Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia kwenye Bajeti Kuu ya Serikali. Kabla sijaanza nina mambo mawili niyaseme, amemaliza kuongea Mheshimiwa Mbunge aliyechangia na jana yamezungumziwa. Hayo majanga mnayoyasikia yamenipata mimi, Asimwe aliyekatwa miguu tunatoka kata moja, lakini huyo ni Asimwe, kwetu kwenye Kisiwa cha Uchumi Gozba, vijana wamechukuliwa na watu wanaojulikana mmoja wakampiga na wakamtosa kwenye maji. Ninaiomba Serikali na nilifarijika nilipomwona Mheshimiwa Waziri Mkuu, watendaji walioko Wilayani Muleba na Kagera waongezewe nguvu, hayo Wabunge wanayoyasema, watendaji walioko kule wanahitaji nguvu za ziada na wataalamu wa intelijensia kusudi watu wapate haki yao hapa duniani, siwezi kuzungumza zaidi litaniumiza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, ninapopigana kuijenga upya Rutoro nina matatizo mawili, Mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga umeme Rutoro hafanyi kazi, inaniletea shida na tatizo lingine Rutoro, kuna watu wanakiuka tamko la Serikali pale ambapo Mheshimiwa Rais alisema wawe wafugaji na huku wawe wakulima. Sasa kwa wakulima kuna watu wanakiuka maelekezo ya Mheshimiwa Rais, wanapeleka ng’ombe kule. Ninashukuru Mheshimiwa Fatma akiwa Hijja Makkah ameniambia ngoja arudi na maji ya zamzam atawafukuzia mbali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nihutubie Taifa, nianze kwa kuwapongeza Mawaziri kwa hotuba zao na nitaanza na Waziri wa Mipango, anasema kupanga ni jambo moja na kutekeleza ni jambo lingine. Sisi tumeamua kutekeleza, tumezipitia bajeti za kisekta tumezimaliza, sasa tunakuja kuwapa baraka kusudi tutekeleze. Angalizo langu kwa Serikali, hii dhana ambayo wanataka kuipigania sana, dhana ya KPI (Key Performance Indicator) ni suala la kawaida, lipo, lakini inaonekana katika Mpango huu wa 2024/2025 wanataka kuliwekea nguvu zaidi kwamba tuwe tuna vipaumbele, sawa tunavijua, tuwe na nidhamu ya utekelezaji, tumekuwa tukisikia viongozi na sisi tunasema lazima tuwe na uwajibikaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la muhimu kabla Waziri hajam-task meneja kufanya hivyo lazima ampe mamlaka. Meneja ambaye hana mamlaka akimwajibisha anamwonea, ayajue majukumu yake, lakini ampe rasilimali, atamwambiaje mtu atengeneze mradi aumalize kabla hajampa pesa on time, lakini atamwambiaje meneja atekeleze mradi aumalize wakati cheti alichonacho ni fake? Kwa hiyo, inaanzia hapo, lazima ajue hizo KPI anazitekelezaje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanachotofautina kitu kingine, lazima wafanye kitu kinaitwa TQM (Total Quality Management). Wasisubiri mwisho wa mwaka kuja kutupa matokeo, waende wana-monitor na yule atakayeshindwa apishe kando kusudi wengine waweze kuendelea na kazi. Kinyume cha hapo nakubaliana na dhana hiyo na kimsingi iliasisiwa hapa Tanzania ikaenda kutekelezwa kwenye nchi nyingine tunabaki kusoma kwenye makaratasi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze mambo 10 yatakayopewa kipaumbele au msukumo. Waziri wa Mipango anasema na tumeliona kwenye sekta kwamba ni kuendeleza kuwekeza katika kukuza uzalishaji kwa Sekta ya Kilimo na kuendelea kuweka uwekezaji katika Sekta ya Kilimo. Ninachoshauri Sekta ya Kilimo ichukue tafsiri asilia, tafsiri asilia ya kilimo ni crops, animal husbandry, livestock, pottery, aquaculture, pisciculture na forest, haya yote yanakwenda pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulizungumza na nilizungumza waziwazi kwamba hapa tukipachukua vizuri tunaweza kupata pato kwenye sehemu hizi inayofikia dola bilioni 12 za kuagiza nje bila kusahau kwamba hiki kilimo kwa mapana yake ndiyo kinatuwezesha kuwalisha Watanzania au kupata chakula mwaka mzima na tukaweza ku-export nje. Profesa nakuelekeza taratibu, unajua kama unatamani kwenda kusoma Ph.D, lazima Profesa amshughulikie taratibu, anaweza akalipiza, lakini tukiyasikiliza vizuri na hizo KPI hapa kuna uhakika wa kupata dola bilioni 12 na nilizungumza kwenye bajeti za kisekta.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la mkazo katika maendeleo vijijini na nimefurahishwa na matamko ya Mheshimiwa Waziri wa Mipango anasema anakwenda kukazia ujenzi au uhamasishaji wa viwanda vidogo vidogo. Ninawaomba Watanzania wasahau vyerehani, nyie katika viwanda vidogovidogo vyerehani ondoka, kwa sababu watu wengi unyanyapaa wao ni pale vyerehani kwamba ni viwanda, lakini niwaambie viwanda vidogo ni shule, huwezi kutoka hapa hujawahi kumiliki kiwanda ukapata kiwanda cha shilingi bilioni kumi ukakiendesha, haiwezekani ni utamaduni, it is a culture. Kwa hiyo, tunapokwenda kujenga viwanda vidogo vijijini maana yake tunajenga utamaduni wa watu wetu miaka ijayo waweze kuwa na utamaduni wa viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine; tunapojenga viwanda vidogo vijijini tunawa-retain wananchi vijijini na kupunguza tabia ya watu kuhamia mijini. Profesa Ndulu alisema kwamba, kijijini ukishaweka umeme, ukaweka barabara za TARURA panapendeka, lovable na pakishakuwa lovable panakuwa livable. Vitu vizuri viko vijijini, TARURA ameshafika, shule zimeshafika, VETA zimefika unakuja mjini kutafuta nini, ugongwe na gari? Kwa hiyo, naomba tuweke viwanda mambo yote yaweze kuishia vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze kuhusu NEDF; Profesa amezungumza suala la kuijenga upya SIDO nakubali na niwaambie wakiijenga SIDO vizuri kama nilivyoiacha wakaanzisha NEDF kama nilivyoiacha, mifuko yote itakwisha. Tofauti ya NEDF na mifuko mingine ni kwamba SIDO wanakupa pesa baada ya kukufundisha, unapohitimu wanakupa kiwanda. Ndio maana wakati ule tulianzisha industrial area wilaya zote, Mheshimiwa Magesa akiwa District Commissioner anakumbuka nilimpa saa 24 aanzishe industrial area akaianzisha. Kwa hiyo, lazima turudi kule wasione tatizo kutazamia, ule mwendo ulikuwa mzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie tozo kwenye gesi ya magari, tumekosea. Mheshimiwa Waziri, Omwana wa umukazi Mwigulu, anisikilize. Kwa nini anaweka pesa kwenye gesi? Kwa nini gesi? Watu wengi hawataki kuzungumza. Sisi kwetu gesi ni kinga, usalama na kwamba, endapo kuna tatizo kwenye ugavi sisi tutabaki salama. In case of disruption in supplies in the gas, we will be safe here.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa dawa ni kuhimiza Watanzania wawape gesi nyingi, wawape kichocheo, ili kusudi moja, tuwe salama kwenye vyombo vya usafiri. Pili, itakapotokea tatizo tutakuwa hatuna tatizo. Hata hivyo, wanapotafuta pesa mbona wanaziacha zinapita? Malori yote yanayopita hapa yanalipa ushuru au tozo? Kuna magari yanapakia mafuta Zambia yanakwenda kushusha mzigo Mombasa yanaharibu barabara za Bashungwa, kuna mengine yanatoka Rwanda, hawajui kwa nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtu haelewi nije nimweleze. namwomba Mheshimiwa Waziri alete wataalam wake nimweleze. Magari ni 400 na kama gesi ni nzuri, niliwaambia Mwaka 2023, ya Serikali ni mangapi? Juzi nimeona Prado tena namba A, Prado la namba TZA ndiyo linakuja limewekewa mtungi wa gesi, kwa nini hawakuweka kwenye hizi VXR? Kwa hiyo, namwomba ndugu yangu Mheshimiwa Waziri, hapo tumekosea. Hiyo shilingi 300 waiondoe, watu wote waingie tuwe salama na tatizo la mafuta, tukishakuwa salama tutajiweka taratibu. Nahitaji muda nimwoneshe pesa zilipo. Magari ya nje yanayopita hapa hayatupi mafuta hapa Tanzania na hatuna lolote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli nyingine ni kusaidia kuweka mazingira mazuri ya biashara, iko kwenye mpango. Ngoja niwaambie, kila export iwe formalized. Kuna watu wanatoka huko watokako wanaleta mitumba hapa, wanaipiga pasi, wanawapa ndugu zetu wakulima, wanawapa mchele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishawaambia tuna potential export ya mchele. Waziri wa Kilimo ameonesha mchele umekwenda juu hata kuliko kahawa. Sasa a-formalize pia, ili a-formalize wawawekee mazingira mazuri wakulima wa mpunga. Wasiwawekee withholding tax, wawapetipeti, wawawekee ma-godown kusudi mchele unapoondoka, wao wanaandika documents tunapata revenue inaingia ndani. Hata hivyo, wakiweka withholding tax mchele utahama saa 9.00 usiku na hawatakuwa na la kufanya na kwanza hawatauona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachukua fursa hii kumpongeza Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Bashe. Baada ya kuona kahawa inaondoka alikuja kutaka ushauri kwangu, nikamwambia akatafute ng’ombe wa maziwa awape walima kahawa, wanaotaka kuuza kahawa kwake wakalipe deni kwa maziwa, waweke mbolea kwenye mibuni halafu mibuni wamuuzie kwenye kahawa. Karagwe na Bukoba KDCU na KCU wamekubaliana na Bashe hakuna kahawa itakayovuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa natengeneza upande huu, naharibu upande ule. Tanzania kunapendeza, sasa mjomba itabidi alie kwa sababu, kahawa ya Tanzania hataipata. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri asitumie nguvu, atengeneze mazingira mazuri ya biashara, the easier of doing business, the blueprint, wakisome kile kitabu. asipende ganda lake, lakini the content matter.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia, kuandaa nguvu kazi kwa soko la dunia. Tunaanzisha Mitaala, Katibu Mkuu wangu wa zamani Waziri wa Sanyansi na Teknolojia, tumeandaa mitaala, ukiona inakuchelewesha ibadilishe, inaitwa radical change. Siyo lazima mchakato, unajua kuna mchakato na kuna radical change. Ukiona unachelewa badilisha. Kama Korea, wanataka nguvu kazi leo waulize wanataka nguvu kazi gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wamebahatika, watoto wetu wanafundishika. Aondoe magari VETA, afundishe vijana Wakorea wanataka nini? Apeleke vijana waende Korea. Hatuwezi kusubiri watoto wetu washindwe halafu tuhangaike. Mheshimiwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia, namweleza, nilimwomba karakana nne mojawapo ikiwa ya urembo, siyo biashara tena. Badilisha ya urembo, fundisha taaluma zinazotakiwa Korea na Ulaya, fundisha vijana wetu miaka sita, miaka minne, waende kutumika ulaya. Watarudi nyumbani wakati wa Eid au Christmas wakiwa wanaendesha magari yenye hali nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nirudie tena. Nimepata muda wa suala la magari yanayotoka nje. Tulifanya maamuzi kwa nia njema tukabadilisha road toll za kwetu. Waende wakapitie road toll na hiyo kuna dilemma kwa sababu, wakinywa mafuta mengi hapa utakuwa na deficit kwa kuwa, utatumia dola ku-import. Hata hivyo, wanaharibu barabara zetu, ni lazima tuwachakate, ili nao tuweze kuona inafanyikaje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo, nilipokuwa ninachangia niliunga mkono bajeti zote bila kuacha hata moja. Sasa ninapokuwa najumuisha nitakuwa kituko nitakaposhindwa kuunga mkono. Sijawahi kusoma bajeti nzuri au hotuba nzuri ya mipango kama ya safari hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti tu ya fedha imezungumza yenyewe. Pia, nachukua fursa hii Mheshimiwa Waziri, juzi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI amenipigia simu ananiambia shule anazonipelekea sasa, tuko tunahangaika na tunakubali hiyo. Hata hivyo, nilimlilia Waziri wa Fedha, lile soko langu waliloniahidi mwaka 2022 na wakamsainisha mkandarasi mpaka leo anasubiri advance; Mheshimiwa Waziri atafute advance yoyote aniwekee wepesi, yeye nimekwishamwekea wepesi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)