Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

Hon. Livingstone Joseph Lusinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtera

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Ukweli ni kwamba ukilitazama Bunge lako lote, ni kwamba wote tunampongeza Mheshimiwa Rais na maneno yaliyokwishasemwa karibu yote ni maneno ambayo Mheshimiwa Rais anayastahili. Kinachobaki ni kuendelea kulijazia nyama tu Azimio la Bunge ambalo limeletwa hapa mbele yetu kwa ajili ya Mkutano wa Afrika uliopitisha Azimio la Dar es Salaam kwa ajili ya Nishati Safi kwa Bara zima la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati ule wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, lengo la Mkutano Mkuu lilikuwa ni kumfanya Rais atulie na aendelee kuwaza mambo makubwa na matunda yake ni haya. Itazame namna Serikali ilivyojipanga katika kukaribisha ule mkutano, lakini watu wanasema kama timu inacheza, halafu kocha anamwangalia mchezaji mmoja anamwingiza na yule mchezaji anayeenda kufunga goli la ushindi, sifa kubwa zinaenda kwa kocha.

Mheshimiwa Spika, unaweza ukaangalia namna Mheshimiwa Rais jicho lake lilivyomwona Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko kwamba anafaa kushika Wizara mbili kwa wakati mmoja. Ameingia na ameenda ku-score goli mwishoni kabisa zile dakika za jioni Tanzania inang’ara katika dunia na Afrika kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uliwasikia viongozi wa Benki ya Dunia (World Bank), ulisikia Benki ya Afrika, Benki ya East Africa, jumla kwa pamoja wanakusudia kuchangia shilingi trilioni 110 kwa ajili ya ku-solve matatizo ya umeme katika Afrika, lakini haya ni mawazo bora ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nini nataka kusema hapa? Kwa sababu pongezi nzito zimetolewa na Bunge hili na kwa mara ya kwanza tumeona Wabunge wa Upinzani wakiunga mkono jambo kubwa linalofanywa na Rais wetu. Tutegemee baada ya mwezi Oktoba malalamiko ya kura kuibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tuwe tayari kwa sababu kazi ya uchaguzi Rais ameshaimaliza, kwa hiyo, tutegemee watu wataanza kulalamika tumeibiwa kura, tumeibiwa kura, lakini siyo kuibiwa kura, mchezaji mwenyewe aliyepangwa pamoja na wasaidizi wake ndiyo hao mliowaona. Baraza zima la Mawaziri lina Mawaziri vijana ambao hawamwangushi Rais, lina wasaidizi wake; Waziri Mkuu pamoja na Naibu Mawaziri wamefanya kazi kubwa kabisa kuhakikisha viongozi wamefika na wameondoka wakiwa salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono Azimio hili. (Makofi)