Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, nami nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pia kabla ya kuanza, naunga mkono Azimio hili mapema kabisa kabla ya muda. Kikubwa ambacho napenda niongelee, tumefikaje hapa mpaka Mkutano Mkuu mkubwa kama huu unafanyika kwenye nchi yetu?

Mheshimiwa Spika, nakumbuka wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Hayati Rais Benjamin Mkapa alijikita sana kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na nyote ni mashahidi kipindi kile ndipo Serikali ya Tanzania iliunganisha barabara nyingi zaidi na kuanzia pale tumekuwa champions upande wa barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunapokuja kwenye suala hili la nishati, nishati safi na hii nyingine ambayo tunaitumia ya umeme ni lazima tumpe maua yake Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo amefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini ninayasema haya? Nakumbuka tarehe 15 Februari, 2023 tulishuhudia Mheshimiwa Rais akishuhudia utiaji wa saini ya mikataba ya kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo wadogo zaidi ya 336, lakini pampu za maji kwenye maeneo yetu mara nyingi tulikuwa na visima vya maji vilivyochimbwa, lakini hakukuwa na umeme; mikataba zaidi ya kupeleka pampu 399, vitongoji 1,522. Pamoja na hayo yote, ninapotaka kuelekea, uko mradi mmoja tumeupitisha hapa kitu kinaitwa gridi imara ya 4.4 trillion.

Mheshimiwa Spika, unapoongelea 4.4 trillion only kuboresha miundombinu ya umeme ambayo they are already existing, inaenda kuimarishwa ili umeme mpya huu unaokuja na huu tunaopelekwa kwa wananchi, wananchi waweze kupata umeme ule katika hali ambayo ni nzuri zaidi bila kukatikakatika na matatizo mengine ambayo yamekuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nyote ni mashahidi 2022/2023, tulipitisha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya mradi wa gridi imara, na ni mradi wa miaka minne. Kwa hiyo, 4.4 trillion achilia mbali miradi ya REA inayoendelea 4.4 trillion kwa ajili ya uboreshaji tu, siyo fedha ndogo. Kwa hiyo, unaweza kuona investment kubwa ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya kwenye suala la nishati ya umeme. Siyo kitu kidogo.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2024 tarehe 11 Mei amekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano uliofanyika Paris. Siyo kitu kidogo. Marais wako wangapi Dunia hii, aende yeye akawe Mwenyekiti Mwenza? Kwa hiyo, unayaona haya yamekuwa yana-flow mpaka delegation hii kubwa inakuja hapa Tanzania. Hayaja-flow kwa sababu ya kitu kingine, there is something ambacho wamekiona na hata wao wamekuja hapa wameshuhudia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nipo kwenye Bunge la Nchi za Maziwa Makuu, theme yetu ya mwaka 2024 ambayo tunaendelea nayo sasa hivi ilikuwa ni kuhimiza nchi za Afrika kwenye matumizi bora ya nishati safi ya kupikia, tunajivunia kilichofanyika hapa. Bahati nzuri tumekuwa mfano wa kuigwa kwenye kugawa mitungi ya gesi na vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, consultancy waliokuja kutoa maandiko yao pale walimtaja Rais Samia specifically kama mtu ambaye amesimama na mfano wa kuigwa kwenye kuondoa matumizi ya nishati inayohatarisha maisha na hatimaye tupo kwenye nishati safi ambayo ime-empower wanawake na wakataja mpaka hiyo mitungi 420,000 ambayo imeshagawiwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, ni kazi kubwa, wote tunajua tuna habari ya barabara, tuna habari ya miradi ya maji, tuna habari ya vituo vya afya, tuna habari ya hospitali za wilaya na mambo mengine lakini kitu hiki ambacho wengi hawakuwa wakikifikiria, leo tumekiona kinafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ugeni huu mkubwa ambao umekuja kutuletea heshima ya kibiashara na mambo mengine kwa sababu vyombo vya Kimataifa zaidi ya 78 vilirusha live broadcasting ya Mkutano huu, vyombo vya Kimataifa siyo kitu kidogo. Nchi imeenda viral sana hii na watu wengi wamejua kilichofanyika hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kipekee, kama Bunge na kama mwananchi ni lazima hili Azimio tulichukue na hata tutakapoenda huko wananchi wote wasimame na Bunge kwa sababu sisi ndiyo wawakilishi wao. Tulichokipitisha hapa tunakipitisha kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwamba kazi ilifanywa na Mheshimiwa Rais ni kubwa, Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kama wenzangu waliotangulia kusema, Chama cha Mapinduzi tarehe 19 tulimaliza hili jambo. Kwa hiyo, kikubwa tuombe Watanzania, tunapoongelea 2030 kumaliza habari ya umeme vijijini na vitongojini, ni miaka mitano ijayo ambayo Rais Dkt. Samia ndio atakuwa anamaliza na maua yake tunampa kuanzia mwaka huu mwezi Oktoba.

Mheshimiwa Spika kwa hiyo, ni lazima Watanzania wakubali kumuunga mkono. Wale ambao hawajafikiwa, tumetajiwa ni miaka mitano tu hii umeme utakuwa umefika kila sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nishati safi ya kupikia tumeambiwa ni 75% by 2030 itakuwa kila sehemu. Sasa ndugu zangu Watanzania wanaotusikiliza, wanafuatilia Bunge hili, ni kitu gani zaidi unaweza ukamdai mtu ambaye amejitoa kwa kila kitu akajaribu kugusa maisha ya wanawake? Leo kwa sababu by the way akiwa Makamu wa Rais alikuja na ajenda ya kumtua mwana mama ndoo, ajenda imeenda vizuri.

Mheshimiwa Spika, Waziri Aweso nadhani wakati Rais anahutubia Bunge ndiyo mtu pekee aliyeambiwa, “ukinizingua, nitakuzingua,” peleka maji. Tunaona maji yanaenda vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo habari ya umeme na nishati safi ya kupikia, akina mama wametolewa kwenye mikaa na kuni na by the way tunaotoka vijijini, tunajua watu wamekuwa wanaitwa wachawi kwa kusingiziwa, kisa tu ule moshi unamwingia mtu, wengine wamepoteza maisha, lakini vitu vyote hivi vinaenda kwisha na kila kitu kinaenda kuwa salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawaomba Watanzania, azimio tunalipitisha kama Bunge, lakini azimio hili ni lao kwa sababu Bunge ni la Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, nami naunga mkono Azimio hili. (Makofi)