Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

Hon. Elibariki Emmanuel Kingu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya hizi dakika tano.

Mheshimiwa Spika, Afrika inakadiriwa kuwa na watu bilioni 1.5, kwa maana ya 1,500,000 na katika hiyo 60% ya population ya Afrika ni vijana walio chini ya miaka 25. Ukiangalia kwa mujibu wa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huu wa Mission Milioni 300 utagundua kwamba population ya watu milioni 185 ambao ni nguvu kazi ya Afrika wanasogezewa miundombinu ambayo itawasaidia kupata ajira katika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mchumi William Smith ana kitu anakiita invisible hand katika uchumi. Kwa maazimio haya yaliyofikiwa Dar es Salaam, nitumie nafasi hii kama Mbunge ninayetokana na wananchi wapendwa kabisa wa Singida Magharibi kusema kwamba Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi uliokaa wiki mbili zilizopita haujafanya makosa kumleta Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mgombea wao wa nafasi ya kiti cha Urais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiki alichokifanya Mheshimiwa Rais wetu, haya yalikuwa ni maazimio ya World Bank Group na African Development Group Aprili, 2024 walipoweka target ya kuwafikia watu milioni 300. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameionesha dunia, ameionesha Afrika kwamba yeye ni mwanamke shupavu, Rais jasiri, mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko duniani licha ya watu wengine wanaweza wakafikiri kwamba mataifa ya Afrika yanaweza yasioneshe uongozi duniani. Rais wetu ameli-prove hilo. Bunge hili hatuna sababu ya kuacha kumpongeza na kutoa azimio la kusimama naye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, angalia weledi wa Rais huyu. Ukitaka kuamini kuwa Rais huyu ni mweledi kwa jambo hili kubwa alilolifanya ambalo litakwenda ku-trigger kuleta employment, litakwenda ku-trigger kuongeza efficiency ya kazi na zaidi kubwa litakwenda kupunguza urban-rural migration kwa sababu watu wengi wa vijijini ambao kwa statistics hizi za dunia inaonesha watu milioni 185 watakwenda kufikiwa na huduma hii, wengi wao wakiwa vijana. Kwa hiyo, janga la ajira kwa vijana linakwenda kupatiwa ufumbuzi. Kwa nini Bunge hili lisimpongeze Rais huyu? Kwa nini Bunge hili lisiinuke na kusema ahsante kwa Rais huyu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kuamini kwamba Rais huyu ni mtu makini, ni mwanamke jasiri na shupavu angalia hata safu ya wasaidizi wake wanaomsaidia kazi, kuanzia kwa Mawaziri. Ona alivyo na safu ya Mawaziri walivyo humble. Nenda kwenye safu ya Waziri Mkuu na Msaidizi wake Naibu Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko pamoja na Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Angalia unyenyekevu wao namna wanavyomsaidia Rais huyu kufikisha ndoto waliyonayo ya kuwapatia Watanzania na sasa amekuwa mwangwi wa kuitangazia dunia na Afrika kwamba umeme utakwenda kuwasaidia Waafrika wengi na vijana kwenye ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninapotaja haya, tusimwache Naibu Waziri Mkuu ambaye ndiye sekta yake ameishikilia. Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu, hongera sana kaka yangu, wewe umekuwa mnyenyekevu, unamsaidia kaka yangu Mheshimiwa Majaliwa na ndiyo maana mageuzi makubwa ya kiuchumi yanafanyika kwenye Taifa hili kwa sababu mnampa Mheshimiwa Rais utulivu wa kufanya kazi. Mheshimiwa Majaliwa, kaka yangu hongera, Mheshimiwa Dkt. Biteko, kaka yangu hongera na mawaziri wote ninawapa hongera. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho lakini siyo kwa umuhimu, ukisoma data za dunia zinatuonesha kwamba kwa Tanzania peke yake, idadi ya kaya ambazo hazijafikiwa ambazo tukipiga mahesabu tutakapokuwa tumemaliza kuzifikia kaya zote uchumi wa Tanzania kwa projection inaonesha, Bara la Afrika ukianza kumega kidogo kidogo ukija katika ngazi ya Taifa mwaka 2050 Afrika inakwenda kuwa na population ya watu 2.5 billion.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo kwa idadi ya watu milioni 17 ambao watafikiwa na umeme wa uzalishaji hapa Tanzania inaonesha kwamba stimulation ya uzalishaji wa umeme kwa Taifa letu itakwenda kuongezeka mara kumi mpaka kufika 2050. Kwa nini tusiinuke na kusema ahsante Mama Samia? Kwa nini Bunge hili lisisimame na kusema pongezi Rais Samia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kwa sababu tumesema mama anaupiga mwingi, nasi Wana-CCM tumesema ndiye mgombea wetu na hilo halina mjadala. Kwa nini sasa Bunge hili pia mwakani tukija mapema tusiseme mitano tena kwa Spika wetu? Ama namna gani jamani? Kwa nini tumemaliza na mama, mwezi wa Kumi tunapokuja tunasema mitano tena kwa Mheshimiwa Dkt. Tulia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana. (Makofi)