi tutawasaidia wananchi wa Dodoma na sura hii kwamba Dodoma ni ya migogoro tutaifuta.