Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

Hon. Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MISSION 300 ULIOFANYIKA DAR ES SALAAM TAREHE 27 - 28 JANUARI, 2025 NA KUHUDHURIWA NA WAKUU WA NCHI 21 ZA AFRIKA

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi tena na wakati huu nikiwa nimerudi nina furaha kubwa sana ndani ya Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Furaha niliyonayo ni kuona kila Mbunge aliyemo humu ndani anatamani kusema yale yote mazuri mema yaliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ninayo furaha na faraja kubwa, huko nje Watanzania wanasema, “Tuseme nini Bwana zaidi ya kushukuru?” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Watanzania na sisi tunasema, “Innallah maswaabirina.” Hakika kila mwenye kusubiri, yuko na Mwenyezi Mungu. Nasi Watanzania tuko na Mwenyezi Mungu, tunaisubiri Oktoba, 2025 tukampitishe Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kishindo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kuwashukuru Wabunge wote kwa kuwa walitamani kuchangia, lakini kwa sababu ya muda, nami pia sitatamani kuutumia muda wenu kwa kuwa mnadhamira na nia ya dhati na njema kwa Taifa letu kwa kuziunga jitihada za kiongozi huyu jemedari, mchapakazi, mahiri, mtulivu na mpenda maendeleo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, wamechangia jumla wachangiaji tisa, akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Sitatamani kupunguza wala kuongeza yale yote uliyotuambia kwa sababu ulikuwa ni sehemu ya mkutano huo na umetupa mrejesho ambao kila Mbunge na kila Mtanzania ameupokea.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo, Mheshimiwa Jesca Kishoa alisema, “Akina mama wako naye, wakina mama tuko naye.” Mimi napenda kusema, akina baba wako na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan; wazee wa Kitanzania wako na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan; na vijana wa Kitanzania wako na mwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, watoto wa Kitanzania leo wanaokalia majengo ambayo hayakuwahi kuwepo, ya kisasa vijijini, yenye umeme na vioo ambavyo vilikuwa vimezoeleka mijini, leo wanasema wako na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Vilevile, wakulima na wafugaji wa nchi hii wako na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema mwanzo, kwa sababu ya muda tunasema, “Innallah mashwabirina.” Tunasubiri Oktoba 2025, Mama Samia alale, sisi tuna deni naye. Kwetu sisi Watanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia kafanya. Tunakuombea kila la heri Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyezi Mungu akupe uzima na afya, Watanzania tumeona kwa mfano na kwa vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwetu sisi vijana ukiingia mtandaoni, nchi za jirani mitandaoni wanasema inafika lini tumpigie kura? Tunataka kuwahakikishia vijana wa nchi za jirani na wananchi wa nchi nyingine kwamba Watanzania tutaifanya kazi hiyo 2025 na ninyi mfanye kazi ya kupiga makofi na kuushangilia ushindi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, nichukue nafasi hii kukushukuru wewe mwenyewe kwa kuruhusu mjadala huu na kuruhusu hoja hii kuja hapa Bungeni kwa sababu wewe ni mama na una mapenzi mema na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa hoja. (Makofi)